Maxaga_TheGiant

Maxaga_TheGiant Become wiser. Use your knowledge to understand and solve problems at your local area.

02/04/2026

Kwa wale waliopata kusoma historia au kusikia hadithi za makabila, hasa ya Wasukuma na Wanyamwezi, hawakukosa kusikia habari ya Ng’wanamalundi.
Mtu huyo aliyewahi kuutingisha utawala wa Wajerumani, alizaliwa katika ukoo wa kawaida akiwa mcheza ngoma mashuhuri, mwaka wa kuzaliwa kwake haufahamiki ila alifariki dunia mwaka 1936, akiwa tayari mtu mzima.

Watu wengi wamekuwa wakimjadili kwa maoni tofauti, wengine wakimsifu k**a shujaa huku wengine wakihusisha uwezo wake na nguvu za giza.
Katika makala hii usahihi wa historia yake unaelezwa na mjukuu wake wa pili, Kishosha Sitta (80) mkazi wa Kijiji cha Mwalugulu wilayani Kahama mkoani Shinyanga, anayesimulia alivyomfahamu babu yake huyo.

Sitta anaanza kueleza kuwa jina halisi la babu yake halikuwa Ng’wanamalundi bali lilikuwa Igulu Bugomola, ambaye alizaliwa katika Kijiji cha Mwakubunga Nera wilayani Kwimba mkoani Mwanza.

Ng’wanamalundi alikuwa mtoto pekee wa kiume na wa mwisho kati ya wanne, kwa baba yake Bugomola na mama yake, Ngolo Igulu.
Sitta anasema Igulu (Ng’wanamalundi), alikuwa na tabia ya uzururaji tangu utotoni na mara nyingi haikuwa rahisi kumkuta nyumbani. Alikuwa mashuhuri kutokana na umahiri wake wa kucheza ngoma na mara nyingi alipokuwa akitembea mitaani alifuatwa na kundi kubwa la watoto.

“Hali hiyo iliwachukiza wazazi wengi wenye watoto waliokuwa wakiambatana naye, kiasi cha kumchukia hata Ng’wanamalundi mwenyewe, kutokana na watoto wengi hasa waliokuwa wakitoka familia za wafugaji kutoweka na hiki kilikuwa chanzo cha mifugo mingi kupotea baada ya kutelekezwa na watoto hao,” anasema Sitta.

Hali ya kuchukiwa kwa Ng’wanamalundi ilienea pale kijijini kiasi cha kuanza kumkebehi, hasa kutokana na umbo lake refu na miguu yake myembamba kuanzia magotini hadi kwenye makanyagio, ikiwa mirefu kuliko kawaida.
Sitta anasema hali hiyo ilisababisha kumdhihaki na kumwongezea chuki zaidi kwa wanakijiji wa eneo hilo waliodiriki kumtukana kwa lugha ya Kisukuma; “Mamirundi galyo lilihumbura bana bise” ikiwa na maana

07/01/2026
2023. At Arusha
31/12/2025

2023. At Arusha

2016. At Kilole Korogwe Tanga
31/12/2025

2016. At Kilole Korogwe Tanga

Wishing U All The Best Cathryn
31/12/2025

Wishing U All The Best Cathryn

Happy 2026 Wherever You Are
31/12/2025

Happy 2026 Wherever You Are

Make Sure Everything Goes Smoothly In 2026Yom TeruahRosh Hashanah
31/12/2025

Make Sure Everything Goes Smoothly In 2026
Yom Teruah
Rosh Hashanah

Address

Kahama
Shinyanga

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Maxaga_TheGiant posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share