19/04/2026
Shirika la Umeme nchini (TANESCO) limetoa taarifa ya kuwepo kwa hitilafu ya dharura katika sehemu ya mfumo wa Gridi ya Taifa, hali iliyosababisha kukatika kwa huduma ya umeme katika baadhi ya Mikoa nchini.
Mikoa iliyoathirika ni pamoja na Dodoma, Njombe, Mbeya, Simiyu, Ruvuma, Geita, Shinyanga, Mara, Mwanza, Tabora, Songwe, Kilimanjaro, Arusha, Iringa pamoja na maeneo ya jirani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma TANESCO, hitilafu hiyo imetokea saa 11:38 jioni na kusababisha kukosekana kwa umeme katika maeneo hayo kwa muda.
Aidha shirika hilo limeomba radhi kwa usumbufu uliosababishwa na kukatika kwa umeme na linawaomba wateja kuwa wavumilivu wakati jitihada za kurejesha huduma hiyo zikiendelea.