
26/09/2025
🇰🇵🤝🇮🇱❌
Uhusiano kati ya Korea Kaskazini na Israel umekuwa ukizidi kuzorota kwa miaka mingi. Korea Kaskazini haijawahi kuitambua Israel k**a taifa, na badala yake imekuwa ikitoa kauli kali za kulaani hatua za Israel dhidi ya Wapalestina.
➡️ Pyongyang mara kwa mara imetangaza kuunga mkono taifa huru la Palestina na kulaani mashambulizi ya Israel huko Gaza na Lebanon.
➡️ Pia kumekuwepo na tuhuma kwamba silaha zenye asili ya Korea Kaskazini zimeonekana mikononi mwa makundi ya wapiganaji wa Kipalestina, jambo lililoongeza mvutano.
➡️ Israel nayo inaiona Korea Kaskazini k**a tishio kutokana na uhusiano wake wa karibu na Iran na makundi yanayopinga uwepo wa Israel.
Kwa sasa, hakuna uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizi mbili, na msimamo wa Korea Kaskazini unaendelea kuongeza uhasama na kuzidisha mvutano katika Mashariki ya Kati.