BMG Media

BMG Media Digital Broadcasting & Marketing

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila Jumatano tarehe 15 Octoba 2025 amekagua miradi ya ujenzi wa madaraja ...
15/10/2025

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila Jumatano tarehe 15 Octoba 2025 amekagua miradi ya ujenzi wa madaraja na barabara Jijini Dar es salaam yenye gharama ya shilingi Bilioni 224.22 inayotekelezwa na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS).

Akizungumza na wananchi waliojitokeza kumlaki Mhe Chalamila amemtaka wakandarasi wa miradi hiyo yote kuhakikisha wanakamilisha miradi hiyo haraka iwezekanavyo kwa muda uliopangwa.

RC Chalamila ameitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na Ujenzi wa Daraja la Jangwani lenye urefu wa mita 390 pamoja na barabara unganishi (0.7km) linalojengwa na Mkandarasi M/s China Communications Construction Company Ltd kwa ufadhili wa Benki ya Dunia chini ya mradi wa uendeshaji wa Bonde la Msimbazi huku Mhandisi Mshauri ni M/s Leporogo Specialist Engineers ya Afrika Kusin iikishirikiana na Afrisa Co nsulting Ltd ya Tanzania na D**g Myeong Engineering Consultants &Architecture Co. Ltd ya Korea Kusini kwa gharama ya shilingi Bilioni 97.

Mhe Chalamila amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kuwalipa wakandarasi ili kukamilisha ujenzi wa miradi hiyo kwa wakati uliopangwa kwa mujibu wa mkataba.

Rc Chalamila amebainisha kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutarahisisha huduma za wananchi kwani watanzania wanasubiri kwa hamu na shauku kubwa miradi hiyo pindi itakapokamilika kwani itakuwa kichocheo cha maendeleo ya mkoa na kuepusha vifo visivyo vya lazima.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukombe kupitia Chama cha Mapinduzi, Dkt. Doto Mashaka Biteko amemshukuru Mwenyekiti wa CCM T...
14/10/2025

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukombe kupitia Chama cha Mapinduzi, Dkt. Doto Mashaka Biteko amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono na maelekezo yaliyowezesha utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa wananchi wilayani, mkoani na Taifa kwa ujumla.

Dkt. Doto Biteko amesema hayo mbele ya Mgombea Urais kupitia CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika mkutano wake wa Kampeni uliofanyika Wilaya ya Bukombe, ikiwa ni sehemu ya Kampeni zake Mkoani Geita Oktoba 12, 2025.

“Mgombea umetufundisha mengi, kupitia kauli mbiu yako ya kazi na utu tunasonga mbele, unatenda zaidi na kusema kidogo. wewe unazungumza matatizo ya watu na maisha yao wakati wote, Utu kwako ni kipaumbele na Kazi kwako ni msingi wa maendeleo” amesema Dkt. Biteko

Ametaja miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ikiwemo Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere, Daraja la JPM, Barabara za lami ndani na nje ya Wilaya ya Bukombe pamoja na taa za barabarani ili kuweka mazingira bora ya ufanyaji wa Biashara.

Dkt. Biteko pia amemshukuru Dkt. Samia na kuahidi kuendelea kuwa msikivu, mwaminifu mwadilifu ikiwa ni sehemu ya uwajibikaji katika nafasi yake ya usaidizi.

Ujenzi wa Daraja la Pangani lenye urefu wa mita 525 na Barabara unganishi na mchepuko zenye urefu wa Kilomita 25 hadi ta...
14/10/2025

Ujenzi wa Daraja la Pangani lenye urefu wa mita 525 na Barabara unganishi na mchepuko zenye urefu wa Kilomita 25 hadi tarehe 30 Septemba 2025 umefikia asilimia 74.3 na kazi ambazo zimefanyika ni pamoja wa Ujenzi wa kuta 2 unganishi za Daraja (Abutments) na nguzo 8 za Kati (Pier) ambapo jumla ya shilingi Bilioni 45.6 zimeshalipwa kwa mkandarasi.

Ujenzi wa daraja hilo ni dhamira kuu ya Serikali kuufungua na kuunganisha Mkoa wa Tanga na ushoroba wa Ukanda wa Pwani ya Afrika Mashariki unaoanzia Malindi – Mombasa – Lunga Lunga/Horohoro - Tanga - Pangani – Bagamoyo (Makurunge) wenye urefu wa kilomita 454.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Tanga Mhandisi Msama Msama wakati alipokagua ujenzi wa mradi huo leo tarehe 14 Octoba 2025 na kuongeza kuwa Daraja hilo likikamilika litakuwa kichocheo cha ukuaji wa uchumi ikiwa ni pamoja na kupunguza muda wa usafiri, urahisishaji wa kufanya biashara na kuwezesha wananchi kuchangamana kwa urahisi, kuwezesha kufikika kwa urahisi kwenye vivutio vya utalii, kuwa kiungo kizuri kati ya bandari za Dar es salaam, Tanga na Mombasa na kuchochea uchumi wa Buluu.

Eng. Msama amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo sehemu ya kwanza ya Tanga – Pangani Kilomita 50 unafadhiliwa kwa asilimia 100 na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Ujenzi na kutekelezwa na TANROADS na Mkandarasi anayetekeleza mradi huo ni CHICO kutoka China umefikia asilimia 75 ya utekelezaji. Sehemu ya pili ya ujenzi wa mradi huo ni Daraja la Pangani na barabara unganishi zenye urefu wa kilomita 25.6 zinajengwa kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kushirikiana na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sehemu ya tatu ni ujenzi wa barabara ya Tungamaa – Mkwaja – Mkange ambayo imefikia asilimia 53 ya ujenzi na ina urefu wa Kilomita 95.2 ambapo itagharimu Shilingi Bilioni 94.538

Halikadhalika, ameeleza kuwa barabara hiyo itawezesha wananchi kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo hususani Mihogo, n**i na mwani na hivyo itarahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji hadi katika masoko mbalimbali ndani na nje ya Mkoa wa Tanga.

Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) inaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa miradi 13 ya dharura kati...
12/10/2025

Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) inaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa miradi 13 ya dharura katika mkoa wa Lindi ambayo itatumia jumla ya shilingi Bilioni 119 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa miradi hiyo ya dharura.

Miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi wa Daraja la Kipwata (Mita 40) na Boksi kalavati eneo la Sakura na Songas, Ujenzi wa Daraja la Mikereng’ende (mita 40) na Boksi kalavati katika maeneo ya Mtandango/ Stakishari na Masaninga, Ujenzi wa Boksi kalavati la Mbwemkuru I (seli 4, 5m x 4m), na matuta ya kuzuia mmomomnyoko wa udongo (Spurdykes), Ujenzi wa Daraja la Somanga Mtama (60m) na Ujenzi wa Daraja la Njenga II (60m) ambapo miradi yote hii ipo katika barabara Kuu ya Marendego – Lindi – Mingoyo.

Miradi mingine ni Ujenzi wa Daraja la Miguruwe (39m) pamoja na Boksi kalavati nne (4), Ujenzi wa Daraja la Zinga (18m) na Ujenzi wa Daraja la Kimambi (39m) ambayo ipo katika Barabara ya Mkoa ya Nangurukuru – Liwale.

Fedha hizo zinaendelea na utekelezaji wa miradi ya Barabara ya Mkoa ya Liwale – Nachingwea ambayo ni Ujenzi wa Daraja la Nangano (20m) na Makalavati ya Dharura ya mawili ya vipimo 2x2, mawili ya vipimo 5x2.5, Ujenzi wa Daraja la Mbwemkuru II (64m). 

Katika Barabara ya Mkoa ya Kiranjeranje- Namichiga serikali inaendelea na Ujenzi wa Daraja la Nakiu (70m) na Ujenzi wa Daraja la Kigombo (25m) na kalavati ya vipimo vya 5x4 huku katika Barabara ya Mkoa ya Tingi – Kipatimo Ujenzi wa Makalavati sita (6) ukiwa unaendelea.

Barabara za Mkoa wa Lindi ziliathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na madhara ya mvua hizo zilizonyesha mfululizo ambapo hata hivyo Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ikatoa fedha jumla ya Shilingi za kitanzania bilioni 19 kwa ajili ya matengenezo ya dharula na kurejesha mawasiliano kwa haraka.

Maonesho ya Keki Kanda ya Ziwa yanatamatika Jumapili Septemba 07, 2025 Handhi Hall jijini Mwanza. Tumia wikendi hii kufi...
06/09/2025

Maonesho ya Keki Kanda ya Ziwa yanatamatika Jumapili Septemba 07, 2025 Handhi Hall jijini Mwanza.

Tumia wikendi hii kufika na kufurahia ladha na bunifu mbalimbali za keki kwa kuonja na kununua kwa punguzo. Hakuna kiingilioni.

Maonesho ya kwanza ya keki Tanzania yanaendelea jijini Mwanza, kuanzia Septemba 03- 07, 2025 katika ukumbi wa Gandhi Hal...
05/09/2025

Maonesho ya kwanza ya keki Tanzania yanaendelea jijini Mwanza, kuanzia Septemba 03- 07, 2025 katika ukumbi wa Gandhi Hall. Njoo uonje na ununue keki kwa punguzo la asilimia 50.

02/09/2025
Mwenge wa Uhuru umezindua Klabu ya Wapinga Rushwa katika Shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza Nyanza (Nyanza English...
25/08/2025

Mwenge wa Uhuru umezindua Klabu ya Wapinga Rushwa katika Shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza Nyanza (Nyanza English Mediaum School) iliyopo Nyamagana mkoani Mwanza. .tz

Address


Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 16:00
Sunday 10:00 - 16:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when BMG Media posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to BMG Media:

  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share