14/08/2023
SIMULIZI MEDIA
MSITU NDANI YA BAHARI
STORY BY ANTHONY
Sehemu ya pili
WHATSAPP: +255754631535
🄹🄸🄽🄸 🅆🄰 🄱🄰🄷🄰🅁🄸
Baada ya pale zaynabu alikuwa akinikataza nimwachie Mamu maji yake,
Aliendelea kunisihi nimrudishie maji yake kwani yeye ameyatoa mbali baharini halafu Mimi naanza kumnyanyasa nayo huku njiani!
Mhhhh nilikasirika maana Mimi sikutaka kabisa Mamu arudi nayo maji yake nyumbani lakini ndo kwanza aling'ang'ania
[email protected]
Tuliendelea na safari yetu ya kurudi nyumbani na tulikuwa tukielekea stand kupanda gaari,
Lakini kiukweli sikuridhishwa na mambo ya Mamu na zaynabu kumuacha Mamu arudi na maji nyumbani, niliendelea kumfanyia fujo nikiwa naipiga Ile chupa idondoke chini Ili niitupe, nilifanya jaribio lakwanza chupa ilidondoka Ile kuinama tu nilipigwa teke mpaka chini,Zay alicheka sana "akasema hayo ndo unataka" niliwafyonya Mamu na Zay,
MCHAKO akasema "[email protected] Emu muache bwana Mamu
Niliitikia sawa, tuliendelea na mambo yetu,
Zay alituonyesha kitu kwenye simu yake, upande wangu niliona wamezubaa na nilizungika upande wa Mamu na kwenda kuitupa Ile chupa,
Niliitoa mikononi make na kuitupa mbali lakini ikadondoka karibu, nilisogea na kuipiga teke pia Mamu aliniwahi kitendo Cha kuipiga teke Ile chuma nae alinisukuma nilienda na chupa mpaka chini na nikawa nimeidondokea,
Ile chupa ilianza kuleta mauzauza maji ndani yake yalionekana kuwa mekundu mithili ya damu,
Wote tulipigwa butwaa wote kuniona Ile Hali,
Mamu aliyawahi maji yake lakini nilimkataza kuichukua alitaka kulazimisha kuichukua lakini nilimzuia, niliichukua Ile chupa na kuitizama Kwa makini niliona maji ni damu tupu, nikatoa mfuniko na kuanza kuyamimina chini lakini Cha Ajabu maji yalitoka meupe kabisa ikiwa kwenye chupa yanaonekana damu,
Tulistaajabu sana Kisha Mamu akadai maji yake NAMI nikampa, alijaribu kumimina kushangaza ikatoka damu!!!!!
Mchako aliyamba Yale maji na kujaribu kumimina Cha Ajabu hayakumwagika kabisa,
Hapo watu tuliokuwa nao njiani walisogea kushangaza kitu kile,
Kuna vijana wawili walitokea wakikimbia walikuwa wakifukuzana walipsmia Yale maji na Yale maji mara yakammwagikia Yale maji na mara mwili mzima alienea Kwa kuloa Yale maji na Cha kushangaza sasa asaaa lionekana kutapakaa damu, mwili mzima halafu alipiga chini huku akigalagala,
Watu waliokusanyika pale walizidi kushangaaa maajabu yaliotokea hapo,
Maji ya damu Yale yalionekana kumsulubu huyu kijana Kwa maana aligalagala Kwa maumivu makali,
Tukiwa Bado tunamtazama hatujui Nini Cha kufanya mara tulishangaaa kijana yule akinyanyuliwa juujuu akielea hewani, alienda k**a umbali wa futi 50 halafu akaganda pale,
Mara ngozi yaka ikaanza kubadilirika Tanga na maumbile yake na kuwa k**a kibabu SI ki Babu sijui kibibi duh alianza kutisha sana hardhat zombi sijui zombi sijui Nini Ile,
*************************
Endelea kufuatilia simulizi za [email protected] pamoja na [email protected]
Gafla alichomoka k**a upepo aliyeyuka k**a Mfano wa mwewe amnyakuavyo kifaraanga Cha kuku mara yuleeeeeeeeeeeeee
KiMbembe tuliobakia hapo chini Kila mmoja alianza kutafuta njia yake ya kukimbilia, mchako hakuweza kujishulisha na kukimbia aliendelea kusimama palepale, nilipotazama upande wa Zay eebwana weee alichomoka k**a vile kiswaswadu kinavyocholopoka mfukoni,Yani na ule ubonge haikuwa kitu kwakwe
Kila upande aliokimbilia Mamu watu walimkataa na kumuogopa maana walijua yeye ni muhusika wa hili jambo,chupa yake ndiyo iliyosababisha maafa kutokea,
Upande wangu nilikuwa Bado sijafanya maamuzi nikimbie ama nifanyaje
Niligeuka upande wanyuma nilimuona mchako amesimama wima akitizama juu mbinguni.
Nilipoendelea kusimama kumtazama vizuri bwana MCHAKO gafla radi ilipiga pande tatu upande wa wale walikokimbilia kushoto kwao na kulia kwao na mbele waendako, ulipiga mwanga mkali mno takribani sekunde 72 na wale walio kimbia wakajikuta wanashindwa kwenda mbele na iliwagharimu kurudi nyuma, walikuja Kwa kukimbia upande wangu na wote waliweza kusimama pale nilipokuwepo, walijazana pale wote na kuona k**a Mimi ndiye mtetezi wao, nilifyatua jicho upande wambele walipotokea kundi hili la watu nilistaajabu Anga limekuwa jekundu pande zote tatu AMBAPO radi ilipiga, nilianza kumtafuta Mamu na Zay Ili tuanze sakata la kujiokoa na janga hili maana ni kifo tu Kwa kwenda mbele, nilimtafuta Mamu nilimuona nikamtafuta Zay huku na huko lakini sikumuona nikamuuliza Mamu, "zayb Yuko wapi? Alitikisa kichwa kuashiria hafahamu, nikamshika mkono mpenzi wangu Mamu na kutaka kutimka nae, lakini kundi nalo lilianza kuniganda na kunifuata niligeuka nyuma Ili kumchukua na MCHAKO nae tukimbie lakini Cha Ajabu MCHAKO sikufanikiwa kumuona bwana MCHAKO nilipiga jicho kule na kule mpaka uko kunako wapi lakini hayupo niliona umati wawatu unaanza kujawa na hofu.
Emu fuatilia kisa hiki soma na toa comments hapo chini
Karibu kujiunga na group letu la simulizi WHATSAPP +255754631535
Sehemu ya kwanza tulipoishia hatukufahamu bwana MCHAKO alifikaje baharini maana yupo Tanga na dar Kwa ule muda alifikajefikaje na hatukupata majibu,
Sehemu ya pili Tumeshangaa kuona haogopi haya mambo na gafla kapotea
Fuatilia uweze kupata vyema kisa hiki.