N-point

N-point nPOiNT is an Online content platform which delivers content across a range of smart devices.
(1)

It offers content beyond news, guaranteeing the best user experience to its customers.

Mahak**a Kuu ya Tanzania, Masijala Ndogo ya Dar es Salaam imeahirisha Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa (CHADEMA...
24/10/2025

Mahak**a Kuu ya Tanzania, Masijala Ndogo ya Dar es Salaam imeahirisha Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa (CHADEMA), Tundu Lissu hadi Novemba 3, 2025, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuendelea kutokana na kukosekana kwa Shahidi.

Wakili wa Serikali Mkuu Renatus Mkude aliieleza Mahak**a kuwa upande wa Jamhuri ulikuwa tayari umeshatoa ushahidi kupitia mashahidi watatu, lakini shahidi wa tatu, Mkaguzi wa Polisi na Mtaalamu wa Uchunguzi wa Kielektroniki Samwel Kaaya, alishindwa kuwasilisha vielelezo vyake vya flash disk na memory card baada ya Mahak**a kukataa kuvipokea.

“Kwa sasa hatuna shahidi mwingine aliye tayari kutoa ushahidi kwa kuwa waliopangwa wanatoka nje ya Dar es Salaam na wanahitaji maandalizi zaidi. Kwa mujibu wa kifungu cha 302 cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (CPA), tunaomba ahirisho,” alisema Mkude.

Kwa mujibu wa Wakili huyo wa Serikali, tarehe 3 Novemba 2025 ilikuwa tayari imepangwa katika ratiba ya kesi hiyo, hivyo aliomba shauri hilo liendelee siku hiyo.

Hata hivyo, Lissu alipinga ombi hilo la kuahirishwa akidai kuwa sababu zilizotolewa na upande wa Jamhuri hazina msingi wa kisheria.

Kutokana na hatua hiyo, Jaji Ndunguru, alisema Mahak**a imezingatia hoja za pande zote mbili na kubaini kuwa ombi la kuahirisha lina msingi wa kisheria kwa kuwa upande wa mashtaka haujawahi kukosa shahidi tangu shauri lianze, hivyo kesi inaahirishwa hadi Novemba 3, 2025.

Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara anawania muhula wa nne katika uchaguzi wa siku ya Jumamosi, akiahidi kuendeleza uk...
24/10/2025

Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara anawania muhula wa nne katika uchaguzi wa siku ya Jumamosi, akiahidi kuendeleza ukuaji thabiti huku wakosoaji wakilaani kile wanachoeleza k**a jitihada za serikali yake za kukandamiza upinzani.

Uchaguzi katika nchi hiyo mzalishaji mkubwa wa kakao duniani unawakutanisha Ouattara, 83, dhidi ya mawaziri wawili wa zamani wa serikali pamoja na mke wa zamani na msemaji wa zamani wa mtangulizi wake, Laurent Gbagbo.

Ouattara ndiye mgombea pekee anayeungwa mkono na chama chenye nguvu cha kisiasa, na hivyo kumfanya kuwa kipenzi wengi.

Wapinzani wengine wawili mashuhuri, Gbagbo na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Credit Suisse Tidjane Thiam, walizuiwa kushiriki.

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kusitisha mara moja mazungumzo yote ya kibiashara na Canada, akitaja tangazo la...
24/10/2025

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kusitisha mara moja mazungumzo yote ya kibiashara na Canada, akitaja tangazo la televisheni lililotumia sauti ya Rais wa zamani Ronald Reagan akipinga sera za ushuru k**a kichocheo cha uamuzi huo.

Kupitia chapisho kwenye mtandao wake wa Truth Social, Trump alisema tangazo hilo, lililodhaminiwa na serikali ya jimbo la Ontario, limeonyesha “mwenendo wa kukera” unaolenga kuingilia masuala ya ndani ya Marekani.

“Kwa kuzingatia tabia yao isiyokubalika, MAZUNGUMZO YOTE YA KIBIASHARA NA KANADA YAMEKOMA KUANZIA SASA,” aliandika Trump Alhamisi usiku.

Rais huyo ameweka kodi ya asilimia 35 kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Kanada, ingawa ameidhinisha msamaha kwa bidhaa fulani zilizo chini ya Makubaliano ya Biashara Huria ya Amerika Kaskazini (USMCA) mkataba wa kibiashara kati ya Marekani, Kanada na Mexico alioufanyia marekebisho katika muhula wake wa kwanza.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wakubaliana kuisaidia Ukraine kifedha katika kipindi kingine cha miaka miwili.Lakini hata hiv...
24/10/2025

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wakubaliana kuisaidia Ukraine kifedha katika kipindi kingine cha miaka miwili.

Lakini hata hivyo wameshindwa kutoa mamilioni ya fedha za Urusi zilizozuiwa ili kutoa ufadhili wa ulinzi wa nchi hiyo

Katika mkutano wao wa jana viongozi hao waliahirisha uamuzi wao wa kutumia kiasi ya Euro bilioni 140 za mali ya Urusi zinazoshikiliwa nchini Ubelgiji hadi hapo Desemba.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameeleza mkutano huo wa Ubelgiji kwamba hatua hiyo italeta matokeo chanya. '' Ningependa kuwashukuru viongozi wote wa Ulaya kwa mosimamo yao thabiti kupitia vikwazo waliyoweka, alisema.

Mkutano huo wa Brussels ulifanyika jana wakati kukitarajiwa kufanyika mkutano mwingine huko London ambako Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer anatarajiwa kuwahimiza viongozi wa Ulaya kuongeza kupeleka vifaa vya kijeshi nchini Ukraine.

Mama wa taifa wa kwanza wa Ghana Nana Konadu Agyeman-Rawlings ameripotiwa kufariki dunia akiwa na umri wa miaka 76.Taaar...
23/10/2025

Mama wa taifa wa kwanza wa Ghana Nana Konadu Agyeman-Rawlings ameripotiwa kufariki dunia akiwa na umri wa miaka 76.

Taaarifa zinasema amefariki mapema leo Alhamisi, 23 Oktoba, katika Hospitali ya Ridge huko Accra.

Shirika la serikali la Utangazaji la Ghana limeshirikisha ujumbe kwenye Jukwaa la X, kutangaza kufo chake.

Nana Konadu Agyeman-Rawlings alikuwa mama wa taifa wa kwanza kutoka Juni 4, 1979, hadi Septemba 24, 1979, chini ya Baraza la Mapinduzi la Wanajeshi (AFRC), na tena kutoka Desemba 31, 1981, hadi Januari 6, 1993, chini ya Baraza la Ulinzi la Kitaifa (PNDC).

Aliendelea kuhudumu k**a mwanamke wa kwanza kutoka Januari 7, 1993, hadi Januari 6, 2001, na kutamatisha muda mihula miwili chini mfumo mpya wa demokrasia wa kaunti.

Ujumbe wa salamu za rambirambi unaendelea kutumwa kwa haraka katika mitandao ya kijamii kufuatia taarifa za kifo chake.

23/10/2025

Mahak**a Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam, imeikataa ripoti ya uchunguzi wa uhalisia wa picha mjongeo (video clip) ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, anayekabiliwa na kesi ya uhaini, yenye maudhui yanayodaiwa kuwa ya uhaini.

Upande wa mashtaka katika kesi hiyo jana Jumatano, Oktoba 22, 2025 kupitia shahidi wake wa tatu iliiomba mahak**a iipokee ripoti hiyo kuwa kielelezo cha ushahidi wa upande wa mashtaka.

Hata hivyo, Lissu aliweka pingamizi dhidi ya ripoti hiyo isipokewe akidai shahidi huyo hana mamlaka ya kisheria kuiwasilisha mahak**ani wala kuiandaa ripoti hiyo kwa kuwa si mtaalamu wa uhalifu wa kimtandao.

Licha ya upande wa mashtaka kupinga hoja zake kuwa hazina mashiko kisheria, lakini Mahak**a katika uamuzi wake leo Alhamisi Oktoba 23, 2025 imekubaliana na pingamizi lake baada ya kuridhia na hoja zake, hivyo ikaikataa ripoti hiyo ikieleza kuwa shahidi huyo hana mamlaka ya kisheria kuwasilisha ripoti hiyo kwa kuwa si mtaalamu wa masuala ya uhalifu mtandao.

23/10/2025

Tume ya Kitaifa ya Uwiani na Maridhiano nchini Kenyac(NCIC) imemtaka Gavana wa Nyeri, Mutahi Kahiga, kutoa maelezo rasmi kuhusu kauli zake zilizozua utata kuhusu kifo cha aliyekuwa kinara wa ODM Raila Odinga.

Kauli hizo zimezua hasira kubwa nchini Kenya, hasa baada ya Kahiga kusema kuwa kifo cha Odinga ni “mpango wa Mungu” ili kanda ya Mlima Kenya ipate faida kutoka kwa rasilimali za serikali ambazo zilikuwa zikitumika sehemu nyingine.

Kahiga alidai kuwa makubaliano ya kisiasa kati ya Rais William Ruto na marehemu Odinga yalibadilisha vipaumbele vya maendeleo ya serikali kuelekezwa zaidi katika kanda ya Nyanza, hali inayodaiwa kumfanya mkoa wa Mlima Kenya kupoteza fursa za kimaendeleo.

Tume ya NCIC imesema kuwa kauli hizo ziliharibu kwa kiasi kikubwa juhudi zilizofanywa kudumisha amani na mshik**ano wa kitaifa, na kwamba Gavana Kahiga anapaswa kuwajibishwa kwa kuwa ni mtu anayeongoza katika nafasi ya umma.

Katika taarifa yao ya Jumatano, Tume ilionya kuwa kauli k**a hizo si tu zinahuzunisha kumbukumbu za shujaa wa taifa, bali pia zinaweza kuchochea migogoro ya kikabila na mivutano ya kijamii wakati taifa linapolia kiongozi wake wa zamani.

23/10/2025

Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza rasmi vikwazo vipya dhidi ya baadhi ya makampuni makubwa ya mafuta kutoka Urusi, hatua inayolenga kuongeza shinikizo kwa serikali ya Rais Vladimir Putin kufuatia kuendelea kwa mvutano wa kisiasa.

Vikwazo hivyo vinahusisha kufungia mali za makampuni kadhaa na kuzuia biashara ya mafuta kati ya Urusi na washirika wake wa kimataifa.

Hatua hiyo imesabisha kupanda kwa bei ya mafuta duniani, huku wachambuzi wakionya kuwa inaweza kuongeza gharama za nishati katika nchi nyingi.

Serikali ya Urusi imelaani hatua hiyo, ikidai kuwa Marekani inajaribu kutumia nguvu za kiuchumi k**a silaha ya kisiasa.

Hata hivyo, Ikulu ya Marekani imesisitiza kuwa vikwazo hivyo ni sehemu ya juhudi za kulinda maslahi ya kimataifa na kudhibiti ufadhili wa kijeshi wa Urusi.

Mkurugenzi wa Sheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Gaston Garubindi ambaye alikuwa anafuatilia kuk**at...
22/10/2025

Mkurugenzi wa Sheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Gaston Garubindi ambaye alikuwa anafuatilia kuk**atwa kwa John Heche, amesema baada ya kufika Polisi wameambiwa tayari Heche amesafirishwa mchana huu kwenda Tarime.

Akiongea na Waandishi wa Habari leo October 22,2025, Gaston amesema “Heche ambaye asubuhi alik**atwa Mahak**ani na Polisi, taarifa ya Polisi inasema kweli wamemk**ata kwa makosa ambayo hawajayasema lakini anasema jambo la Heche halipo Dar es salaam lipo Tarime na anadai tayari wamemsafirisha Heche kutoka Dar kwenda Tarime”

“K**a Chama tunajipanga kuagiza Mawakili waliopo Mara na Mwanza ili waelekee huko kutoa huduma za kisheria kwa Heche”.

Mahak**a Kuu Masjala Ndogo jijini Dar es Salaam imekubaliana na pingamizi lililowasilishwa na Mwenyekiti wa Chama cha De...
22/10/2025

Mahak**a Kuu Masjala Ndogo jijini Dar es Salaam imekubaliana na pingamizi lililowasilishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, na kukataa kupokea ‘flash disk’ na ‘memory card’ zilizokuwa zimetolewa k**a vielelezo mahak**ani.

Uamuzi huo umetolewa leo na jopo la majaji watatu likiongozwa na Jaji Dustan Nduguru, baada ya mahak**a kubaini kuwa shahidi wa upande wa mashtaka ambaye ni Mkaguzi wa Polisi hakuwa mtaalamu wa picha za mjongeo (video), bali ni mtaalamu wa picha mnato pekee.

Israel imepokea miili miwili ambayo Hamas inasema ni mateka wengine wawili waliofariki ambao walikuwa wamezuiliwa huko G...
22/10/2025

Israel imepokea miili miwili ambayo Hamas inasema ni mateka wengine wawili waliofariki ambao walikuwa wamezuiliwa huko Gaza.

Jeshi la Israel limesema majeneza mawili yalikabidhiwa kwa wanajeshi katika ardhi ya Palestina na shirika la Msalaba Mwekundu ambalo hapo awali lilipokea kutoka kwa Hamas.

Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilisema majeneza hayo, ambayo yalisindikizwa na wanajeshi, yalikuwa yamevuka hadi Israel na yatachukuliwa kutambuliwa rasmi Tel Aviv.

Kuthibitishwa kwa utambulisho wao kutamaanisha kuwa Hamas imewahamisha mateka 15 kati ya 28 wa Israel waliofariki dunia chini ya awamu ya kwanza ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosimamiwa na Marekani mapema mwezi huu.

Mateka wote 20 walio hai waliachiliwa muda mfupi baada ya kufikiwa kwa makubaliano hayo.

Tume ya Uchaguzi ya Uganda imetangaza tarehe 15 Januari 2026 k**a tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo, ambapo Rais Yowe...
22/10/2025

Tume ya Uchaguzi ya Uganda imetangaza tarehe 15 Januari 2026 k**a tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo, ambapo Rais Yoweri Museveni atataka kuongeza muda wa Utawala wake hadi karibu nusu karne.

Kwa sasa ndiyo Kiongozi wa nne barani Afrika aliyeongoza kwa muda mrefu zaidi, Serikali ya Museveni imebadilisha Katiba mara mbili ili kuondoa ukomo wa umri na muda, na kumruhusu kusalia madarakani tangu 1986.

K**a ilivyokuwa katika Uchaguzi wa 2021, Mpinzani Mkuu wa Museveni anatarajiwa kuwa Mwanasiasa wa Pop mwenye umri wa miaka 43, Bobi Wine, ambaye amedhihirisha uimbaji wake ili kupata msingi mkubwa wa kuungwa mkono miongoni mwa wapiga kura vijana.

Katika Uchaguzi wa 2021, Wine alipata 35% ya kura, wakati Museveni ni 58%.

Wine alidai ushindi wake uliibiwa, lakini Tume ya Uchaguzi ilikanusha madai hayo.

Address

Kimweri Street

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when N-point posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to N-point:

  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share