10/03/2023
MUME AMUUA MKEWE NA KUMFUKIA CHUMBANI
๐ฃMwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Salima Maulid mkazi wa Mtaa wa Mbilani Kata ya Kidogo Chekundu Manispaa ya Tabora, ameuawa na mtu anayedaiwa kuwa ni mumewe kisha mwili wake kufukiwa chumbani, chini ya uvungu wa kitanda.
Tayari mwili wa marehemu umefukuliwa na Jeshi la Polisi limetangaza kumsaka mtuhumiwa wa mauaji hayo, ambaye alitoweka kusikojulikana baada ya kutekeleza tukio hilo. (cc: azam tv)