Snadareal Tv

Snadareal Tv Snadareal Tv ni jukwaa la habari na Taarifa mbalimbali ya kijamii, Kiuchumi, Siasa Michezo Burudani

08/08/2026
MKURUGENDEZI WA SNADAREAL TV ASHIRIKI MBIO ZA MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA ITIGIMkurugenzi wa Snadareal TV John Hassan...
22/07/2026

MKURUGENDEZI WA SNADAREAL TV ASHIRIKI MBIO ZA MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA ITIGI

Mkurugenzi wa Snadareal TV John Hassan ameshiriki Mbio za Mwenge wa Uhuru mapema leo Julai 22, 2026 katika Halmashauri ya Itigi, Wilaya ya Manyoni mkoani Singida. Ushiriki huo umeonyesha dhamira ya chombo hicho ya kuendelea kuwa sehemu ya matukio muhimu ya kitaifa yanayolenga kuhamasisha maendeleo, uzalendo na mshikamano miongoni mwa Watanzania.

Mbio hizo ziliongozwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026, Ndugu Wazo Mwang’onda, ambaye ameendelea kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuhimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli zinazochochea ustawi wa jamii na maendeleo ya Taifa.

Kupitia ushiriki wake, Mkurugenzi wa Snadareal TV ameendelea kuthibitisha dhamira ya chombo hicho cha habari ya kuwa karibu na wananchi kwa kuripoti matukio muhimu yanayogusa maendeleo ya jamii. Snadareal TV inaendelea kutekeleza jukumu lake la kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha kwa kuifikia jamii kwa habari za ukweli na uhakika.
https://www.instagram.com/p/DbF3l5Rjo3v/?igsh=MXM3djdyZzhmbnlqcw==

18/07/2026

NARINA EMPIRE SOFT OPENING SINGIDA

11/07/2026

MSANII MOO CLASSIC SINGIDA ICON AZUNGUMZIA SUALA LA YEYE KUWA MSANII ANAYEENDESHA BODA BODA

BALOZI LAZARO NYALANDU AIPONGEZA SNADAREAL TV KWA KUIBUKA MSHINDI MDAU SHUPAVU AWARD BEST DIGITAL MEDIA PLATFORM.Balozi ...
06/07/2026

BALOZI LAZARO NYALANDU AIPONGEZA SNADAREAL TV KWA KUIBUKA MSHINDI MDAU SHUPAVU AWARD BEST DIGITAL MEDIA PLATFORM.

Balozi na Mshauri wa Rais Masuala ya Diplomasia, Balozi Lazaro Nyalandu, ameipongeza Snadareal TV kwa kuibuka mshindi wa Tuzo za Mdau Shupavu Awards 2026 katika kipengele cha Best Digital Media Platform, akieleza kuwa ushindi huo ni uthibitisho wa mchango mkubwa wa chombo hicho katika kuhabarisha jamii na kuhamasisha maendeleo ya Mkoa wa Singida na Taifa kwa ujumla.

Tuzo hizo zilitolewa Mei 25, 2026 katika Ukumbi wa Aqua Vitae Resort, mkoani Singida, chini ya uratibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Holly Smile, Arnold Bweichum. Kwa mujibu wa Balozi Nyalandu, mafanikio hayo yametokana na juhudi, ubunifu na weledi wa Snadareal TV katika kuwasilisha habari zenye maslahi kwa wananchi.

Akizungumza mapema mwezi Julai 2026 alipokutana na Mkurugenzi wa Snadareal TV, John Hassan, Balozi Nyalandu alisema amekuwa akifuatilia kwa karibu kazi zinazofanywa na chombo hicho, ambazo zimeendelea kuhabarisha wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii, kiuchumi na maendeleo, hususan ndani ya Mkoa wa Singida.

“Nimekuwa nikishuhudia kwa karibu kazi kubwa inayofanywa na Snadareal TV katika kuhabarisha wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii, kiuchumi na maendeleo mkoani Singida na nchini. Ushindi huu ni motisha wa kuendelea kufanya kazi kwa weledi na ubunifu zaidi,” alisema Balozi Lazaro Nyalandu.

Aidha, Balozi Nyalandu alimtakia kila la heri Mkurugenzi wa Snadareal TV pamoja na timu nzima ya chombo hicho, akiwahimiza kuendelea kusimamia maadili ya taaluma ya uandishi wa habari na kutumia jukwaa lao kuhabarisha umma kwa usahihi, uwajibikaji na uzalendo huku wakichochea maendeleo ya jamii.
https://www.instagram.com/p/DabgdV1DOg0/?igsh=amE3Zzk4YXFyenBz

05/07/2026

WANAFUNZI WA S/M UNYAMIKUMBI MIAKA YA 1970'S WARUDISHA FADHILA KWA JAMII, WAJITOLEA KUKARABATI JENGO LA DARASA WALILOSOMEA

Follow account hii kwa habari mbalimbali za Ndani na Nje ya nchi 🌐🌐🌐
03/07/2026

Follow account hii kwa habari mbalimbali za Ndani na Nje ya nchi 🌐🌐🌐

21.9k Followers, 5 Following, 152.0k Likes - Watch awesome short videos created by SNADAREAL TV

25/06/2026

RC DENDEGO AIPONGEZA TAKUKURU MKOA WA SINGIDA KWA KUOKOA FEDHA
ZA SERIKALI KATIKA MIRADI

23/06/2026

MSANII ALIKIBA WA SINGIDA AELEZA
ALIVYOSOTA LOCK UP KISA MSANII ALIKIBA, AFUNGUKA KWA MAUMIVU MAKALI

19/06/2026

Kazi kazi kazi na Nyuki✅

Address

Singida

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Snadareal Tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category