SPARK LIGHT TV

  • Home
  • SPARK LIGHT TV

SPARK LIGHT  TV Kwa Habari zote kali za Ndani na Nje ya Nchi,Uchumi ,Biashara ,Burudani na Michezo

Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM TAIFA Ndg. Jessica Mshama amesema Chama Cha Mapinduzi kinajali sana u...
11/07/2025

Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM TAIFA Ndg. Jessica Mshama amesema Chama Cha Mapinduzi kinajali sana uwezo wa Vijana katika uongozi ndio maana kinawaamini na kuwapa nafasi za juu za kiuongozi.

Ndg. Jessica ameonesha uthabiti wa CCM katika uongozi wake kwa kuitofaugisha na vyama vingine kutokana na kuwaamini Vijana katika nafasi mbalimbali za kiuongozi na kwamba ushindi wa CCM hautokani kwa bahati mbaya kwa sababu kimejenga zaidi kwa Vijana.

Kuhusu suala la Uchaguzi, Ndg. Jessica Mshama amesema kuwa Viongozi wa Juu wa Jumuiya ya UVCCM wamekuwa wakiratibu Mikutano inayohusisha Ziara zao katika Mikoa mbalimbali kwa ajili ya kuhamasisha Vijana kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali pamoja na kujiandaa kupiga kura ifikapo Oktoba 2025.

Ndg. Jessica Mshama aliyasema hayo wakati wa mahojiano na Watangazi wa Kipindi cha Sentro cha Clouds Tv kilichofanyika Jana 08 Julai, 2025 katika studio za Clouds Tv Jijini Dar es Salaam.

09/07/2025

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli PURA Mhandisi Charles Sangweni amesema hali ya upatikanaji wa Gesi asilia Nchini umezidi kuimarika hadi kufikia futi za ujazo zaidi ya Tilioni 57.54

Mhandisi Sangweni ameyabainisha hayo mara baada ya Kutembelea Banda la Mamlaka hio katika Maonesho ya 49 ya Biashara Kimataifa Dar es salaam Sababasa.

"Kuna miradi mikubwa hivi karibuni inakuja kuna mradi wakuchimba visima vinavyotoa gesi na vyakuzalisha vitakavyochimbwa mkoa wa Mtwara na tunategeme kutoandani muda kutoka kwenye uzalishaji wa kawaida wa kwa siku" amesem Sangweni

09/07/2025

Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini amesema Wizara hiyo inawahakikishia wananchi kuwa huduma za msaada wa Kisheria zitakuwa endelevu kwani uzoefu uliopatikana wakati wa Utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia umeonesha huduma hiyo ni hitaji kubwa kwa wananchi.

Mhe. Sagini ameyasema hayo leo Julai 8, 2025 katika maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2025) mara baada ya kutembelea banda la kutolea huduma la Wizara na mabanda ya Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo.

“Baada ya uzoefu wa miaka minne tumeridhika kuwa huduma ya Msaada wa kisheria inahitajika na ndio maana Wizara ya Katiba na Sheria inalifanya jambo hili kuwa endelevu kwa kuwapeleka maafisa ngazi ya halmashauri ili wawasaidie wananchi, Pia tunashirikiana na wadau wengine k**a Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kutoa huduma za Msaada wa kisheria pamoja na maafisa Ardhi wa Mikoa kuwaeleimisha wananchi juu ya sheria ya ardhi ili kupunguza migogoro”, amesema Mhe Sagini.



08/07/2025

Wananchi wametakiwa kuzingatia ubora wa bidhaa wanazozalisha, hasa zile zinazouzwa kupitia Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), kwa kuwa bidhaa hizo zimekuwa zikiuzwa hata katika masoko ya kimataifa na hivyo kuchangia kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa TEHAMA wa TMX, Goodluck Luhanjo, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Aidha, ametoa wito kwa sekta binafsi kuendelea kushirikiana na serikali katika kuwekeza kwenye ujenzi wa maghala maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa mazao ya kilimo, na kuwasihi wananchi waendelee kufuatilia taarifa sahihi kupitia tovuti ya TMX pamoja na kutembelea banda lao kwenye maonesho ya Sabasaba ili kupata elimu zaidi.

Pia ameeleza moja ya majukumu makuu ya TMX ikiwa ni pamoja na kuhakikisha bei za bidhaa zinafunguliwa kwa uwazi kupitia mfumo wa ushindani.
tz

Mkurugenzi wa VETA, CPA Anthony Kasore, asema watoto wadogo wanapaswa kuanza kujifunza ujuzi mapema ili kuwa na ufanisi ...
08/07/2025

Mkurugenzi wa VETA, CPA Anthony Kasore, asema watoto wadogo wanapaswa kuanza kujifunza ujuzi mapema ili kuwa na ufanisi katika maisha ya baadaye.



‎Leo, tarehe 7 Julai 2025, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi  (VETA)Anthony, amesisitiza umuhimu wa kuanzisha watoto wadogo kwenye ujuzi wa maisha mapema ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi na kijamii.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi huyo alieleza kuwa mfumo wa elimu nchini umeendelea kuboreshwa ili kutoa fursa kwa kila mtoto kupata elimu ya vitendo inayoweza kumuwezesha kujitegemea na kuleta mabadiliko kwa jamii.

‎‎‎Akizungumzia sera mpya ya elimu, Kasore amesema kuwa katika mwaka 2023, Serikali ilifanya maboresho kwenye sera ya elimu, na mwaka huu, Rais wa Tanzania alizindua rasmi sera hiyo ya elimu ya ufundi stadi. Sera hii inasisitiza kuanzisha ujuzi kwa watoto kuanzia ngazi ya shule za msingi na sekondari, ambapo wanafunzi watajifunza mbinu za ubunifu na ujasiriamali.


Amesema VETA ni kutoa elimu itakayowasaidia Watanzania kupata ujuzi utakao wawezesha kujiajiri na kushiriki katika uchumi wa nchi. Alisisitiza kuwa ni muhimu kutoa elimu ya ujuzi inayohusisha ubunifu ili watoto wa kizazi cha sasa waweze kuzalisha bidhaa na kufanya biashara zao wenyewe, huku wakijua umuhimu wa kuingia kwenye soko la ajira na kujenga ustawi




Mkuu wa kitengo cha mawasiliano shirika la Maendeleo ya Petroli na gesi TPDC Maria Mselemu amesema kufuatia utendaji kaz...
07/07/2025

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano shirika la Maendeleo ya Petroli na gesi TPDC Maria Mselemu amesema kufuatia utendaji kazi la shirika hilo umewafanya kuibuka kidedea kwenye maonesho ya 49 ya biashara ya kimataifa maarufu k**a sabasaba.

Akizungumza mara baada ya kupewa tuzo hiyo katika maonesho ya 49 ya biashara ya kimataifa amesema wamekuwa wakifanya vizuri kwenye maeneo tofauti na kupelekea kupata tuzo mbalimbali.

"Kwetu hii ni tuzo ya tano kwenye maonesho haya lakini sisi kwetu hii ni kawaida kwani tumekuwa tukipata tuzo kwenye maeneo taofauti ikiwemo tuzo ya mazingira",amesema Mselemu.

Akizungumzia tuzo hiyo ya mazingira amesema kufuatia matumizi ya nishati safi ya kupikia wameweza kuondoa hewa ukaa kwa tani laki moja.

"Kwa kutumia nishati safi ambayo tunaweka kwenye magari lakini pia kupikia pia kufanyakazi kwa umakini ndio kichocheo cha kutufanya kuwa kinara na hata kupatata tuzo kadhaa"ameongeza.



07/07/2025

TIKA kuhakikisha watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limetoa zawadi ya majiko ya umeme kwa Wananchi waliofika katika banda lao lililopo kwenye Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa maarufu sabasaba.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 7,2025 katika viwanja vya maonesho hayo, Mkurugenzi Mtendaji Tanesco, Lazaro Twange amesema wananchi waliofika katika banda lao wamepata fursa ya kupata elimu juu ya umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia na kisha kupatiwa zawadi ya majiko ya umeme.

Amesema katika banda la Tanesco kuna majiko hayo ya umeme na wananchi waliojibu vema maswali waliyoulizwa wamepata fursa ya kujishindia zawadi ya majiko hayo kwa ajili ya kuyatumia katika kupikia.

“Ni maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan kwamba watanzania tuhame kwenye kutumia nishati isiyokuwa safi na kutumia iliyosafi, hivyo hapa tunazungumzia nishati ya umeme na tuna majiko haya ya umeme yamefanyiwa utafiti na kuthibitika kuwa yanaweza kupikia na chakula kikaiva kwa kutumia chini ya Unit moja,



07/07/2025

Wizara ya katiba na Sheria imepokea tuzo ya Mshindi wa Kwanza miongoni mwa wizara zote zilizo shiriki katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendeles katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es salaam.

Tuzo hiyo imetolewa leo na Rais wa Serikali ya Zanzibar, Mhe Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati ufunguzi ramsi ws maonyesho hayo.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dktm Franklin Jasson Rwezimula amewapongeza watumishi Kwa jitahada zao pamoja na huduma walizozitoa zimewavutis wananchi wengi katika kutoa msaada wa sheria na Elimu kuhusu Katiba.

Naibu Katibu Mkuu Huduma za Hazina Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo ametembelea banda la Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za...
06/07/2025

Naibu Katibu Mkuu Huduma za Hazina Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo ametembelea banda la Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, Bi. Omolo ameipongeza PPAA kwa kuanza matumizi ya Moduli ya kupokea na kushughulikia malalamiko na rufaa katika mfumo wa NeST. Kupitia maonesho hayo, Bi. Omolo amefahamishwa majukumu na mafanikio ya Mamlaka ya Rufani kwa kipindi cha miaka minne chini ya Uongozi wa Serikali ya awamu ya sita.



05/07/2025

Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) limesema kwa mwaka wa fedha 2024/25 limefanya mauzo ya bidhaa cha kiasi cha tani laki saba kumi na tatu mia nane na sita zenye thamani ya Sh tirioni 2.5 .

Hayo ameyasema leo Ofisa Mipango wa Soko la Bidhaa Tanzamia (TMX), Eva Msangi kwenye maonesho ya sababasaba jijini Dar es Salaam ambapo amesema miaka inavyozidi kwenda wanategemea wataongeza bidhaa zaidi ikiwemo mbogamboga na matunda

Aidha, Eva amesema kwa upande wa madini wameanza na madini ya vito ambapo mpaka kufikia sasa wameshafanya minada mitatu ya madini kwa eneo la mererani na muitikio umekuwa mkubwa kwani soko halitaji usafiri .

05/07/2025

Wizara ya katiba na Sheria Kupitia kituo cha Katiba na Ufuatiliaji Haki imeshiriki Maonesho ya ya 49 ya Biashara(Sabasaba) ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa watanzania kuhifamu Katiba na haki zao za msingi.

Akizungumza na waandishi wa habari Wakili wa Serikali kutoka Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki, Doris Dalio amesema mpaka sasa wamehudumia wsty 200 kwenye kitengo cha katiba ambao wamepewa Elimu ya Katiba na wajibu wao wakulinda nchi.

"Tunawaelekeza haki zao za msingi na wajibu wao k**a wananchi ukizingatia tupo katika mwaka wa uchaguzi tunawakumbusha haki yao ya msingi ya kuchaguna kuchaguliwa kwa kujitokeza na kuchagua nafasi mbalimbali" amesema

Ameongeza kuwa watanzania wengi wana shauku ya kuijua katiba na kiu ya kuendelea kujifunza na wao wamejipanga kikamilifu kuhakikisha kila mtanzania anaifahamu katiba n wajibu wake k**a mtanzania.

05/07/2025

Serikali kupitia Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ( DCEA ), mesisitiza kuwekeza nguvu zaidi kwa watu walioathirika na urahibu wa dawa za kulevya, kwa kuwapatia huduma stahiki ikiwemo kuwarudisha katika maisha yao ya kawaida kwa kuwapatia elimu.

Hayo yameelezwa na Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo wakati akizungumza alipotembea katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba, Jijini Dar es Salaam.

Kamishna Lyimo ameeleza kuwa Mamlaka inatoa matibabu bure kwa waraibu wa Dawa hizo.

Ameongeza kuwa, Makakati wa pili wa Mamlaka ni kupunguza uhitaji ambapo kuna watu wanazalisha hapa ndani kwenye mashamba na dawa zingine zinapita katika mbinu za siri ambazo wanazijua wengine tayari wameshawak**ata.

Ameweka wazi, kuwa katika Maonesho Wanatoa elimu Kinga ya kuwalinda jamii endapo watafikiwa na dawa hizo kwa njia zozote wajue madhara yake ambayo wamewaelezea kwenye Elimu wanayotoa.

Address


Alerts

Be the first to know and let us send you an email when SPARK LIGHT TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to SPARK LIGHT TV:

Shortcuts

  • Address
  • Telephone
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share