Kusini News

Kusini News Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Kusini News, News & Media Website, Songea.
(2)

PATA HABARI NA MAKALA MBALIMBALI ZA KUVUTIA KIDIJITALI KUTOKA KATIKA VIJIJI,HALMSHAURI,WILAYA,MIKOA,KITAIFA NA KIMATAIFA KUPITIA KUSINI MEDIA KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIMU 0784765917 BARUAPEPE [email protected]

RAS RUVUMA AVUTIWA NA UBUNIFU TUNDURU DC, ASISITIZA TEKNOLOJIA NA UONGEZAJI THAMANI KUKUZA UCHUMITeknolojia, ubunifu na ...
05/08/2026

RAS RUVUMA AVUTIWA NA UBUNIFU TUNDURU DC, ASISITIZA TEKNOLOJIA NA UONGEZAJI THAMANI KUKUZA UCHUMI

Teknolojia, ubunifu na uongezaji thamani vinaendelea kuwa nguzo za mapinduzi ya kilimo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Wakili Mary Makondo,ametembelea Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea Viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya.

Akiwa katika banda hilo Bi. Makondo alipokea maelezo kuhusu teknolojia za kisasa na mbinu bora zinazotumiwa na Tunduru DC kuongeza uzalishaji na tija katika sekta za kilimo na mifugo.

Pia alitembelea mabanda ya wajasiriamali na kujionea bidhaa zinazozalishwa na kusindikwa wilayani humo, akipongeza juhudi zao za kuongeza thamani ya mazao na kuchochea uchumi wa ndani.

Ziara hiyo inaakisi dhamira ya Mkoa wa Ruvuma ya kuhamasisha matumizi ya teknolojia, ubunifu na ushiriki wa wadau katika kuimarisha kilimo, mifugo na ujasiriamali, sambamba na kaulimbiu ya Nanenane 2026: “Tambua Soko; Ongeza Tija Kutekeleza Dira 2050.”

KILIMO, LISHE NA ASALI VYATAJWA KUWA NGUZO YA UCHUMI WA BAADAYEJe, Ruvuma iko tayari kugeuza kilimo kuwa injini ya uchum...
05/08/2026

KILIMO, LISHE NA ASALI VYATAJWA KUWA NGUZO YA UCHUMI WA BAADAYE

Je, Ruvuma iko tayari kugeuza kilimo kuwa injini ya uchumi na lishe bora? Hilo ndilo lililopewa msukumo baada ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Wakili Mary Makondo, kutembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Bi. Makondo aliwataka Maafisa Lishe wa Halmashauri ya Mbinga kuongeza elimu ya lishe bora hadi vijijini ili kupunguza udumavu na kuimarisha afya ya watoto.
Pia alisisitiza uongezaji thamani wa mazao na kupanua biashara ya bidhaa za kahawa nje ya Mbinga ili kufungua masoko mapya na kuongeza ajira kwa vijana.

Katika hatua nyingine, aliutaka uongozi wa Halmashauri kuwekeza kwenye mizinga ya kisasa ili kuongeza uzalishaji wa asali na kukuza uchumi wa wafugaji nyuki.
Maonesho ya Nanenane yanaendelea kukutanisha halmashauri, taasisi na wadau mbalimbali wakionesha teknolojia na fursa za uwekezaji katika kilimo, mifugo, uvuvi na ujasiriamali.

Hakuna ubishi maendeleo ya Ruvuma yatajengwa kupitia kilimo chenye tija, lishe bora na uwekezaji unaoongeza thamani ya mazao

05/08/2026

MFAHAMU BINTI NDEMBO MGANGA WA JADI WA KURITHI ALIYEPATA UMAARUFU TANZANIA NA AFRIKA
Binti Ndembo amefungua kituo chake katika kijiji cha Mtwarapachani wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma
Fuatilia sehemu ya nne ya makala ya Binti Ndembo

05/08/2026

MFAHAMU BINTI NDEMBO MGANGA WA JADI WA KURITHI ALIYEPATA UMAARUFU TANZANIA NA AFRIKA
Binti Ndembo amefungua kituo chake katika kijiji cha Mtwarapachani wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma
Fuatilia sehemu ya tatu ya makala ya Binti Ndembo

05/08/2026

MFAHAMU BINTI NDEMBO MGANGA WA JADI WA KURITHI ALIYEPATA UMAARUFU TANZANIA NA AFRIKA
Binti Ndembo amefungua kituo chake katika kijiji cha Mtwarapachani wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma
Fuatilia sehemu ya pili ya makala ya Binti Ndembo

05/08/2026

MFAHAMU BINTI NDEMBO MGANGA WA JADI WA KURITHI ALIYEPATA UMAARUFU TANZANIA NA AFRIKA
Binti Ndembo amefungua kituo chake katika kijiji cha Mtwarapachani wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma
Fuatilia sehemu ya kwanza ya makala ya Binti Ndembo

Royal Tour pamoja na watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwenye Mto Rufiji, Hifadhi ya Taifa ya Nyerere jana.
05/08/2026

Royal Tour pamoja na watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwenye Mto Rufiji, Hifadhi ya Taifa ya Nyerere jana.

Raslimali adimu kutoka kusini Wanapatikana kigogo landabar Dsm soko jipya la kabichi kwa +255755238159
05/08/2026

Raslimali adimu kutoka kusini Wanapatikana kigogo landabar Dsm soko jipya la kabichi kwa +255755238159

SERIKALI YAIMARISHA ULINZI WA MAFUTA NCHINI HUKU MGOGORO WA MASHARIKI YA KATI UKITIKISA SOKO LA DUNIAWakati mgogoro wa M...
05/08/2026

SERIKALI YAIMARISHA ULINZI WA MAFUTA NCHINI HUKU MGOGORO WA MASHARIKI YA KATI UKITIKISA SOKO LA DUNIA

Wakati mgogoro wa Mashariki ya Kati ukiendelea kuathiri usafirishaji wa mafuta duniani, Serikali imeanza kuchukua hatua za kuimarisha usalama wa upatikanaji wa mafuta na kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa na akiba ya kutosha ya nishati.

Akiongoza kikao kazi Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, alisema Serikali imeweka mikakati madhubuti ya kulinda usambazaji wa mafuta nchini kufuatia changamoto zinazoendelea katika soko la kimataifa, ikiwemo athari zilizotokana na kufungwa kwa njia ya usafirishaji kupitia Mlango Bahari wa Hormuz, mojawapo ya njia muhimu zaidi za biashara ya mafuta duniani.

Kikao hicho kiliwakutanisha viongozi wakuu wa sekta ya mafuta na gesi, akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati (Mafuta na Gesi), Dkt. James Mataragio; Kamishna wa Mafuta, Bw. Godluck Shirima; Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Bw. Salum Mnuna; Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Bw. M***a Makame; na Mkurugenzi Mtendaji wa PBPA, Bw. Erasto Simon, kwa lengo la kuimarisha uratibu na utayari wa sekta hiyo.

05/08/2026

BEI YA MAHINDI YAWATIA WASIWASI WAKULIMA SONGEA WAIOMBA SERIKALI KUFUNGUA HARAKA SOKO LA NFRA

Wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma, wameitaka Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kuharakisha kutangaza bei elekezi na kuanza ununuzi wa mahindi kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), wakisema kuchelewa kwa zoezi hilo kunawalazimu kuuza mazao kwa hasara.

Wakizungumza katika mikutano ya Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Dkt. Lazaro Komba Bunungu, wananchi walisema mahindi ndiyo tegemeo kuu la uchumi wa familia nyingi, lakini kwa sasa kilo moja inauzwa kati ya Shilingi 300 hadi 400, huku gunia la kilo 100 likiuzwa Shilingi 30,000 hadi 40,000, kiwango wanachodai hakilingani na gharama za uzalishaji.

Akijibu hoja hizo, Dkt. Lazaro Komba Bunungu alisema Serikali ipo katika hatua za mwisho za kuanza ununuzi wa mahindi kupitia NFRA.
Alikumbusha kuwa Juni 20 aliliomba Bunge kuhakikisha NFRA inapanga bei yenye tija ili kulinda maslahi ya wakulima na kuongeza mchango wa sekta ya kilimo .

Address

Songea

Telephone

+255784765917

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kusini News posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Kusini News:

Shortcuts

Share