07/09/2025
STORY: “Kikulacho Ki nguoni Mwako”
‎
‎Nilikuwa naamini ndoa yangu kwa asilimia mia moja.
‎Mke wangu, mama wa watoto wangu watatu, nilimpenda kwa dhati. Rafiki yangu wa karibu kabisa, ambaye tumeshiriki mengi, nilimchukulia k**a ndugu.Na kwa kuwa nyumbani hakukuwa na ugomvi wowote, niliona sina sababu ya kusikiliza maneno ya watu waliokuwa wakinieleza kuwa niangalia na kufanya uchunguzi kuwa kuna kitu hakiko sawa kati ya mkeo wangu na rafiki yangu…"
‎Nilidhani ni wivu tu wa watu.
‎Ni kachukulia poa tu maana walimwengu kwa maneno Huwa wazima nikaamua kunyamaza, nikiogopa kuvunja ndoa yangu kwa maneno ya watu.
‎✓Lakini siku moja, safari ya usiku ilinifunulia siri kubwa kuliko zote.
‎
‎Nilikuwa naelekea mkoani kikazi, lakini katikati ya safari gari langu likapa shida nikaita fundi, lakini haikuwezekana maana fundi alisema Lilihitaji matengenezo makubwa. Nikaamua kurudi nyumbani, nikidhani nitawashtua kwa furaha familia yangu maana Mrs hakutaka ni safiri kwa sababu ilikuwa ni muda mfupi tu nikiwa nimetoka safari nyingine k**a siku mbili tu hivi
‎Lakini mida hiyo ya saa saba usiku, nilipofika nyumbani…
‎Nilipigwa na butwaa. Mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani. Niligonga kwa muda mrefu.
‎Hatimaye, mke wangu akaja kufungua mlango akiwa amechanganyikiwa. Nilipowasha taa, macho yangu yakakutana na sura niliyokuwa siitegemei rafiki yangu wa karibu ndiye alikuwa ndani ya nyumba yangu, usiku huo!
‎
‎Nilihisi damu zangu zikisimama. Nilishindwa kuzungumza.
‎Mke wangu alijitetea: “Tulifunga mlango kwa sababu ni usiku, na yeye alikuja tu k**a rafiki…”
‎
‎Lakini moyoni nilijua, sikuhitaji mtu mwingine kuthibitisha.
‎Yule rafiki ambaye niliamini, ambaye nilimlisha, niliweka siri zangu mikononi mwake… ndiye aliyekuwa msaliti wangu mkubwa.
‎Na mke niliyemtetea kila mara, niliyeamini hata zaidi ya maneno ya watu… ndiye aliyegeuka kuwa mkuki uliopenya moyo wangu.
‎
‎Leo najua maana ya methali ile isemayo:
‎“Kikulacho, ki nguoni mwako.”
‎
‎Na sasa nimebaki na maswali:
‎Hivi ndoa ni imani au ni macho?
‎Rafiki ni nani wa kweli?
‎Na ni lipi bora — kuamini maneno ya watu au macho yako binafsi?