
12/08/2025
Chama Cha wananchi CUF kimezindua ilani ya uchaguzi ndani ya wilaya ya MOROGORO Mjini kwaajili ya kueleza changamoto na utekelezaji wa majukumu yao wanayopaswa kuyatekeleza huku wakitangaza majina ya wagombea kwa nafasi ya ubunge ngazi ya majimbo na udiwani ngazi ya kata.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Cuf zilizopo manispaa ya Morogoro mwenyekiti wa CUF wilaya ya MOROGORO Rashid Athuman amesema ilani hiyo imebebba zaidi ya mambo 16 yanayopaswa kutekelezwa kiutawala endapo watapata ridhaa ya kuongoza kutoka kwa wananchi.
“Ilani yetu imejikita zaidi katika mambo makuu 16 lakini kwa ucahhche k**a ajira,miundombinu,afya,elimu uwajibikaji nidhamu katika mamlaka za umma na ulinzi na usalama leo naona idadi ya vijana morogoro katika ajira imekuwa ni changamoto kubwa kwahiyo sisi k**a chama cha siasa tumekuja na tiba jinsi gani tunaweza kutatua kero za wananchi katika masuala hayo ya afya,ajira na miundombinu mana barabara zetu zimekuwa mbovu ,lakini ilani yetu imejikita ni namna gani tutafufua viwanda kwenye mji wetu wa Morogoro, tukichukua dhamana hiyo tutafufua viwanda vyote lakini kipaumbele chetu kingine ni kuweka bandari kavu”Amesema
Aidha mwenyekiti wa chama hicho ametumia nafasi hiyo kutangaza majina ya wagombea waliopitishwa na baraza la CUF mkutano mkuu Taifa katika majimbo 6 kwa nafasi za ubunge kwa jimbo la Ulanga,Malinyi,Kilosa,Kilombero,Morogoro Kusini na Morogoro mjini ambapo katika majimbo hayo wawili ni wanawake na 4 ni wanaume huku wakisimamisha wagombea 19 ngazi ya udiwani kati ya kata 29.
Wagombea hao ni Rashid Athumani Gogomelo kwa jimbo la Morogoro mjini ,jimbo la kilosa ni Sailasi Ramadhani Kasaaro ,kilombero Geogre Cosmas Mwaduha,Ulanga ni Dkt Batuli Salehe ,Morogoro kusini hossein Kiva na Malinyi ni Mwajuma
Nae mkurugenzi wa mipango na uchaguzi wilaya ya Morogoro mjini Nasibu Salum Mbogoya amesema wamejiandaa vema kushiriki katika uchaguzi mkuu na wametoa nafasi kwa makundi ya wanawake na vijana kuweza kugombea nafasi mbalimbali.
“Tumejaribu kugusa makundi mbalimbali katika kuandaa wagombea hususani tumegusa makundi ya wananwake