06/12/2025
ZIJUE SHERIA ZA MPIRA WA MIGUU TFF & ZFF
Leo nimeona nifungue darasa fupi kwa mashabiki wote wa kandanda hapa nchini, ili kila mmoja wetu aelewe kwa undani. Karibuni sana, tuchambue hatua kwa hatua.
1️⃣ Sheria ya Mpira (The Ball)
Mpira unaotumika lazima uwe wa mviringo (spherical), uwe na shinikizo sahihi na ukubwa kulingana na viwango vya FIFA. Mechi rasmi lazima zitumie mpira ulioidhinishwa na TFF au ZFF.
2️⃣ Sheria ya Wachezaji (The Players)
Timu lazima ianze na angalau wachezaji 8 ili mchezo uwe sahihi. Idadi kamili ni wachezaji 11 kwa kila upande (akiwemo kipa). Team zote za Tanzania na Zanzibar kwa ujumla lazima zifuate kanuni hii bila shaka.
3️⃣ Sheria ya Vifaa (Equipment)
Kila mchezaji anatakiwa kuvaa jezi, bukta, soksi, viatu na shin guard. Jezi ya kipa lazima iwe tofauti na wachezaji wengine ili kutambulika haraka.
4️⃣ Sheria ya Mwamuzi (The Referee)
Mwamuzi ndie mwenye mamlaka ya juu zaidi ndani ya uwanja. Maamuzi yake ni ya mwisho. Ndio maana tunasema. Mwamuzi ni kioo cha ligi yetu.
5️⃣ Sheria ya Kuanza & Kuendelea kwa Mchezo
Mechi huanza kwa kupiga mpira kutoka kati kati ya uwanja kwenye michoro na kiduara husika kilichothibitishwa kuwa ni kati kati. Baada ya goli, mpira pia huanzwa tena kutoka kati kati.
6️⃣ Sheria ya Mpira kuwekwa nje ya Uwanja
Mpira ukiwa umevuka mistari yote ya uwanja (iwe hewani au ardhini), unachukuliwa kuwa umetoka, hapo Sheria nyengine zitaamua k**a ni kona or goal kick.
7️⃣ Sheria ya Kufunga Goli
Goli ni halali iwapo tu:
●Mpira umevuka mstari wa goli kikamilifu.
●Hakuna kosa lililotokea kabla ya kufunga hapa namaanisha foul, offside, kuingiliwa na mpira mwengine kutoka nje au kuguswa na referee.
8️⃣ Sheria ya Offside
Mchezaji anakuwa offside iwapo ameweka mwili wake mbele ya beki wa mwisho kabla ya pasi kutolewa. Lakini si offside ikiwa yupo nyuma ya mpira, au anapokea pasi moja kwa moja kutoka kwenye kona, goal kick au throw in.
TUTAENDELEA KESHO KAA TAYARI ASUBUHI SAA 3:00