28/12/2024                                                                            
                                    
                                                                            
                                            Putin aomba radhi kwa Aliyev wa Azerbaijan kutokana na ajali mbaya ya ndege 
 Rais wa Urusi Vladimir Putin amempigia simu mwenzake wa Azerbaijan, Ilham Aliyev, kueleza masikitiko kwa ajali mbaya ya ndege iliyotokea nchini Kazakhstan wiki hii, Ikulu ya Kremlin ilisema.
 Putin aliomba radhi kwa ukweli kwamba tukio "lilifanyika katika anga ya Urusi," na kuongeza kwamba lilitokea wakati wa uvamizi wa ndege zisizo na rubani za Ukrain, ambazo zilikuwa zikizuiwa na ulinzi wa anga.
 Kamati ya Uchunguzi ya Urusi inachunguza tukio hilo kwa ukiukaji unaowezekana wa sheria za usalama wa angani, Kremlin ilisema.  "Wataalamu wa kiraia na kijeshi" nchini Urusi wanahojiwa kuhusu matukio hayo, iliongeza