01/03/2024
.
✍🏻Timu mbili ambazo kipindi cha kwanza kila mmoja alikuwa anaona njia sahihi ya kupita ni katikati ya uwanja na wote wawili wakafunga njia za ndani : Al Ahly bila mpira wakiwa 4-4-1-1 wakati Yanga bila mpira wanakuwa 4-1-4-1 , wote wakiwa compact sana na kukubali kuacha space pembeni tu .
✍🏻Kipindi hiko hiko cha kwanza Al Ahly upande wao wa mashambulizi ni kushoto kwao : Maaloul na El Shahat wakati Yanga ilionekana sana nao upande wa kushoto Pacome na Lomalisa . Lakini kwanini kipindi cha kwanza njia zao hazikufanikiwa sana ?
1: Musonda alikuwa na kazi ya kurudi nyuma dhidi ya Maaloul ( mara chache sana alisinzia ) lakini mara nyingi alifanikiwa na ndio maana Al Ahly hawakutengeneza sana nafasi
2: Yanga wao licha ya Lomalisa kuwa na space upande wa kushoto shida walikuwa wanachelewa kushambulia kwa idadi kubwa ya wachezaji kwenye eneo la Al Ahly
✍🏻Kipindi cha pili Al Ahly ndio walionekana kupata suluhisho zaidi jinsi gani ya kuifungua Yanga
1: Rotations ya fullbacks na wingers wao pembeni ya uwanja , kivipi na ilisaidia nini ?
2: Pale ambapo Maaloul ana overlap basi El Shahat anaingia ndani kwenye halfspace , na El Shahat akibaki pembeni basi Maaloul anafanya runs kwa ndani sawa sawa na upande wa Percy Tau na Tawfik .... faida yake ?
3: Moja , Kupata space katikati ya mstari wa ulinzi na kiungo wa Yanga , Mbili kuharibu muundo wa ulinzi wa Yanga kwenye eneo lao la pili ulinzi ( kiungo ) na tatu kutengeneza idadi ya wachezaji wengi pembeni ya uwanja ( overloads )
✍🏻Nafikiri baada ya goli moja pale mechi ikabadilika ikawa k**a ya mpira wa kikapu , timu zote zikaacha spaces za kutosha katika mistari yao maana yake nani atakuwa mfanisi kutumia hizo spaces ?
NOTE
1: Diarra kuna saves anafanya zinaonekana nyepesi lakini positioning yake ni nzuri
2: Abdelmonem ni kitasa aisee , nguvu , kasi , akiwa na mali mguuni utulivu wa hali ya juu
3: Leo unaona kabisa kuna energy fulani ilikosekana kwa Al Ahly kwenye kiungo kwasababu ya Dieng kukosekan