Injili KILA SIKU

Injili KILA SIKU Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Injili KILA SIKU, Digital creator, Kilimanjaro, Same.

Karibu kwenye Injili Kila Siku 🙏
Tunashiriki Neno la Mungu kila siku kwa mafundisho mafupi, mahubiri na kutia moyo.
“Neno lako ni taa ya miguu yangu.” – Zaburi 119:105

Fedha ni chombo, lakini baraka hutoka kwa MUNGU.Usiombe pesa pekee, omba hekima, bidii na neema ya kuzalisha mafanikio y...
29/04/2026

Fedha ni chombo, lakini baraka hutoka kwa MUNGU.
Usiombe pesa pekee, omba hekima, bidii na neema ya kuzalisha mafanikio ya kweli.
MUNGU akifungua mlango, hakuna wa kuufunga. 🙏

Ukiwa na mizizi ndani ya Kristo, dhoruba za maisha haziwezi kukuangusha. Mkimbilie Yesu Leo
29/04/2026

Ukiwa na mizizi ndani ya Kristo, dhoruba za maisha haziwezi kukuangusha.
Mkimbilie Yesu Leo

TOBA YA KWELI 🤍Kulikuwa na kijana mmoja aliyeitwa Danieli. Alikulia katika maadili mazuri, lakini kadri alivyokua, alian...
20/04/2026

TOBA YA KWELI 🤍

Kulikuwa na kijana mmoja aliyeitwa
Danieli. Alikulia katika maadili mazuri, lakini kadri alivyokua, alianza kujiingiza kwenye marafiki wabaya na maisha ya anasa. Polepole, alijikuta amepoteza mwelekeo—alikuwa mbali na Mungu na hata familia yake ilianza kumchoka.
Siku moja alipata matatizo makubwa yaliyomfanya abakie peke yake bila msaada. Akiwa amekaa kimya usiku, alikumbuka maisha yake ya zamani na jinsi alivyokuwa na amani moyoni. Machozi yalimtoka, akasema, “Mungu, k**a bado unanipokea, ninarudi kwako.”
Alipochukua uamuzi huo, alianza kubadilika taratibu. Aliomba, akajitenga na marafiki waliomvuta chini, na kurudi kwenye njia sahihi. Haikuwa rahisi, lakini kila siku alihisi uzito ukiondoka moyoni mwake.
Baada ya muda, watu walishangaa kuona mabadiliko yake.

19/04/2026

Unastahili Kuabudiwa ��

19/04/2026

Bila Yesu ni Buree

19/04/2026

Uamsho ni Ajenda Yetu
by
Askofu Barnabas Mtokambali,
Askofu mkuu wa kanisa la T.A.G

“Usisimame katikati ya safari…hata ukichoka, songa mbele kidogo kidogo.Hatua zako ndogo leo ndizo ushindi wa kesho.” 💪✨
19/04/2026

“Usisimame katikati ya safari…
hata ukichoka, songa mbele kidogo kidogo.
Hatua zako ndogo leo ndizo ushindi wa kesho.” 💪✨

KILIO CHA SIRI KINASIKIKA MBINGUNIKulikuwa na mwanamume mmoja aliyeitwa Musa.Kwa nje alionekana ana nguvu, anacheka na w...
19/04/2026

KILIO CHA SIRI KINASIKIKA MBINGUNI

Kulikuwa na mwanamume mmoja aliyeitwa Musa.
Kwa nje alionekana ana nguvu, anacheka na watu, anaonekana yupo sawa…
Lakini ndani alikuwa anapitia maumivu makubwa sana.
Alikuwa na madeni, familia inamtegemea, na hakuna aliyejua anachopitia.
Kila usiku alipokuwa peke yake, alikaa kimya…
Machozi yakimtiririka taratibu…
Hakuna aliyemuona. Hakuna aliyemsikia.
Siku moja akiwa amechoka sana, alipiga magoti chumbani kwake akasema:
"Mungu… sina nguvu tena. K**a utanisaidia, ni sasa."
Hakuna kilichotokea papo hapo…
Hakuna sauti ilisikika…
Lakini moyoni alipata amani ndogo sana.
Kesho yake, alipigiwa simu na mtu ambaye hakuwa ameongea naye kwa muda mrefu.
Akamwambia:
"Nilihisi nikukumbuke… kuna nafasi ya kazi hapa, njoo ujaribu."
Musa alishangaa.
Akaenda… akapata nafasi.
Polepole maisha yakaanza kubadilika.
Siku moja alikaa peke yake akakumbuka yale machozi yake ya usiku…
Akatabasamu na kusema:
👉 “Kumbe kilio changu cha siri, Mungu alikisikia.”
UJUMBE:
Kuna maombi ambayo hayana kelele…
Lakini yana nguvu kubwa mbele za MUNGU
👉 Usinyamaze moyoni ukadhani uko peke yako
👉 Mungu anasikia hata yale usiyowaambia watu
👉 Kilio chako si bure

MLANGO ULIOFUNGWA NI ULINZIKulikuwa na mwanamke mmoja aliyeitwa Rehema.Alitamani sana kupata kazi fulani kubwa aliyoiomb...
19/04/2026

MLANGO ULIOFUNGWA NI ULINZI

Kulikuwa na mwanamke mmoja aliyeitwa Rehema.
Alitamani sana kupata kazi fulani kubwa aliyoiombea kwa muda mrefu.
Alifunga na kuomba, akaamini kabisa kuwa hiyo ndiyo ilikuwa nafasi yake.
Siku ya majibu ilipofika… alikataliwa.
Alilia sana.
Alimlalamikia Mungu:
"Kwa nini umeniacha? Nilikuamini!"
Wiki chache baadaye, alipata kazi nyingine ndogo ambayo hakuipa thamani sana.
Lakini kwa sababu ya hali, akaikubali.
Miezi michache ikapita…
Habari zikaja—ile kampuni aliyokuwa anatamani kuajiriwa ilifungwa ghafla kutokana na matatizo makubwa ya kifedha.
Watu waliokuwa wameajiriwa pale walipoteza kazi.
Rehema aliposikia hilo… alinyamaza.
Akatambua kitu kikubwa:
👉 Kukataliwa kwake kulikuwa ni ulinzi, siyo hasara.
Alipiga magoti akasema:
"Mungu, samahani… nilidhani umenifungia mlango, kumbe ulikuwa unaniokoa."
UJUMBE:
Si kila mlango unaofungwa ni mbaya.
Mengine Mungu anayafunga ili kukulinda na kile usichokiona

👉 Ukikataliwa, usikate tamaa
👉 Mungu anaona mbali kuliko wewe
👉 Unacholia leo, kesho utashukuru kwa nini kilifungwa

18/04/2026

Siri ya Mafanikio
by
Rv.Nimrod Swai

Address

Kilimanjaro
Same
0000

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Injili KILA SIKU posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share