05/09/2026
Baadhi ya vijana wamehimizwa kuacha tabia ya kuchagua kazi na badala yake kutumia fursa mbalimbali zilizopo katika kujiajiri, ikiwemo kilimo, ufugaji na shughuli nyingine za uzalishaji.
Akizungumza na UFR kupitia kipindi cha Konekti leo Septemba 5, 2026, Kocha wa Vijana wa Kujitegemea na Mtetezi wa Haki za Wanawake Mkoa wa Tabora, Steven Kimaro, amesema mfumo wa elimu umekuwa ukichangia kuwafanya vijana wengi kulenga ajira badala ya kuwa wabunifu na kuanzisha fursa za ajira.
Kimaro amesema changamoto nyingine ni baadhi ya vijana kutokuwa tayari kujifunza ujuzi mpya, huku akisisitiza kuwa mtaji si fedha pekee, bali maarifa, ujuzi na rasilimali walizonazo vinaweza kuwa msingi wa kuanzisha shughuli za kiuchumi.
Aidha, amewataka vijana kutumia fursa zinazopatikana kupitia mafunzo, ufadhili wa masomo, mikopo na miradi ya kilimo, huku akiwaonya dhidi ya kutegemea betting na forex k**a njia rahisi ya kutafuta utajiri.
π» Sikiliza Uyui FM Radio popote ulipo duniani, bofya kiungo (link) kwenye bio yetu.