13/01/2026
HUU UKWELI UTAKUUMA LAKINI UTAKUWEKA HURU DAIMA📌
1. THAMANI YAKO HAIPUNGUI ETI SABABU WATU HAWAKUJUI..
Unaweza usithaminiwe na mtu mmoja na hii haimaanishi haufai kwa wengine.
Mfano...ukikosa kuthaminiwa na kikundi fulani basi tambua kuna mahali pengine utaonekana dhahabu,hao waliokuona haufai muda huo...wape muda watakuja kuielewa thamani yako...
2.HAIJALISHI WEWE NI MWEMA KIASI GANI,HAUTAWEZA KUWAFURAHISHA WOTE...
Tambua sio wote watakaothishwa nawe hata ufanye nini...mwanadamu hata ufanye vipi bado hawaridhika nawe hivyo punguza ama acha kuwafurahisha watu..
3.JIULIZE KWANINI WALIJISIKIA KUKUSEMA
Ikiwa watu wameweza kukusema juu ya UBAYA wako...basi ni vyema kuangalia chanzo..
Pale unapoona unasema vibaya,nakushauri fanya uchunguzi kwa huyu mtu aliyechaguliwa kupokea taarifa za UBAYA wako ndipo utaweza kuona na kutambua nani si MWAMINIFU..
4.SIO KILA MTU UNAYEMSAIDIA ATAKUTAKIA MEMA BAADAE..
Wapo wanaotumia wengine kwa ajili ya manufaa yao...
Na ndivyo huenda ikawa imewahi kukutokea pia..wapo wanaokujia wakihitaji msaada wako kifedha au kihisia lakini wanapofanikiwa wanakusahau kabisaa..
5.,IKIWA UPENDO NA JUHUDI ZAKO HAZIPWEI THAMANI,BASI BORA KUONDOKA KWA HESHIMA..
Kuendelea kuwepo mazingira ambayo hauthaminiwi ni kujiumiza..ni vyema kuondoka KIMYA KIMYA ili upate kulinda HESHIMA yako..
Usikubali kupoteza muda mahali ambapo hawaioni thamani, acha kutumia ENERGY yako mahali ambapo hapatakiwi kuendelea kutumika..
6.WALIOANGUKA ZAIDII YA MARA MOJA...NDIO HUPAA KWA NGUVU ZAIDI💪
Siku zote MAUMIVU hufundisha na kutoa SOMO kali katika maisha..
Jifunze kusimama tena imara pale unapoanguka...chukua FUNZO la anguko lako kisha lifanyie kazi na kusonga mbele..
7.TABIA YA KWELI HUONEKANA WAKATI WA SHIDA NA RAHA..
Wapo wanaokuwa wema kwako kipindi wanapohitaji kutoka kwako lakini unapokuwa katika mazingira magumu hutoweka na kujikuta umebaki mwenyewe..
Unapoona hali hii jitahidi kuwa makini sana...
Walio wa kweli wanakuwa nawe katika hali yeyote ile iwe ni umepanda au kushuka,uko nacho ama hauna bado wanakuwa pamoja nawe..
Ukiweza kuzingatia haya machache niliyoeleza hapa...ukweli huu ukiukubali basi utakuwa HURU kabisaa..
Yours,
Jacqueline Ruwaichi
💕💕💕💕💕💕💕💕