Saza tv

Saza tv Kwa matangazo ya biashara Piga +255654525654 Karibuni
(2)

JE TANZANIA TUTAWEZA KWELI KURUSHA SATTELITE?Nchi zote za Africa zilizowahi kurusha sattelite, zimekuwa zikitumia makamp...
07/08/2025

JE TANZANIA TUTAWEZA KWELI KURUSHA SATTELITE?

Nchi zote za Africa zilizowahi kurusha sattelite, zimekuwa zikitumia makampuni ya nje kwenye kurusha, na hata sehemu ya kurushia huwa ni huko huko nje ya bara la Africa.

Hizi ndizo Kampuni ambazo Ilihusika kurusha sattelite za Africa

NCHI: Kenya
JINA LA SATTELITE: 1KUNS-PF
JINA LA ROCKET ILIYORUSHA: SpaceX Falcon 9 (CRS-14)
TAASISI ZILIZOHUSIKA: Chuo Kikuu cha Nairobi, Kenya Space Agency, JAXA
MWAKA: 2018
MAHALI ILIPORUSHIWA: Kennedy Space Center, USA

---

NCHI: Ghana
JINA LA SATTELITE: GhanaSat-1
JINA LA ROCKET ILIYORUSHA: SpaceX Falcon 9 (CRS-11)
TAASISI ZILIZOHUSIKA: All Nations University, Kyutech
MWAKA: 2017
MAHALI ILIPORUSHIWA: Kennedy Space Center, USA

---

NCHI: Nigeria
JINA LA SATTELITE: NigComSat-1
JINA LA ROCKET ILIYORUSHA: Long March 3B (China)
TAASISI ZILIZOHUSIKA: NIGCOMSAT Ltd, CGWIC
MWAKA: 2007
MAHALI ILIPORUSHIWA: Xichang Satellite Launch Center, China

---

NCHI: Angola
JINA LA SATTELITE: AngoSat-1
JINA LA ROCKET ILIYORUSHA: Zenit-3SL
TAASISI ZILIZOHUSIKA: RSC Energia, Ministry of Telecommunications (Angola)
MWAKA: 2017
MAHALI ILIPORUSHIWA: Sea Launch Platform, Pacific Ocean

---

NCHI: Ethiopia
JINA LA SATTELITE: ETRSS-1
JINA LA ROCKET ILIYORUSHA: Long March 4B
TAASISI ZILIZOHUSIKA: ESSTI, China Academy of Space Technology
MWAKA: 2019
MAHALI ILIPORUSHIWA: China

---

NCHI: Misri
JINA LA SATTELITE: EgyptSat-1
JINA LA ROCKET ILIYORUSHA: Dnepr Rocket
TAASISI ZILIZOHUSIKA: National Authority for Remote Sensing and Space Sciences
MWAKA: 2007
MAHALI ILIPORUSHIWA: Baikonur Cosmodrome, Kazakhstan

---

NCHI: Afrika Kusini
JINA LA SATTELITE: SUNSAT
JINA LA ROCKET ILIYORUSHA: Delta II
TAASISI ZILIZOHUSIKA: Stellenbosch University
MWAKA: 1999
MAHALI ILIPORUSHIWA: Vandenberg Air Force Base:
Credit Za Jamii

*VITU VITATU DUNIANI AMBAVYO HATUTOVIONA MPAKA TUNAINGIA MAKABURINI*Yeah! Umesoma vizuri kabisa. Unaonaje kukiwa na kitu...
07/08/2025

*VITU VITATU DUNIANI AMBAVYO HATUTOVIONA MPAKA TUNAINGIA MAKABURINI*

Yeah! Umesoma vizuri kabisa. Unaonaje kukiwa na kitu ambacho unaambiwa hutakiwi kukiona mpaka mwaka fulani? Tena mwaka ambao unaamini hautokuwa duniani?

Utafanyaje? Utahisi vitu hivyo vina nini? Kwa nini vimefanywa siri mpaka miaka ya mbele ambayo wewe na mimi hatutokuwa hai? Unajua ni vitu gani? Hebu visome hapa chini.

1. Kabla ya kifo chake, malkia Elizabeth alimwandikia barua Mayor wa Sydney nchini Australia na juu ya bahasha akaandika: ‘Tafadhali usiifungue barua hii mpaka mwaka 2081’.
Hakuna mtu anayejua kuna kitu gani kimeandikwa ndani ya barua hiyo na pia hakuna anayejua sababu ya malkia Elizabeth kufanya kitu k**a hicho. Kwa nini barua isiruhusiwe kufunguliwa sasa hivi na wakati hata mtu aliyeandikiwa inawezekana asifike mwaka uliotajwa?
Barua hiyo imewekwa kwenye vault maalumu huko Sydney na hakuna mtu anayeruhusiwa kufungua na kuisoma barua hiyo.

2. Kitu cha pili ni kwamba mwaka 2015 kulikuwa na filamu iliyoitwa 100 Years ambayo iliigizwa na muigizaji maarufu John Malkovich ambayo imetolewa taarifa kwamba hiyo muvi haitakiwa kuonyeshwa mahali popote pale mpaka tarehe 18/November/ 2115 (Miaka 100) baada ya kuigizwa. Filamu hiyo itaonyeshwa mwaka huo katika Onyesho la filamu la Cannes.Filamu inahusu nini? Hakuna anayejua.

3. Unamkumbuka mke wa rais John F. Kennedy wakati mumewe alipouawa alikuwa ndani ya gari akishuhudia? Unaikumbuka ile suti ya pinki aliyoivaa ambayo ilimwagikiwa damu ya mumewe?
Sasa baada ya tukio hilo, ile suti ilichukuliwa na kuhifadhiwa mahali ambapo hakuna mtu yeyote yule anayeruhusiwa kuiona mpaka ifikapo mwaka tarehe 26/10/22103.
Kwa nini mambo haya matatu yamefichwa? Kwa nini yatatolewa katika kipindi ambacho asilimia kubwa tutakuwa makaburini? Hakuna ajuaye.

Vika Media ✍🏿
C&p

Aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Kongwa, Job Yustino Ndugai amefariki Dunia leo August 06,2025 akiwa an...
06/08/2025

Aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Kongwa, Job Yustino Ndugai amefariki Dunia leo August 06,2025 akiwa anaendelea kupatiwa matibabu Hospitalini baada ya kuugua ghafla.

Ndugai amekuwa Spika wa Bunge tangu November 17, 2015 hadi Januari 06, 2022 alipojiuzulu na kuendelea kuwa Mbunge wa Kongwa nafasi ambayo ameendelea kuitetea kwa kuchukua fomu tena mwaka huu ambapo ameshinda kwenye kura za maoni.

Ndugai ambaye amezaliwa January 22,1960 alishinda kura za maoni za Ubunge wa Jimbo la Kongwa kwa kupata kura 5690.

RUBANI WA PABLO ESCOBAR: Nilikuwa na Lamborghin 30Nadhani ushawahi kusikia mengi kuhusu mwanaume aliyejulikana kwa jina ...
06/08/2025

RUBANI WA PABLO ESCOBAR: Nilikuwa na Lamborghin 30

Nadhani ushawahi kusikia mengi kuhusu mwanaume aliyejulikana kwa jina la Pablo Escobar ambaye alifariki dunia kwa kupigwa risasi mwaka 1988.

Kuna stori nyingi kuhusu huyu mwamba, alikuwa akiingiza dola milioni 70 kila siku, yaani kwa wiki aliingiza zaidi ya dola milioni 490 (Hiyo ni kutoka kwa maelezo ya mtoto wake)

K**a ushamsikia sana huyo mwamba, basi leo acha nikuletee stori kuhusu mchizi ambaye alikuwa akipiga kazi zake za kusafirisha madawa hayo kwenda sehemu mbalimbali kwa kutumia ndege binafsi.

Anaitwa Tirso ‘TJ’ Dominguez, aliwahi kuwa rubani wa muuza madawa ya kulevya maarufu, Pablo Escobar kutoka nchini Colombia amefunguka kwa mara ya kwanza tangu miaka ya 1980 ambapo alikuwa akifanya kazi ya kusambaza madawa ya kulevya ya mwanaume huyo sehemu mbalimbali duniani kwa kutumia ndege.

Mchizi huyu alikuwa akipiga mzigo na kundi jingine la madawa ya kulevya na baadaye kufuatwa na Pablo na kuambiwa alitaka kumuajiri kwa ajili ya kumfanyia kazi zake.

Jamaa akakataa kwa kuwa alikuwa akilipwa mzigo mkubwa wa dola milioni 4 kwa mwaka. Pablo akaona siyo kesi, mambo yasiwe mengi, mimi nitakulipa dola milioni 20.

Unaachaje pesa hiyo? Ni mara tano ya kile alichokuwa akilipwa, akakubali kupiga naye kazi.

“Nilikuwa na Lamborghin 30,” alisema katika Podcast iitwayo Co***ne Air.

Dominguez kwa sasa ana miaka 73 na alisema hakutaka kabisa kufanya kazi hiyo lakini baada ya baba yake kutakiwa kulipa kiasi cha dola 100,000 ili apate dili la kusambaza sukari, na hakuwa na pesa, dogo akaamua kuchukua jukumu la kujifunza urubani na kuanza kusafirisha bangi.

Alipofanikisha na kuwa rubani kamili ndipo akapewa mchongo kwamba alikuwa anajichelewesha tu kwani kuna washikaji walimuweka mezani dola laki nane kwa ajili ya kusafirisha madawa ya kulevya.

Anasema hakutaka kujifikiria mara mbili, akakutana na watu hao, akazungumza nao na kukubaliana, alipofanya safari ya kwanza, wao wakampa dola milioni moja. Mzigo ulizidi kuongezeka kadiri muda ulivyosonga mpaka kufika dola milioni 4.

Baada ya kufanya kazi hiyo nzuri na wapinzani wa Pablo, akafuatwa na kuambiwa jamaa alitaka kupiga naye mzigo.

Katika kipindi cha mafanikio yake makubwa, jamaa alimiliki majumba ya kifahari, akafungua kampuni ya kuuza magari, akafungua kampuni ya ndege ndogo.

Baada ya kumalizana na Pablo mwaka 1988, FBI walianza kumfuatilia yeye na kuvamia nyumba yake iliyokuwa Florida, Marekani. Alik**atwa na kush*takiwa kwa makosa ya kusafirisha madawa ya kulevya, kutakatisha pesa na kesi nyingine kibao.

Maofisa hao wakachukua mali zake k**a magari, ndege na nyinginezo.

Mwaka 1991 Dominguez alipelekwa mahak**ani ambapo huko akapewa hukumu ya kula nyundo ya miaka 13 gerezani. Hiyo ilikuwa na miaka miwili ndani yake kwa kosa la kutaka kutoroka kwa helkopta yake wakati akitumikia kifungo chake gerezani.

Kwa sasa Dominguez anaendelea na maisha yake, anasema alilipia gharama ya yote aliyofanya kwa kufungwa gerezani. Anasema: “Kufeli ni pale unapoamua kuacha. K**a utaanguka, basi anguka kwa kusogea mbele.”

02/08/2025

WANANCHI SAZA WAELEZEA SIFA ZA VIONGOZI WANAOWAHITAJI

02/08/2025

KAIMU MUENEZI CCM SAZA ATOA WITO KWA WATIA NIA SAZA NA WANANCHI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

02/08/2025

MKURUGENZI WA UCHAGUZI WA CCM AKITOA ELIMU KWA WANANCHI WA SAZA KUHUSU KANUNI MBALIMBALI ZA UCHAGUZI KUELEKEA UCHAGUZI WA KUWAPATA WAWAKILISHI WATAKAOPEPERUSHA BENDERA YA CCM KATIKA NAFASI ZA UDIWANI NA UBUNGE..

02/08/2025

PETER MGOMBEA UDIWANI WA KATA YA SAZA ALIVYOZUNGUMZIA VIPAUMBELE VYAKE VYA SEKTA YA MADINI NA MAJI IKIWA WAJUMBE WATAMPA NAFASI YA UONGOZI

30/07/2025

Address

Saza
Songwe

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Saza tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Saza tv:

Share