19/11/2025
𝐓𝐔𝐏𝐎 𝐊𝐔𝐍𝐃𝐈 𝐆𝐔𝐌𝐔
Ukiachana na mwaka 2018 tulipowekwa kundi moja na As Vita, Al Ahly na JS Saoura, Basi safari hii tumewekwa kwenye Kundi gumu pia
Tunaweza kuchukulia rahisi kila kitu ila sio Kundi hili, Mpango mkakati mzuri ndio utatuvusha hapa na sio Mazoea
Esperance, Simba na Petro wote ni HEAVYWEIGHT CLUBS Afrika, Wakati ambao Stade Malien anaingia k**a Underdog wa Kundi japokua nae ana uzoefu wa kushiriki mara kwa mara michuano ya CAF
Binafsi namuhofia zaidi Petro kuliko Esperance, Simba tunaweza kupata Alama 3 hadi 4 kwa Giant k**a Esperance tukijipanga vizuri ila tunaweza tukasumbuliwa mno na Petro k**a tutawadharau
Nina uhakika, Kundi hili kutakua na Suprize itayowashangaza wengi, Esperance anaetajwa k**a GIANT wa kundi anaweza kupitia magumu k**a itavyokua kwa Simba, Petro na Stade Malien
Kwa Simba SC tunapaswa kupigania Alama 3 za Nyumbani kwetu dhidi ya Petro na Esperance, Kisha tukatafute Alama 4 kwa Stade Malien
Hapo hesabu za kufikisha Alama 10 zitakamilika na huenda ikawa rahisi kufuzu Robo
Tupo Kundi gumu sana, Sio sehemu ya kuja kwa mazoea
Viwango News