Dsfdhghgjg

Dsfdhghgjg Karibuni

15/07/2025

PSG KUVUNJA REKODI: OFA YA €250M KWA COLE PALMER YAWEKA HISTORIA MPYA YA USAJILI!

Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni, Paris Saint-Germain (PSG) wanapanga kutoa ofa ya kuvunja rekodi ya dunia ya €250 milioni ili kumnasa kiungo Mshambuliaji wa Chelsea, Cole Palmer. Hii ni zaidi ya ofa ya awali ya €200 milioni ambayo PSG walikuwa tayari kuwasilisha kwa Chelsea. Kwa sasa, Chelsea wameweka bei ya €250 milioni kwa Palmer, wakionyesha kuwa hawako tayari kumuuza kwa kiasi chochote chini ya hicho.

Cole Palmer, ambaye alijiunga na Chelsea kutoka Manchester City mnamo 2023 kwa ada ya £40 milioni, aliibuka kuwa Mchezaji muhimu katika kikosi cha The Blues. Katika msimu wa 2024/25, alifunga mabao 27 na kutoa pasi 15 za mabao katika mashindano yote, akichangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya Chelsea kushinda UEFA Conference League na FIFA Club World Cup.

Kwa sasa, mashabiki wa soka wanapaswa kusubiri kuona ikiwa PSG wataweza kuvunja Benki na kumshawishi Chelsea kumuuza Nyota wao.

Toa maoni yako


15/07/2025

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imepangwa kwenye Kundi C kwenye droo ya makundi ya kombe la Mataifa Afrika iliyofanyika usiku huu katika ukumbi wa Kimataifa wa Mohammed V uliopo Rabat jijini Morocco. Stars imepangwa Kundi c sambamba na Nigeria, Tunisia na Uganda.

Makundi ya AFCON 2025 itakayofanyika kuanzia Desemba 21, 2025 hadi Januari 18, 2025 ni k**a ifuatavyo:

Group A: Morocco, Mali, Zambia, Comoros

Group B: Egypt, South Africa, Angola, Zimbabwe

Group C: Nigeria, Tunisia, Uganda, Tanzania

Group D: Senegal, DR Congo, Benin, Botswana

Group E: Burkina Faso, Equatorial Guinea, Sudan

Group F: Ivory Coast, Cameroon, Gabon, Mozambique

15/07/2025

Mwenyekiti wa Shirikisho la Klabu Afrika (ACA), ambaye pia ni Rais wa Yanga, Hersi Said, amesema sasa ni wakati wa kuanza kufanya kazi ya klabu na kujenga uimara kwa maslahi mapana ya mpira wa miguu.

Hersi amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kusaini makubaliano ya kuweka Makao Makuu ya ACA ambayo yatakuwa jijini Rabat nchini Morocco

“Shukran za dhati kwa wenyeji wetu, Shirikisho la Mpira la Falme ya Morocco, hususan Rais Fouzi Lekjaa” ameandika Hersi

(Imeandaliwa na )

Address


Telephone

+255693640639

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dsfdhghgjg posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share