
17/08/2023
TAMBUA MAANA YA TAFSIRI YA KISHERIA YA KOSA LA UHAINI LILIVYOTAFSIRIWA KWENYE SHERIA ZA TANZANIA NA UMUHIMU WAKE WA KIKATIBA WA KUIREKEBISHA AU KUTOIREKEBISHA.
Kwa kufuata sheria za Tanzania kifungu cha 39 ( 1 ) cha kanuni za adhabu kinahukumu kuwa mtu yeyote ambaye yumo ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote, kujaribu kumuua Rais, kuanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano, kusababisha, kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kuhusu kifo, kumlemaza, kumzuia, kufungwa kwa Rais.
Kumwondolea Rais heshima na jina la mkuu wa nchi, amiri jeshi mkuu, au kiongozi wa serikali, kupindua serikali iliyo madarakani, kutishia serikali, bunge au mahak**a kwa makosa haya na yale yaliyotajwa hapo juu mtu wa namna hiyo atakuwa ametenda kosa la jinai ambalo ni kosa la uhaini
Kwa kufuata sheria za Tanzania imehalalishwa kuhukumu kifo kwa raia yeyote atakaye wekwa hatiani kwa kosa la uhani kulingana na kifungu cha sheria namba 39 na 40 cha kanuni ya adhabu.
Watanzania tuwe makini kwenye hotuba zetu za kisiasa tunazozielimisha kwenye umma wa watanzania ili zisikiuke sheria za nchi na kusababisha tuhukumiwe kifo kwa kosa la uhaini.
Kupinga makosa yaliyofanyika kwenye mkataba wa bandara siyo kosa la jinai wala siyo kosa la uhaini. Pia kufanya maandamano ya kupinga makosa yaliyofanyika kwenye mkataba wa bandara siyo kosa la jinai wala siyo kosa la uhaini. Hapa inamaanisha kuwa kupinga makosa ya serikali na viongozi wake siyo kosa la uhaini.
Bali kwa mujibu wa kanuni za adhabu ya kifungu cha sheria namba 39 na 40 ni kosa la uhaini kuangusha mamlaka ya urais kinyume cha sheria za nchi na za kikatiba, ni kosa la uhaini kuangusha taasisi ya urais kinyume cha sheria za nchi na za kikatiba, ni kosa la uhaini kuangusha mamlaka ya bunge, ni kosa la uhaini kuangusha mamlaka ya mahak**a, ni kosa la uhaini kuangusha mamlaka ya viongozi wa serikali na pia ni kosa la uhaini kuiondolea heshima serikali na viongozi
Kwa hiyo basi kwa kufuata sheria za Tanzania imebainika kuwa serikali ya Tanzania kamwe haiwezi kuangushwa kwa njia ya maandamano, au kwa njia ya kuikosesha heshima serikali na viongozi wake kwa sababu kufanya hivyo ni kosa la uhaini.
Swali linakuja, je ni aina gani ya ukosoaji dhidi ya makosa ya serikali na viongozi wake ambao hautaikosesha heshima serikali na viongozi wake? Je hatuoni umuhimu wa kurekebisha sheria hiyo inayotafsiri kosa la uhaini na hukumu yake? Naomba majibu yenu.
Kwa maswali na ushauri nipigie 0757559876.
Ni mimi Doctor Claudius Haule Ligendayika