
03/08/2025
TANZIA.
Katibu Mkuu wa Kanisa la Moravian Tanzania, Jimbo la Kusini, kwa niaba ya Halmashauri Kuu ya Jimbo, anatangaza kwa masikitiko makubwa kifo cha mfanyakazi wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini, Ndugu Furaha Baraka Kamwela.
Ndugu Kamwela amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Marehemu alikuwa mfanyakazi wa Kanisa katika Idara ya Fedha KMT-JK na Mazishi yanatarajiwa kufanyika Iwambi, Mbeya, siku ya Jumanne tarehe 5 Agosti 2025.
"Mungu ampumzishe kwa amani. Amen."
Imetolewa na:
Mch. Stephen Mwaipopo
Katibu Mkuu – Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini
Njiwa Media tutaendelea kukuletea taarifa zaidi kuhusiana na msiba huu.