12/04/2026
Rubani aliambiwa abebe wagonjwa wa akili (wenda wazimu) kutoka Kenya🇰🇪 kwenda Marekani 🇺🇸. Alikubali na kuwapakia ndani ya ndege yake 🙂. Kila mahali kulikuwa na kelele nyingi.
Baadaye, mmoja wa wagonjwa wa akili alimkaribia rubani na kumwambia: “Tafadhali nifundishe jinsi ya kuendesha ndege?”
Rubani akamjibu: “Nitakufundisha kuendesha ndege ikiwa utawaambia marafiki zako wawache kelele.” 😒
Yule mtu aliye na shida ya akili aliingia ndani. Baada ya dakika chache, kila mahali kukawa kimya k**a malaika aliingia ndani ya ndege. 😌
Baada ya muda, yule mtu alirudi na kumwambia rubani kwamba sasa kila mahali ni shwari. Rubani alifurahi na kumuuliza: “Uliwaambia nini ili watulie?”
Yule mtu aliye na shida ya akili akajibu: “Nilifungua mlango ili waende kucheza nje.”
Rubani alizimia! 🤣🤣🤣😂