Majibu Ya Biblia

Majibu Ya Biblia MAJIBU YA MASWALI YAKO KATIKA BIBLIA

02/08/2026

MAOMBI MAALUMU (Day 13)

Kipengele: MAOMBI YA KUOMBEA SADAKA ULIZOWAHI KUTOA.

Bwana YESU KRISTO atukuzwe!
Najua unafahamu kuhusu sadaka.
Hebu soma somo hili kwa utulivu Kisha Maombi, somo hili ambalo Mimi Peter Mabula nakuletea Wewe rafiki yangu ni Ufunuo wa wazi ambao nilipewa kwa habari ya kutoa Sadaka na kuiombea hiyo Sadaka.

✓✓Kuna sadaka ya fungu la kumi, kuna sadaka ya kawaida(Sadaka ya dhabihu) na sadaka zingine kulingana na maelekezo ya ulimwengu wa roho wa Nuru.

Kabla ya yote ngoja nikuonyeshe faida ya sadaka mojawapo.

Ezekieli 44:30 "Na kitu cha kwanza cha malimbuko yote ya vitu vyote, na kila toleo la kila kitu
cha matoleo yenu, litakuwa la makuhani. Tena mtampa kuhani sehemu ya kwanza ya unga
mbichi, ili kukalisha baraka juu ya nyumba yako."

✓✓Biblia inasema hivi "ILI BARAKA IWE JUU YA NYUMBA/FAMILIA YAKO TOA SADAKA YA MALIMBUKO"
Maana yake sadaka hii utasababisha MUNGU aikalishe baraka juu ya nyumba Yako yaani familia Yako.

Sasa inawezekana umekutana na Neno la MUNGU likikutaka usiache kutoa sadaka yako au zaka yako mwaka baada ya mwaka
Kumbu 14:22 " Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka."
Ila hujui kazi yake kiroho.

Wakati mwingine umekutana na Neno la MUNGU likisema kwamba sadaka ni takatifu kwa MUNGU lakini wewe hujui faida za kutoa hiyo sadaka au zaka na unajiuliza je MUNGU kweli anahitaji sadaka na zaka za nini.

Walawi 27:30 "Tena zaka yote ya nchi, k**a ni mbegu ya nchi, au k**a ni matunda ya nchi, ni ya BWANA; ni takatifu kwa BWANA."

Wakati mwingine unajiuliza kwanini MUNGU ameagiza kwamba zaka au fungu la kumi wapewe watumishi na ni haki yao siku zote.

Hesabu 18:21" Na wana wa Lawi(Makuhani), nimewapa zaka yote katika Israeli kuwa urithi wao, badala ya huo utumishi wautumikao, maana, ni huo utumishi wa hema ya kukutania."

◼️Najua unafahamu kwamba sio kila mahali unaweza kutoa matoleo yako bali kule ambalo ROHO wa MUNGU atakupa msukumo rohoni ili utoe.
Kumbu 12:13-14 "Ujihadhari usitoe sadaka zako za kuteketezwa katika kila mahali upaonapo; bali katika mahali atakapopachagua BWANA katika kabila zako mojawapo, ndipo utakapotoa sadaka zako za kuteketezwa, ndipo utakapotenda yote nikuamuruyo."
Japokuwa umesikia msukumo rohoni kutoa lakini unashindana na maagizo hayo ndani ya roho yako, unajiuliza kwanini umapewa maagizo ya kiroho kutoa matoleo yako?

◼️Ni kwa sababu sadaka ni jambo la kiroho na lenye faida nyingi za kiroho.

Mawakala wa shetani nao kwa kujua baadhi ya kazi za sadaka kiroho ni rahisi kumfunga mtu kupitia sadaka.
◼️Moja ya mambo ya kujua kuhusu sadaka ni kwamba moyo huambatana na sadaka iliko.
Mathayo 6:21" kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako."

Aliyeyasema haya ni Bwana YESU KRISTO Mwokozi mwenyewe akitutaka tutoe sadaka zetu kwenye ufalme wa MUNGU maana kwa njia hiyo sehemu ambako sadaka zetu zitakuwa na roho zetu zitakuwa huko, ni jambo jema sana kutoa matoleo yetu kwa MUNGU katika KRISTO YESU.

Lakini kwa sababu moyo(nafsi) huifuata sadaka basi ukitoa sadaka kwa mashetani ujue moyo wako unaifuata sadaka hiyo huko.

✓Ukitoa kwa mganga ujue moyo wako unaifuata sadaka yako huko.

✓Kwa sababu sadaka huhusika kutengeneza agano basi ujue sadaka yako inaweza kutengeneza agano kati yako na nguvu za giza.

✓Kuna watu hawakuwahi kuhusika na nguvu za giza ila matambiko ya ukoo yalizifanya nguvu za giza kuwafuatilia. Na matambiko huhusisha sadaka na damu ya sadaka hizo za kipepo.

✓Kuna watu hawakuwahi kuhusika na nguvu za giza ila walidanganywa na kutoa vitu(Sadaka) vyao kwa mashetani.

Kuna watu walikwenda kwa waganga wa kienyejj ili kuzifuata nguvu za giza kwa wao kutoa sadaka/kafara au chochote kwa mganga basi hadi muda huu nafundisha somo hili wao wanamilikiwa na nguvu za giza.

Kupitia matambiko na mazindiko na mambo yote ya uganga wa kienyeji watu wengi hujikuta wameambatanisha na uzao wao kwa mashetani.
Zaburi 106:37 "Naam, walitoa wana wao na binti zao Kuwa dhabihu kwa mashetani."

Mwanamke mmoja kwenye ulimwengu wa roho Mara nyingi alijiona kuzimu huku mapepo wakimtesa, wakisema kwamba wana uhalali maana walikabidhiwa ukoo na babu yake huyo mwanamke kupitia tambiko lenye sadaka nzuri.

Katika ulimwengu wa mwili ni mateso mengi sana amekutana nayo.

Sadaka kumpa mtu ambaye hujamthibitisha k**a ni Mtumishi wa MUNGU wa kweli katika KRISTO YESU ni jambo la hatari sana.

Mimi binafsi kuna vipindi tofauti kuna watu ambao ni marafiki zangu Facebook, mtu wa kwanza siku moja aliandika meseji inbox zaidi ya 5 akiomba nimtumie Tsh 5,000 au 2,000 na anashida nayo sana, hajala tangu asubuhi, roho yangu ikawa nzito sana hivyo nikakaa karibu masaa 4 bila kumjibu huyo ndugu, baadae nikafungua profile yangu na kukuta amepost muda mfupi uliopita akiwa na gari yake nzuri na akiwa na familia yake wakila chakula, maelezo tu aliyoandika yanaonyesha wala hakuhitaji 2000 kwa sababu hana, baadae nilijua ni hila za shetani, maana nafsi yako inaweza hata kuambatana na sadaka yako kwenda kwa mchawi.
Mtu mwingine siku moja alinitafuta sana akiomba pesa ya kununua dawa anaumwa, ni tsh 5000 nikamwambia anipigie nimuombee na atapona, akakataa kuombewa, baadae nilijua pesa yangu inatafutwa k**a sadaka ili kuifunga huduma yangu kiroho.

Kwa sasa watu wa namna hiyo ni wengi sana na huwa hata siwajibu maana najua wanachotafuta.

Kumbuka pia kutokutoa sadaka mbalimbali kwa MUNGU ni hatari sana kwako kuliko ukitoa, hivyo usiache kamwe kutoa Sadaka kwa MUNGU katika KRISTO YESU, Muhimu hapo ni huyo Mtumishi unayempa mthibitishe kuwa ni Mtumishi wa kweli wa Bwana YESU KRISTO.

Ndugu kutoa kwa MUNGU katika KRISTO YESU ni muhimu sana na ina faida sana kwako kiroho lakini zingatia sana kwamba sio kila mtu wa kumpa sadaka yako, ukimpa Mtumishi wa shetani ujue na moyo wako unaweza kuambatana na sadaka yako katika madhabahu ya shetani, ni hatari sana usipojua kuomba katika jina la YESU KRISTO na ukitumia damu ya YESU KRISTO ya agano ili kujinasua.

Sadaka katika KRISTO zina kazi yake kiroho ndio maana watu wa MUNGU tangu zamani walitoa sadaka.

✓✓Sadaka ni hitajio la kiroho japokuwa wengi hawajui.

Jambo la kwanza kujua ni kwamba hakuna agano bila sadaka, yaani agano lolote haliwezi k**imama k**a hakuna sadaka zetu.

Kwanini leo tuombe juu ya sadaka tulizowahi kutoa?

1. Sadaka hunena.

Waebrania 11:4 "Kwa imani Habili alimtolea MUNGU dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; MUNGU akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena."

Ingawa Habili alikufa lakini sadaka alizokuwa ametoa kabla kwa MUNGU ilisababisha awe ananena, kwa sababu ya Sadaka

Ni k**a sadaka ya Ibrahimu iliyotengeneza agano na MUNGU na agano hilo likakumbukwa Miaka mingi baadae kwa ajili ya Uzao wake.

Kutoka 2:24-25 " MUNGU akasikia kuugua kwao, MUNGU akakumbuka agano lake alilolifanya na Ibrahimu na Isaka na Yakobo. MUNGU akawaona wana wa Israeli, na MUNGU akawaangalia."

MUNGU alikumbuja agano likilotengenezwa na Sadaka, hiyo ndio maana ya kusema sadaka inazungumza.

Sadaka ya Habili ilikuwa inanena, hata sadaka yako inaweza kunena.
K**a ulitoa sadaka kwa MUNGU ielekeze sadaka yako inene mema juu ya nini.
K**a ulitoa sadaka kwa mashetani na hiyo sadaka ya kipepo inaendelea kunena basi ifute hiyo sadaka kwa damu ya YESU KRISTO ya agano.

2. Kuna sadaka ulitoa kwa MUNGU k**a mbegu ili ziote na ujue uvune.

2 Wakorintho 9:6 "Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu."

K**a ulitoa sadaka ya namna hii kwa MUNGU basi omba kupewa nguvu na uwezo wa kuvuna k**a ulivyopanda.

3. Kwa sababu ni heri(baraka) kutoa kuliko kupokea, omba MUNGU akupe uheri unaotokana na kutoa kwako.

Matendo 20:35" Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana YESU, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea."

4. Kwa sababu sadaka kuitoa kwa MUNGU hutengeneza agano na MUNGU basi imalisha agano hilo kwa Maombi na utakatifu.

Zaburi 50:5 "Nikusanyieni wacha MUNGU wangu Waliofanya agano nami kwa dhabihu."

Kinyume chake ni kwamba k**a ulitoa sadaka kwa mawakala wa shetani na sadaka hiyo ikatengeneza agano na mashetani basi futa agano hilo la kipepo kupitia sadaka yako, lifute agano hilo kwa damu ya YESU KRISTO ya agano.

5. Utoaji humfanya MUNGU awakemee maadui zako.

Malaki 3:11 "Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi."

Hivyo mwambie MUNGU awakemee maadui zako(wataje), na akiwakemea MUNGU maana yake hawatakugusa tena.
Maadui k**a magonjwa na maroho wote wa kuzimu na hata wanadamu wanaotumika kipepo.
Nina mengi sana ila kwa leo ngoja niishie hapo.
Usiache kutoa zaka na sadaka ila to a kwa Mtumishi wa MUNGU aliye hai.
Omba katika maeneo hayo 5 na MUNGU wa Mbinguni atakutendea Muujiza wako uliotokana na Sadaka zako.
MUNGU akubariki sana sana.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la MUNGU wa Mbinguni.
+255714252292(Sadaka ya kuipeleka Injili, Ushauri, Maombi, Whatsapp n.k)
Ubarikiwe sana.

https://wingulamashahidi.org/2026/07/23/nifinyange-bwana/ *NIFINYANGE BWANA*Jina la Mwokozi wetu YESU KRISTO libarikiwe ...
23/07/2026

https://wingulamashahidi.org/2026/07/23/nifinyange-bwana/

*NIFINYANGE BWANA*

Jina la Mwokozi wetu YESU KRISTO libarikiwe sana, karibu tujifunze Biblia, Neno la Mungu wetu lililo taa na mwanga wa njia yetu (Zab.119:105).

Yeremia 18: 1 “Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa Bwana, kusema,

2 Ondoka, ukashuke mpaka NYUMBA YA MFINYANZI, na huko nitak**ikizisha maneno yangu.

3 Basi nikashuka mpaka nyumba ya mfinyanzi, na tazama, alikuwa akifanya kazi yake kwa magurudumu. 4 NA CHOMBO KILE, ALICHOKUWA AKIKIFINYANGA, KILIPOHARIBIKA MKONONI MWAKE YULE MFINYANZI, ALIKIFANYIZA TENA KUWA CHOMBO KINGINE, k**a alivyoona vema yule mfinyanzi kukifanya”.

Katika mstari wa 4 tunasoma kuwa Mfinyazi alikifinyanga chombo kilichoharibika na kuwa chombo kingine, zingatia hilo neno “chombo kingine” maana yake sio tena chombo kile cha kwanza kilichoharibika.

Tuchukue mfano labda mfinyazi huyu alifinyanga kikombe cha maji hapo kwanza, na baadae akaone kimeharibika au kina kasoro, ndipo anapokivunja vunja kile kikombe cha udongo na kuutia tena maji na kuufinyanga tena kuwa sahani..

Sasa udongo ni ule ule umeweza kutoa chombo kingine kipya tofauti na kile cha kwanza, na MUNGU alimwambia hivo hivyo YEREMIA, lakini Yeremia hayupo sasa, ila sisi tupo, hivyo anatuambia sisi kuwa tujifunze kwa Mfinyanzi kwakuwe yeye (MUNGU) ndiye mfinyanzi mkuu wa maisha yetu.

Yeremia 18: 5 “Ndipo neno la Bwana likanijia, kusema,

6 Ee nyumba ya Israeli, je! Siwezi mimi kuwatendea ninyi vile vile k**a mfinyanzi huyu alivyotenda? Asema Bwana. Angalieni, K**A UDONGO ULIVYO KATIKA MKONO WA MFINYANZI, NDIVYO MLIVYO NINYI KATIKA MKONO WANGU, EE NYUMBA YA ISRAELI”.

Je wewe ni chombo cha aina gani?..

K**a maisha yako yametawaliwa na dhambi basi fahamu kuwa ni dhahiri kuwa wewe ni chombo kilichoharibika, k**a maisha yako yametawaliwa na ugomvi, uasherati, wizi, masengenyo, kiburi na mambo mengine yote ambayo ni kinyume cha Neno la MUNGU (yaliyotajwa kwenye Wagalatia 5:19-20), huu ni wakati wa wewe kumkimbilia mfinyazi Mkuu YESU KRISTO, akufinyange kuwa chombo kingine cha heshima..

Warumi 9:21 “Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima?”

Bwana YESU anaweza kukufanya kuwa mwingine kabisa, mtu wa maana kabisa, ambapo ile hali yako ya ulevi wa pombe au ulevi wa anasa inayokusumbua, kinachotakiwa tu ni kukiri kuwa wewe ni mkosaji mbele zake na unahitaji msaada wake, na baada ya hapo kutubu dhambi zako mbele yake huku ukidhamiria kabisa kuacha mambo yote mabaya, na kumwambia naomba unifinyange tena, kupitia Roho wake mtakatifu atakayeingia ndani yako atakugeuza na kuwa mtu mwingine.

Kumbuka toba isiyo ya kumaanisha haileti matokeo yoyote kwa mtu anayetaka mabadiliko, hakikisha unapotubu dhamiria kujitakasa, kwa kujitenga na vichocheo vyote vya dhambi, k**a ulikuwa ni mlevi acha kwenda Bar, k**a ulikuwa unajiuza jizuie kwa bidii kwenda vituo vya ulivyokuwa unafanya biashara hiyo, ili uumpe nafasi Roho Mtakatifu ndani yako kukufinganya upya kuwa chombo kingine.

2Timotheo 2:21 “Basi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hao, atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema”.

Bwana YESU akubariki sana.

+255693036618/ +255789001312

Jina la Mwokozi wetu YESU KRISTO libarikiwe sana, karibu tujifunze Biblia, Neno la Mungu wetu lililo taa na mwanga wa njia yetu (Zab.119:105). Yeremia 18: 1 “Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa Bwana, kusema, 2 Ondoka, ukashuke mpaka NYUMBA YA MFINYANZI, na huko nitak**ikizisha maneno y...

https://wingulamashahidi.org/2026/07/22/atawafanyia-wamchao-matakwa-yao/ *ATAWAFANYIA WAMCHAO MATAKWA YAO.*Zaburi 145:19...
22/07/2026

https://wingulamashahidi.org/2026/07/22/atawafanyia-wamchao-matakwa-yao/

*ATAWAFANYIA WAMCHAO MATAKWA YAO.*

Zaburi 145:19 “Atawafanyia wamchao matakwa yao, Naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa”.

Pamoja na kwamba tumeagizwa kuomba “Mapenzi yake yatimie/yatimizwe (Mathayo 6:10”.

Lakini “Siri” moja kuu ni kwamba zaidi ya asilimia 90 ya Maombi ya wanaomcha MUNGU ni mapenzi ya MUNGU.Kwanini?..

Kwasababu maandiko yanatuambia hapo kuwa “Atawafanyia wamchao matakwa yao, Naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa”.

Zingatia hilo neno “Atawafanyia wamchao matakwa yao”.

Kumbe Mungu anawapatia watu wake wanaomcha “Matakwa yao, yaani haja zao wanazozitaka”.

Kwa mtu anayemcha Mungu akiomba amani, ni asilimia kubwa ya hitaji lake hilo kuwa ni mapenzi ya MUNGU.

Mtu anayemcha MUNGU akiomba afya, ni asilimia zaidi ya nusu kuwa anaomba jambo ambalo ni mapenzi ya MUNGU.

Mtu anayemcha MUNGU akiomba akiomba mambo mengine yote ikiwemo mafanikio ya kiroho na kimwili ni mapenzi ya MUNGU, kwasababu MUNGU anawapa wamchao matakwa yao.

Je unataka kupewa matakwa yako na MUNGU?.Jibu ni rahisi “Mche Mungu tu”..Na Biblia inasema kumcha Mungu ndio hekima na kuepukana na uovu ndio ufahamu (Ayubu 28:28).

Sasa hatuwezi kumcha MUNGU kwa nguvu zetu, inahitajika kuwezeshwa na Roho Mtakatifu, kwasababu tabia ya kumcha MUNGU, ni zao la Roho Mtakatifu.Isaya 11:2 “Na roho ya BWANA atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, *ROHO YA MAARIFA NA YA KUMCHA BWANA”.*

Sasa k**a kumcha Bwana ni zao la Roho Mtakatifu, je tunampataje Roho Mtakatifu..

Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”

Kumbe kanuni ya kupokea Roho ni kutubu na kubatizwa kwa jina la YESU KRISTO!.

Basi maana yake tukitubu na kubatizwa tutapokea Roho Mtakatifu k**a ilivyoandikwa, na matokeo ya kujaa Roho Mtakatifu, ni uwezo wa kumcha MUNGU kuingia ndani yako.Na matokeo ya kumcha MUNGU sana ni k**ikiwa maombi yako na Bwana kukupa matakwa yako.

Je umeokoka?..Je unamcha Bwana?.

Zaburi 112:1 “Haleluya. Heri mtu yule amchaye BWANA, Apendezwaye sana na maagizo yake.

2 Wazao wake watakuwa hodari duniani; Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa”.

3 Nyumbani mwake mna utajiri na mali, Na haki yake yakaa milele”.

Bwana akubariki.

Zaburi 145:19 “Atawafanyia wamchao matakwa yao, Naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa”. Pamoja na kwamba tumeagizwa kuomba “Mapenzi yake yatimie/yatimizwe (Mathayo 6:10”. Lakini “Siri” moja kuu ni kwamba zaidi ya asilimia 90 ya Maombi ya wanaomcha MUNGU ni mapenzi ya MUNGU.Kwanini?.. Kw...

20/07/2026
https://wingulamashahidi.org/2024/12/19/tutampiga-kwa-ndimi-zetu/ *TUTAMPIGA KWA NDIMI ZETU.*Silaha ya Mwisho mwisho kab...
15/07/2026

https://wingulamashahidi.org/2024/12/19/tutampiga-kwa-ndimi-zetu/

*TUTAMPIGA KWA NDIMI ZETU.*

Silaha ya Mwisho mwisho kabisa ya adui kumshambulia Mtu ni “ULIMI WA UOVU”.. Ukiona Maneno ya uongo kuhusu wewe, au ya vitisho au ya uchonganishi yanatembea huku na huko basi fahamu kuwa adui ndio yupo katika hatua za mwisho mwisho, kukuacha!..(Ni wakati wa kumaliza jaribu).

Na k**a ukiweza k**imama katika hiko kipindi bila hofu, wala kutetereka wala kurudi nyuma, basi shetani unaweza usimwone tena baada ya hapo, kwa kipindi kirefu sana.

Mfano katika biblia tunamwona Nabii Yeremia,

Adui alimtafuta mara nyingi kwa njia mbalimbali ili amnyamazishe asitoe unabii, lakini kila alichojaribu ili kumzuia Yeremia asitoe unabii, kilishindikana, na ndipo akatumia silaha yake ya mwisho ya NDIMI ZA UOVU, ili yamkini amtishe Yeremia, lakini pia haikusaidia,

Yeremia 18:18 “Hapo ndipo waliposema, Njoni na tufanye mashauri juu ya Yeremia; maana sheria haitampotea kuhani, wala shauri halitampotea mwenye hekima, wala neno halitampotea nabii. Njoni, na TUMPIGE KWA NDIMI ZETU, wala tusiyaangalie maneno yake yo yote.

19 Niangalie, Ee Bwana, ukasikilize sauti ya wanaoshindana nami”.

Wakati huo kilitokea kikundi kiovu na kuanza kumtisha Yeremia kwa maneno mengi, na pia kumzushia mambo mengi na zaidi ya yote, ya uchonganishi na kumchafua mbele ya Mfalme, ili tu Yeremia ak**atwe asiendelee kutoa unabii.

Yeremia 38: 4 “Ndipo wakuu wakamwambia mfalme, Twakuomba, mtu huyu auawe, kwa kuwa aidhoofisha mikono ya watu wa vita, waliobaki katika mji huu, na mikono ya watu wote, kwa kuwaambia maneno k**a hayo; maana mtu huyu hawatafutii watu hawa heri, bali shari.

5 Naye mfalme Sedekia akasema, Tazama, yu mikononi mwenu; maana mfalme siye awezaye kufanya neno lo lote kinyume chenu”.

Mtu mwingine aliyepigwa kwa NDIMI OVU ni nabii Danieli, soma Danieli 6..

Sasa kwanini Adui, aiweke hii silaha ya ulimi k**a chaguo lake la mwisho?… Ni kwasababu anajua ulimi wa mtu unaweza kuwasha moto mkubwa, na k**a mtu hatakuwa na Imani ya kutosha basi anaweza kuanguka kabisa…

Yakobo 3:6 “Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum”

Hivyo shetani anaweza kukuwashia tu moto kupitia ulimi wa mtu au ndimi za watu, na moto huo ukawa mkubwa sana, kiasi kwamba k**a huna imani na ujasiri wa kutosha, unaweza kurudi nyuma kabisa.

Shedraka, Meshaki na Abednego walijikuta wapo katika tanuru la Moto, kwasababu tu ya baadhi ya watu waliotumia ndimi zao kupeleka mash*taka kwa mfalme kuwa hawataki kuisujudia ile sanamu.(Danieli 3:8-12).

Danieli naye alijikuta katika tundu la simba kwasababu tu ya vinywa vya watu, na Yeremia naye alijikuta katika lile shimo refu lenye giza lililojaa matope kwasababu ya maneno ya watu(Yeremia 38:6)..

Lakini wote hao walishinda, kwani moto ule uliokusudiwa juu yao uliwala maadui zao, na mashimo yale na matundu yale yaliyokusudiwa juu yao yaliwaharibu maadui zao, lakini k**a wangetetemeka na kuogopa na kurudi nyuma bila shaka wangepotea kwa kuharibiwa na ibilisi!.

Na sisi hatuna budi k**imama Imara bila hofu, kwa ujasiri mwingi pale ambapo adui anatumia NDIMI za watu k**a silaha yake…

Hiko ni kipindi cha kuwa na imani na ujasiri….mipango inapopangwa ya vitisho au uchonganishi, havitasimama endapo wewe utasimama.

Ni wakati wa k**imama na kuamini huku tukiomba, na silaha za ndimi zao zitaanguka, na Bwana atatukuzwa.

Ifuatayo ni mistari inayozungumzia hatari ya NDIMI ZA UOVU…

Zaburi 57:4 “Nafsi yangu i kati ya simba, Nitastarehe kati yao waliowaka moto. Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale, Na ndimi zao ni upanga mkali.”

Zaburi 64: 2 “Utanificha mbali na shauri la siri la watenda mabaya, Mbali na ghasia ya watu wafanyao maovu;

3 Waliounoa ulimi wao k**a upanga, Wameielekeza mishale yao, maneno ya uchungu,

4 Wapate kumpiga mkamilifu faraghani, Kwa ghafula humpiga wala hawaogopi.

5 Walijifanya hodari katika jambo baya; Hushauriana juu ya kutega mitego; Husema, Ni nani atakayeiona”

Zaburi 140:1 “Ee Bwana, uniokoe na mtu mbaya, Unihifadhi na mtu wa jeuri.

2 Waliowaza mabaya mioyoni mwao, Kila siku huondokesha vita.

3 Wamenoa ndimi zao k**a nyoka, Sumu ya fira i chini ya midomo yao”.

Lakini pamoja na kwamba adui anatumia ndimi kutushambulia, vile vile na sisi tunaweza kutumia ndimi hizo hizo, kumharibu.

Mithali 18:21 “Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake”

Tunampiga shetani kwa ndimi zetu, kwa njia ya KUOMBA, na hususani maombi yanayohusisha mfungo.

Bwana atubariki.

+255789001312/
+255693036618

Silaha ya Mwisho mwisho kabisa ya adui kumshambulia Mtu ni “ULIMI WA UOVU”.. Ukiona Maneno ya uongo kuhusu wewe, au ya vitisho au ya uchonganishi yanatembea huku na huko basi fahamu kuwa adui ndio yupo katika hatua za mwisho mwisho, kukuacha!..(Ni wakati wa kumaliza jaribu). Na k**a ukiweza k**i...

https://wingulamashahidi.org/2024/06/11/shika-sana-ulicho-nacho-asije-mtu-akaitwaa-taji-yako/ *SHIKA SANA ULICHO NACHO, ...
12/07/2026

https://wingulamashahidi.org/2024/06/11/shika-sana-ulicho-nacho-asije-mtu-akaitwaa-taji-yako/

*SHIKA SANA ULICHO NACHO, ASIJE MTU AKAITWAA TAJI YAKO.*

Ufunuo 3:11 “Naja upesi. SHIKA SANA ULICHO NACHO, asije mtu akaitwaa taji yako”.

Hapo anasema “..Asije mtu.” na si “..Asije shetani”. Maana yake anayeitwaa taji ya mtu ni MTU, kwasababu shetani yeye taji lako au langu halimsaidii kitu, kwasababu haendi kulivaa.. lakini mwingine akilichukua litaenda kumfaa anakokwenda!.

Labda tuzidi kuliweka hili vizuri..

Aliyelichukua Taji la “Yuda Iskariote” ni mtu aliyeitwa “Mathiya”… baada ya Yuda kushindwa kushikilia alichopewa…

Matendo 1:24 “Kisha wakaomba, wakasema, Wewe, Bwana, ujuaye mioyo ya watu wote, tuonyeshe ni nani uliyemchagua katika hawa wawili,

25 ashike mahali katika huduma hii na utume huu, alioukosa Yuda, aende zake mahali pake mwenyewe.

26 Wakawapigia kura; kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja”.

Vile vile aliyeichukua Taji ya “ESAU” ni ndugu yake “YAKOBO”…Baada ya kuidharau ile haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa tamaa ya chakula kimoja tu.

Waebrania 12:16 “Asiwepo mwasherati wala asiyemcha Mungu, k**a Esau, aliyeuuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza kwa ajili ya chakula kimoja.

17 Maana mwajua ya kuwa hata alipotaka baadaye kuirithi baraka, alikataliwa (maana hakuona nafasi ya kutubu), ijapokuwa aliitafuta sana kwa machozi”

Umeona unapoacha kuthamini kile ulichopewa, basi mwingine atakichukua,..unapoacha kuthamini nafasi yako mwingine ataichukua.. Unapoacha kuthamini huduma yako uliyopewa na Mungu, mwingine ataichukua na utapoteza thawabu zako.

> Umepewa huduma ya Uinjilisti, usiipuuzie na kuifanya kilegevu.. Bwana anaweza kuiondoa kwako na kumpa mwingine atakayeifanya vizuri na kwa ushujaa.

> Umepewa huduma ya maombezi, fanya hayo kwa bidii, usipuuze kwani Bwana anaweza kuiondoa kwako na kumpa mwingine ikiwa utaipuuza.. na thawabu yako (Taji yako) utakuwa umeipoteza.

> Umepewa huduma ya kukirimu (kwamba kupitia ulivyopewa unahudumia watumishi na kazi ya Mungu) basi usidharau neema hiyo kwasababu Bwana anaweza kuiondoa kwako na kumpa mwingine na hivyo Taji yako ikaondoka, fanya uliyojaliwa na BWANA kwa bidii sana..(Na huduma nyingine zote ni hivyo hivyo).

SHIKA SANA ULICHO NACHO!!.. SHIKA SANA ULICHO NACHO!!!… SHIKA SANA ULICHO NACHO!! Kwasababu kina thamani kubwa!.. Hakikisha unakizalia matunda.

Na majira haya, shoka lipo kwenye mashina ya miti kukata kila tawi lisilozaa,

Luka 3:9 “Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni”.

Bwana atusaidie tusikatwe. Lakini Neno ni moja tu kwetu. TUSHIKE SANA TULIYO NAYO!!!

Bwana akubariki.

Kwa mawasiliano: +255789001312/ +255693036618

Ufunuo 3:11 “Naja upesi. SHIKA SANA ULICHO NACHO, asije mtu akaitwaa taji yako”. Hapo anasema “..Asije mtu.” na si “..Asije shetani”. Maana yake anayeitwaa taji ya mtu ni MTU, kwasababu shetani yeye taji lako au langu halimsaidii kitu, kwasababu haendi kulivaa.. lakini mwingine akilichuk...

https://wingulamashahidi.org/2026/07/09/mtolee-bwana-kwa-ufunuo-k**a-hana/ *MTOLEE BWANA KWA UFUNUO K**A HANA*Jina la Bw...
09/07/2026

https://wingulamashahidi.org/2026/07/09/mtolee-bwana-kwa-ufunuo-k**a-hana/

*MTOLEE BWANA KWA UFUNUO K**A HANA*

Jina la Bwana YESU libarikiwe, karibu tujifunze Biblia, Neno la MUNGU wetu lililo Taa na Mwanga wa njia zetu (Zab. 119:105).
Katika Biblia tunajifunza jambo kubwa sana kwa mwanamke “Hana” ambaye alikuwa tasa lakini baadae Bwana alimfungua tumbo lake na kuzaa watoto.

Katika usomaji wa kitabu cha 1Samweli mlango wa kwanza na wa pili, ni rahisi kufikiri kuwa Hana alimwekea MUNGU nadhiri ya kumtoa mtoto wake wa kwanza atumike kwenye nyumba ya MUNGU daima, bila kuwa na ufunuo au sababu yoyote (ni rahisi kufikiri hilo).

Lakini tukijifunza kwa undani, tunaona wazi kuwa sababu kuu ya Hana kumtoa mtoto wake wa kwanza (Samweli) atumike kwenye nyumba ya MUNGU daima, ni matatizo aliyoyaona ndani ya nyumba ya MUNGU, kwa wakati ule.

Kwani walikuwepo wana wawili wa kuhani Eli, walioitwa Hofni na Finehasi, vijana hawa hawakuwa waaminifu katika nyumba ya MUNGU,

Kwani walikuwa wanatumia vibaya dhabihu na sadaka zilizokuwa zinaletwa nyumbani mwa Bwana, na zaidi sana walikuwa wakizini na wanawake waliokuwa wakihudumu ndani ya nyumba ya MUNGU, na sifa zao hizo mbaya ziijulikana na watu wote, na hata mwanamke “Hana” aliwajua kwa sifa hiyo.

1 Samweli 2:22 “Basi Eli alikuwa mzee sana; naye alisikia habari za mambo yote ambayo wanawe waliwatenda Waisraeli; na jinsi walivyolala na wanawake waliokuwa wakitumika mlangoni pa hema ya kukutania.

23 Akawaambia, Mbona mnatenda mambo k**a hayo? Maana nasikia habari za matendo yenu mabaya kwa watu hawa wote.

24 Sivyo hivyo, wanangu, kwa maana habari hii ninayoisikia si habari njema; mnawakosesha watu wa BWANA.

25 Mtu mmoja akimkosa mwenzake, Mungu atamhukumu; lakini mtu akimkosa BWANA, ni nani atakayemtetea? Lakini hawakuisikia sauti ya baba yao, kwa sababu BWANA amekusudia kuwaua”.

Kwasababu hiyo basi Hana, aliona shukrani pekee ambayo anaweza kumpa MUNGU endapo Mungu atamfungua tumbo lake si kutoa pesa, kwasababu hata akizipeleka madhabahuni nyumbani mwa MUNGU zitatumiwa vibaya na wale vijana wawili wa Eli (Hofni na Fineasi), wala si dhabihu kwasababu pia zinatumika vibaya.

Ndipo alipotafakari na kuona nadhiri bora na sadaka maalumu itakuwa ya kumtoa mwanae wa kwanza kwa Bwana akawe Mtumishi wa madhabahuni,

Hiyo aliona inaweza kuwa sadaka njema kwake kwa BWANA, Kwani mtoto yule atakuwa katika misingi sahihi ya kiMungu, na atasimama katika kazi ya nyumba ya Bwana kwa uaminifu na kuwa baraka kwa Israeli yote.

Ndivyo Hana alivyofanya, na kupitia sadaka yake hiyo ya kiufunuo, Mungu alisikia maombi yake na kumpa mtoto Samweli, ambaye ndiye aliyekuja kuwaa nabii mkuu Israeli kwa wakati ule.

Ni hivyo hivyo kwa MUNGU wetu, aliona baraka kubwa atakayoibarikia dunia si kuleta mvua nyingi yenye kustawisha nafaka ili matatizo ya njaa yaishe duniani, wala si kumfanya kila mtu kuwa milionea, bali ni kwa kumtoa mwanae pekee YESU KRISTO, K**a dhabihu iliyo hai na sadaka kuu, na kupitia sadaka hiyo leo hii tunabarikiwa kwa baraka zote.

Na sisi tunajifunza mambo hayo hayo, kutazama katika roho ni nini cha kumtolea BWANA, si kila wakati fedha au mali zitakuwa ni sadaka sahihi kwa MUNGU au kwa Nyumba yake au kazi ya MUNGU, wakati mwingine wewe mwenyewe unaweza kuwa sadaka bora kwa kujitoa mwili wako na muda wako kutumika.

Warumi 12:1 “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.

Au si wewe bali mwanao anaweza kuwa bora zaidi na akawa sadaka yenye kumpendeza Bwana. (Kwa wewe kumuandaa kuwa mtumishi, kwa kumfundisha, kumwombea na kumtolea sadaka kwa MUNGU).

Kuna wakati ardhi inaweza kuwa sadaka nzuri kwa Bwana zaidi ya fedha, kuna wakati, kununua kitu na kukipeleka nyumbani mwa Bwana inaweza kuwa bora zaidi kuliko kutoa tu fedha, na kuna wakati fedha ni muhimu zaidi kuliko kitu utakachopeleka, hivyo ni muhimu kuwa na jicho la kiroho na kujua ni kipi kinafaa kutoa kwa wakati huo.

Na kumbuka siku zote, ni heri kutoa kuliko kupokea (Matendo 2:35).

Bwana YESU atusaidie katika kumtolea yeye matoleo yenye kumpendeza.

Shalom.

+255789001312/
+255693036618

Jina la Bwana YESU libarikiwe, karibu tujifunze Biblia, Neno la MUNGU wetu lililo Taa na Mwanga wa njia zetu (Zab. 119:105). Katika Biblia tunajifunza jambo kubwa sana kwa mwanamke “Hana” ambaye alikuwa tasa lakini baadae Bwana alimfungua tumbo lake na kuzaa watoto. Katika usomaji wa kitabu cha ...

Address

Tanga
21101

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Majibu Ya Biblia posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share