03/07/2026
💔 RECHO DANGWA, NIKOSEE LAKINI USINIPOTEZE KABISA💔
Recho, umbali au kuwa nje ya nchi usiwe sababu ya kuacha kabisa yale mazuri yaliyowahi kutuunganisha. Maisha yana vipindi vyake, watu hubadilika, mazingira hubadilika, lakini kumbukumbu nzuri hubaki kuwa sehemu ya historia ambayo haiwezi kufutika kirahisi. Kumbuka uliniambia Mjomba wako yupo Kigoma na ulivyoniaga kwenda Zanzibar iliniuma lakini bado nilikuwa nakupenda! Ulivyoanza kubadilika na kutukana mimi nilinyamaza.
K**a nilikukosea kwa namna yoyote ile, leo naomba msamaha kwa moyo wa dhati. Wanasema anayesamehe si dhaifu, bali ni mwenye nguvu zaidi ya hasira zake.
Mpenzi wangu Recho Dangwa; Allah anasema katika Qur'an: *"Na wasamehe na wapuuze. Je, hampendi Allah akusameheni?"* (Surat An-Nur 24:22) *"Na suluhu ni bora."* (Surat An-Nisa 4:128) Mimi naamini kuwa tofauti za maoni hazipaswi kuzika kabisa kumbukumbu nzuri za jana. Nakukumbuka, nakukosa, na bado naamini kuwa mlango wa mazungumzo haupaswi kufungwa milele.
Marafiki, ndugu na wote wanaosoma ujumbe huu, nawaomba mnisaidie kuniombea msamaha ikiwa nilikosea lakini hata yeye ni shahidi kuwa aliwahi kunikosea shangazi yake wa Dodoma alihusika kusuluhisha, na kumwambia kuwa moyo wa kusamehe hujenga zaidi kuliko moyo wa kuadhibu.
Recho, Ujumbe huu haijalishi utakufikia ukiwa na mwenzangu au ukiwa mwenyewe, ila tambua kuwa Hamisi bado anakupenda, fahamu kuwa kuna watu wanaamini kuwa maridhiano ni bora kuliko migogoro, na kumbukumbu nzuri zina thamani kuliko tofauti zilizopita.Naomba come again my Love kumbuka tuliyopitia Dsm, kumbuka nilivyokuwa naongea na marafiki zako juu yako.
Miss you my lovely wife RECHO DANGWA. Karibu nyumbani wakati wowote moyo wako utakaporuhusu.❤️