East Africa TV

  • Home
  • East Africa TV

East Africa TV Official EastAfricaTV page
(873)

Tenga muda ujifunze ufugaji wa sungura – kuanzia kujenga nyumba, kutunza watoto, hadi kulisha ipasavyo.Fursa kubwa ya ki...
20/08/2025

Tenga muda ujifunze ufugaji wa sungura – kuanzia kujenga nyumba, kutunza watoto, hadi kulisha ipasavyo.
Fursa kubwa ya kipato ipo kwenye ufugaji wa sungura

20/08/2025

Tunduma ulio mpakani mwa Tanzania na Zambia imekuwa kero kubwa ambayo mara kadhaa imesababisha mgomo wa madereva kwa kufunga barabara huku mamlaka zikiendelea na jitihada za kumaliza changamoto hiyo.

20/08/2025

Jeshi la polisi Kanda maalumu ya Tarime / Rorya linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kusafirisha dawa zakulevya aina ya bangi na Mirungi ,huku kilo 449 za bangi na nyavu haramu 230 zikichoma moto na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ismail Ali ussi katika Kijiji cha Rabour Wilaya ya Rorya Mkoani Mara.

20/08/2025

Siku chache baada ya EATV Kuripoti taarifa ya wakazi wa kijiji cha Lwamgasa mkoani Geita kuvamia ofisi za TFS na kuchoma moto shamba la miti kwa madai ya kunyanyaswa na kuzuiwa kufanya shughuli za kilimo katika eneo hilo,Serikali kwa kushirikiana na TFS wamewaruhusu wananchi kuendelea na shughuli za kilimo huku taratibu za kutafuta suluhu ya kudumu kati ya wananchi na TFS zikiendelea.

20/08/2025

Kufuatikia kuuawa kwa kijana Wilson Mbise mkazi wa kata ya King’ori Wilayani Arumeru mkoani Arusha wakati akiadhibiwa kwa mujibu wa Taratibu za kimila,vijana wanne walionusurika katika tukio hilo wameiomba Serikali kuchukua hatua za haraka dhidi ya wahusika ikiwa ni Pamoja kudhibiti uwepo wa tamaduni zenye kuhatarisha usalama ndani ya jamii.

20/08/2025

Bei ya machungwa imeanza kupanda mkoani Dar es salaam kutokana na kuanza kumalizika kwa Msimu wa machungwa ambayo mengi yanatoka mkoani Tanga.

Mwezi uliopita kurasa ilizungumza na Wafanyabiashara wa machungwa ambao walisema yatapanda bei na sasa chungwa moja mtaani linaanzia shilingi 150/- mpaka shm250/- kulingana na ubora wake.

20/08/2025

Kutokana na Changamoto ya baadhi ya wazazi na walezi kuwaficha watoto wenye mahitaji maalumu serikali kupitia idara ta elimu msingi imeitaka jamii kuwaibua watoto hao pindi ambapo idara ya elimu msingi itakapopita kuwatambua watoto hao kwaajili ya kuanza shule.

Akizungumza na Kurasa Mary Venansi ambaye ni Afisa Elimu maalumu Msingi manispaa ya Geita amesema watoto wenye mahitaji maalumu wanaobainishwa ni wengi tofauti na wale wanaoandikishwa kuanza shule.

20/08/2025

Wazazi hususani wanawake wametakiwa kuachana na tabia ya kudharau chanjo ya polio ili kuwalinda watoto wao dhidi ya ulemavu wa kudumu.

Wito huo unafuatia tabia iliyokithiri kwa baadhi ya wazazi kutomalizia sindano zote nne za chanjo hiyo huku wataalamu wa afya wakieleza madhara ya kufanya hivyo.

20/08/2025

anasema kuwa siku ya ijumaa Morocco anakufa mapema sana mbele ya Taifa Stars



Address

Mikocheni Light Industrial Area

0255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when East Africa TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to East Africa TV:

Shortcuts

  • Address
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share