15/09/2025
MTIKISIKO WA HIRIZI
SEHEMU YA 3
“N’na maana kuwa Shaka hakutoroka. Aliruhusiwa kuondoka!”
“Aliruhusiwa? Aliruhusiwa na nani?”
“Hilo ni jambo lingine. Lakini mimi binafsi hainiingii akilini kuwa Shaka alitoroka. Atatoroka vipi chini ya ulinzi, akiwa ni mtu mwenye rekodi mbaya sana anayepaswa kuchungwa k**a mtu yeyote anavyoichunga mboni ya jicho lake?”
Inspekta Banda aliguna.
“Unasikia afande,” Kessy aliendelea. “Shaka alihukumiwa jela akiwa ni mtu hatari, jambazi sugu ambaye vyombo vyote vya dola vinamtambua. Pale Keko wanamjua vizuri Shaka. Walimpokea wakiwa wanamjua vizuri. Kwa vyovyote, walipaswa kumchunga vilivyo.”
“Lakini nadhani hujaisahau ripoti ya kutoweka kwake pale gerezani,” Banda alisema. “Shaka aliondoka katika mazingira ya kutatanisha…”
“Kutatanisha vipi afande wakati inasemekana kuwa yule askari aliyekuwa na kundi la wafungwa alibaki ameduwaa tu wakati Shaka akiondoka taratibu?” Kessy alikuwa king’ang’anizi.
“Kwa hiyo unataka kusema kwamba kulikuwa na njama za kumtorosha?”
“Ndivyo picha inavyojionyesha.”
“Ok, lakini hilo silo jambo linalotuhusu kwa sasa,” Banda alisema. “Twende kwanza Magomeni. Ni huko tutakapopata la kufanya.”
Walipofika Magomeni na kuwahoji Mado na Temba wakapata picha ya matumaini. Wakatoka.
“Anaweza kuwa yeye?” Kessy alimuuliza Banda wakati akiondoka hapo kituoni.
“Ndiye,” sauti ya Inspekta Banda ilikuwa kavu. “Niliepuka kusema hivyo mbele ya wale vijana ili kuepusha usumbufu ambao wangetupa. Kwa vyovyote wangetaka kujua watazipataje milioni zao kumi.”
Kicheko kikamtoka Kessy. Akauliza, “ Wana ndoto za milioni kumi kabla hata mtuhumiwa hajapatikana?”
Inspekta Banda hakujibu.
SHAKA alitambua fika kuwa alipaswa kuwa makini dhidi ya askari, hivyo alipoingia ndani ya treni, alikwenda moja kwa moja kwenye behewa la vinywaji na vyakula. Huko aliketi na kuagiza chupa ya maji lita moja. Akatulia kitini akinywa taratibu.
Hadi treni ilipofika kituo cha Saranda hali ilikuwa shwari. Kituoni hapo akashuka na kuagiza kuku na viazi mbatata kisha akarudi behewani. Akiwa na miwani yake mieusi usoni, miwani ambayo hakuwa tayari kuitoa bila ya sababu muhimu, huku kofia ikiwa imeganda kichwani pake, Shaka alianza kukifakamia chakula hicho kwa pupa na baada ya dakika chache tu zoezi hilo likawa limehitimishwa.
Akaingiza mkono mfukoni na kutoa noti zilizokuwamo. Alipozihesabu, akafarijika. Zilikuwa ni pesa za kumtosha kiasi. Kwa kiwango hicho hakuiona sababu ya kumfanya ashindwe kunywa bia mbili, tatu katika kuiliwaza akili yake k**a alivyoamini. Saa moja baadaye koo likawa limeshateremsha bia mbili. Akaongeza ya tatu.
Hadi treni ilipokuwa inaingia Tabora, bia tano zilikuwa zimeshatua tumboni mwake na kuichangamsha akili yake. Naam, kwa kiasi fulani alijihisi kuwa timamu kisaikolojia huku pia akijali kuwa makini katika maongezi na mtu yeyote.
Kwa jumla hakutaka kuzoeana na yeyote kwa kiwango kikubwa, na hilo alilifanya kwa kuwa hakumwamini yeyote kwa kipindi hicho.
Aliendelea kukaa humo katika behewa la vinywaji na maakuli hadi saa 7 usiku. Na wakati huduma ilipositishwa na wateja kutakiwa kuondoka, yeye alimwita mmoja wa wahudumu wa behewa hilo na kunong’ona naye pembeni. Muda mfupi baadaye kijana huyo alikuwa na shilingi 5,000 kibindoni.
“Us’konde mwanangu,” Shaka aliambiwa. “Pumzika humu hadi kunakucha. Na k**a unataka bia unaweza kuendelea kuagiza.”
Alichohitaji Shaka siyo kuendelea kukaa humo ili anywe bia, hapana. Shida yake ilikuwa ni kupata nafasi ya kulaza mbavu hadi kunakucha. K**a angekuwa na pesa za kutakata asingesita kuonana na TT na kumpa nauli ya chumba cha daraja la kwanza. Baada ya hapo angemtafuta ‘mrembo’, kati ya ‘warembo’ wengi wanaozagaa-zagaa ndani ya mabehewa, na ‘mrembo’ huyo angeifanya safari kuwa fupi kuliko ilivyo.
ASUBUHI ya siku iliyofuata treni iliingia Kigoma mjini. Na k**a alivyokuwa makini safarini, hata pale stesheni Shaka hakupachukulia kwa uzito wa kawaida. Alijua fika kuwa askari nchi nzima watakuwa na taarifa kuhusu yeye, hivyo watakuwa wakimsaka k**a gaidi au haini.
Hadhari ikapewa kipaumbele. Akatulia behewani akiwaacha wenye haraka zao wateremke, yeye akawa miongoni mwa wachache wa mwisho. Na alipoteremka alikwenda moja kwa moja kukodi teksi moja kati ya nyingi zilizokuwa zimefurika mbele ya jengo la kituo hicho........
HII SEHEMU YA PILI HAIJAFIKA MWISHO K**A UNAITAJI MWENDELEZO WA SEHEMU HII YA PILI TUTAFUTE :-
1) whatsapp tukuunge kwenye channel ya FULL STORY Bonyeza link hii👉👇
wa.me/qr/XEAQUXEYQNCEB1 TUKUUNGE KWENYE CHANNEL YETU
2) Jiunge na channel yetu ya bure kwa kubonyeza link hii 👉 whatsapp.com/channel/0029VbB2NaAA2pLGdeJDzo29
3) Tufollow kwenye page yetu ya clubzila kwa kubonyeza link hii 👉 clubzila.com/STORY?ref=11084 upate simulizi kali