Jamvi la habari

  • Home
  • Jamvi la habari

Jamvi la habari Gazeti Bora la Kiswahili lenye kuhabarisha, kuelimisha, kuburudisha na Kufunza. Tuwasiliane kupitia :

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa...
14/07/2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka kwenye picha ya pamoja na Mawaziri mara baada ya Kikao cha mwisho cha Baraza la Mawaziri cha Serikali ya Awamu ya Sita kilichofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Julai, 2025.

Mawaziri, Makatibu Wakuu pamoja na viongozi wengine wakiwasili Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Julai, 2025 kwa aj...
14/07/2025

Mawaziri, Makatibu Wakuu pamoja na viongozi wengine wakiwasili Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Julai, 2025 kwa ajili ya kuhudhuria Kikao cha mwisho cha Baraza la Mawaziri cha Serikali ya Awamu ya Sita kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba 2025.

Hii ni habari kwa ufupi kwa wale ambao hawajaangalia PSG alivyokandwa na Chelsea kupitia hii picha nadhani mtakuwa mshaj...
14/07/2025

Hii ni habari kwa ufupi kwa wale ambao hawajaangalia PSG alivyokandwa na Chelsea kupitia hii picha nadhani mtakuwa mshajua mechi ilikuaje 😅

Powered by: 🍺

PSG wamepokea kipigo ndani ya pitch na nje ya pitch ni huzuni kwa kweliChelsea Bingwa mpya wa FIFA CLUB WORLD CUP hili n...
13/07/2025

PSG wamepokea kipigo ndani ya pitch na nje ya pitch ni huzuni kwa kweli

Chelsea Bingwa mpya wa FIFA CLUB WORLD CUP hili ni kombe lake la pili kwa mashindano hayo pia ni kombe la kwanza toka kombe hilo liboreshwe msimu huu ivyo Chelsea inakuwa timu ya kwanza kuwa bingwa wa kombe hili jipya

FT’ Chelsea 3 - 0 PSG

✍🏼

PSG wamepokea kipigo ndani ya pitch na nje ya pitch ni huzuni kwa kweliChelsea Bingwa mpya wa FIFA CLUB WORLD CUP hili n...
13/07/2025

PSG wamepokea kipigo ndani ya pitch na nje ya pitch ni huzuni kwa kweli

Chelsea Bingwa mpya wa FIFA CLUB WORLD CUP hili ni kombe lake la pili kwa mashindano hayo pia ni kombe la kwanza toka kombe hilo liboreshwe msimu huu

FT’ Chelsea 3 - 0 PSG

✍🏼

Hii inaitwa mgeni hataki soda anataka mia 6 yake 🙌🏻HT’ Chelsea 3 - 0 PSG
13/07/2025

Hii inaitwa mgeni hataki soda anataka mia 6 yake 🙌🏻

HT’ Chelsea 3 - 0 PSG

Rais wa zamani wa Nigeria, Muhammed Buhari, amefariki dunia leo Julai 13, 2025 wakati akipatiwa matibabu jijini London.B...
13/07/2025

Rais wa zamani wa Nigeria, Muhammed Buhari, amefariki dunia leo Julai 13, 2025 wakati akipatiwa matibabu jijini London.

Buhari aliyeiongoza Nigeria mara mbili k**a mkuu wa jeshi na rais amefariki akiwa na umri wa miaka 82, Shirika la Habari la AP limemnukuu katibu wake wa habari, Bashir Ahmad leo Jumapili.

Kupitia akaunti yake ya X (zamani Twitter) Ahmad ameandika: “INNA LILLAHI WA INNA ILAIHIR RAJI’UN.
Familia ya rais huyo wa zamani imetangaza kufariki kwa Muhammadu Buhari, GCFR, mchana wa leo katika kliniki moja mjini London. Mwenyezi Mungu ampokee katika Aljannatul Firdaus, Amin.”

Ikumbukwe Buhari aliingia madarakani mwaka 2015, akisimamia kipindi kibaya zaidi cha uchumi nchini humo na kupambana na uasi.

Kwa mujibu wa tovuti rasmi ya Ikulu ya Nigeria, Buhari alizaliwa Desemba 17, 1942, huko Daura, Jimbo la Katsina, Nigeria. Alilingia jeshini akiwa na umri mdogo mwaka 1961 na kupata mafunzo nchini Nigeria, Uingereza, India na Marekani.

Katika kipindi chote cha utumishi wake jeshini, alishikilia nyadhifa mbalimbali muhimu za k**andi na wafanyakazi, akipanda vyeo na kufikia Meja Jenerali.

Katibu wa NEC,Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi CCM CPA. Amos Makalla akiongea na Wandishi wa Habari leo...
13/07/2025

Katibu wa NEC,Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi CCM CPA. Amos Makalla akiongea na Wandishi wa Habari leo July 13 2025 katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM Dodoma amesema hakuna Mtia Nia yeyote aliyeenguliwa kwenye nafasi za kuomba kugombea nafasi za Udiwani au Ubunge.

CPA. Makalla amesema mchakato bado unendelea ndani ya Chama na sasa Sekretarieti ya Chama hicho inaendelea kupokea taarifa kutoka Mikoani kisha kwenda Kamati kuu na baadae taarifa rasmi itawekwa wazi.

“Naomba nisisitize, kwa utaratibu wetu wa Chama cha Mapinduzi mpaka sasa hakuna Mtu ambaye ameenguliwa au kukatwa k**a ambavyo inaripotiwa kwenye Vyombo vya Habari, nimeona ( wameandika ) huyu kapenya au huyu kafyekwa, huyu hayupo kwenye tatu bora, k**a nilivyosema mchakato huu wa uteuzi utahitimishwa na kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi hapo ndio itakuwa mwisho wa kupata majibu ya mchakato mzima wa Wagombea wanaoteuliwa kwenda katika kura za maoni” - Amos Makalla.

“Kamati Kuu itakapohitimisha tutatoka kuwaambia walioteuliwa kwenda katika kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi, zamani nyie mnajua ilikuwa Watu wote wakigombea wote wanakwenda kupigiwa kura za maoni kwahiyo tumesema utaratibu wa sasa watateuliwa wachache ili kwenda kupigiwa kura za maoni” - Makalla.

13/07/2025
MAJALIWA AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA IBADA YA KUWEKWA WAKFU ASKOFU MTEULE DKT. DANIEL MONOWAZIRI MKUU Kassim Majaliwa le...
13/07/2025

MAJALIWA AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA IBADA YA KUWEKWA WAKFU ASKOFU MTEULE DKT. DANIEL MONO

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Julai 13, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ibada ya kumweka wakfu na kumuingiza kazini Askofu Mteule Dkt. Daniel Henry Mono wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Mwanga.

Ibada hiyo imefanyika katika kanisa la KKKT Dayosisi ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Lionel Andres Messi aweka record mpya ligi kuu ya marekani MLS kwa kufunga magoli 2 kwenye mechi 5 mfululizo na kumfanya...
13/07/2025

Lionel Andres Messi aweka record mpya ligi kuu ya marekani MLS kwa kufunga magoli 2 kwenye mechi 5 mfululizo na kumfanya kufikisa idadi ya magoli yake yote 872 huku akiwa na assist 385

⚽️ ⚽️ vs Montréal
⚽️⚽️ vs Columbus
⚽️⚽️ vs Montréal
⚽️⚽️ vs New England
⚽️⚽️ vs Nashville

Hivi sasa Messi ndio kinara wa magoli ligi kuu ya marekani MLS ana magoli 16 na assist 8

Powered by: 🍺

✍🏼

Address


Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jamvi la habari posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Jamvi la habari:

Shortcuts

  • Address
  • Telephone
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share

SGR

"Miaka 120 ikiyopita Wakoloni waliona umuhinu wa kujenga reli na sisi kuelekea uchumi wa viwanda tunajenga Reli ya SGR huwezi kutenganisha Viwanda na Reli"-Masanja Kadogosa Mkurugenzi TRC