Azania Post

Azania Post Online Newswire

JOSE MOURINHO HOI!:TIMU ya Man united chini ya Ole Gunner Solskjaer imeibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Tottenham S...
05/12/2019

JOSE MOURINHO HOI!:
TIMU ya Man united chini ya Ole Gunner Solskjaer imeibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Tottenham Spurs ya Jose Mourinho.

Mechi hiyo imepingwa usiku wa kuamkia Desemba 5, 2019 katika uwanja wa Old Trafford jijini Manchester nchini Uingereza.

Wengi waliamini kuwa Spurs ingeshinda katika mechi hiyo kutokana na mwenendo wa kusuasua wa Man United lakini hali ikawa tofauti na kupelekea kocha mbwatukaji na mwenye vijembe vingi Mourinho kutuliza mzuka wake huo.

Man united ilijiakikishia kupata pointi tatu muhimu kufuatia magoli ya yaliyofungwa na mshambuliaji asiyekuwa na ‘kosistenti’ Marcus Rashford kunako dakika ya 6 ya mchezo kabla ya dakika 48 kufunga la pili kwa mkwaju wa penati.

Dele Alli wa Spurs alifunga goli la kufuatia machozi kunako dakika ya 38.

Msimamo wa ligi baada ya mechi za jana usiku:

SUMAYE ANG'ATUKA CHADEMA:ALIYEKUWA mwenyekiti wa Chadema kanda ya Pwani, Frederick Sumaye amejiondoa katika chama hichoS...
04/12/2019

SUMAYE ANG'ATUKA CHADEMA:
ALIYEKUWA mwenyekiti wa Chadema kanda ya Pwani, Frederick Sumaye amejiondoa katika chama hicho

Sumaye ambaye pia ni waziri mkuu mstaafu ametangaza uamuzi wake huo leo Desemba 4, 2019 jijini Dar es Salaam na kwamba uamuzi wake umetokana na fitna(Figisu) alizofanyiwa baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa chama cha Chadema taifa.

‘‘Baada ya kutafakari kwa kina, ustaarabu unasema toka sasa hutakiwi, wako watakaosikitika nimelazimika kujiondoa CHADEMA kutoka leo hii, mimi sio Mwanachama wa CHADEMA na sijiungi na chama chochote, ila niko tayari kutumika na chama chochote kwa ushauri," amesema Sumaye

Ameeleza kuwa alitaka kugombea nafasi ya Uenyekiti ili kuondoa dhana iliyopo miongoni mwa watu kuwa nafasi ya Mwenyekiti ndani ya CHADEMA ni ya Freeman Mbowe na haiguswi.

Pia ametaja sababu za kusitisha nia ya kugombea Uenyekiti wa Chama Taifa. 'Nasitisha rasmi safari hiyo kwa usalama wangu, usalama wa wanachama na chama chenyewe, maana Mwenyekiti Mbowe ameshasema sumu haionjwi kwa ulimi na mimi sitaki kuionja kwa sumu hiyo'’.

UMEME VIJIJINI KULIPIWA KWA KUDUNDULIZA:WANANCHI wa maeneo ya vijijini ambao hawana uwezo wa kulipia shilingi elfu 27 kw...
04/12/2019

UMEME VIJIJINI KULIPIWA KWA KUDUNDULIZA:
WANANCHI wa maeneo ya vijijini ambao hawana uwezo wa kulipia shilingi elfu 27 kwa mkupuo za kuunganishiwa umeme sasa wanaweza kulipia huduma hiyo kwa kudunduliza kidogo kidogo.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani Desemba 3, 2019 kijijini Mnekezi, wilayani Chato mkoani Geita alipokuwa akizungumza na wananchi kabla ya kuwasha rasmi umeme kijijini hapo.

Alikuwa akitoa maelekezo kwa wataalamu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwamba, wahakikishe wananchi wote wanaunganishiwa umeme bila kubagua hali zao kiuchumi k**a ilivyo azma ya serikali.

Alisema pamoja na serikali kupunguza gharama za kuunganisha umeme vijijini hadi shilingi elfu 27 tu lakini bado wako wananchi ambao kipato chao hakiwezi kuwaruhusu kulipa pesa hiyo kwa mkupuo, hivyo akawataka watendaji hao kupokea malipo ya wananchi husika kwa mtindo wa kudunduliza.

“Akipata elfu 10 akaleta, pokea umwandike; kesho akileta nyingine elfu tano pokea hadi pale atakapotimiza kiwango kinachotakiwa cha elfu 27” alisema

Katika hatua nyingine, Waziri alitoa hamasa kwa wananchi wa kijiji hicho na vingine vyote nchini ambako miradi mbalimbali ya umeme inatekelezwa, kutochagua kazi.

Alitoa hamasa hiyo baada ya kutoa maagizo kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini nchi nzima, kuhakikisha wanaajiri vibarua kutoka maeneo husika ili kuharakisha kazi lakini pia kuinua kipato cha wananchi, hususan vijana wa maeneo hayo.

Aidha, aliwataka wananchi kuachana na kasumba ya kulalamika kuwa hawajaunganishiwa umeme wakati hawajalipia huduma husika kwa visingizio tofauti, ikiwemo madai ya ukosefu wa nguzo.

“Wananchi, suala hili narudia tena kulisemea; ninyi mnachotakiwa kufanya ili muunganishiwe umeme ni kulipia tu na kuandaa nyumba zenu kwa kuweka mfumo wa nyaya. Suala la nguzo na vifaa vingine haliwahusu. Lipieni ili mletewe umeme,” alisisitiza.

Waziri Kalemani, ambaye pia ni Mbunge wa eneo husika (Chato), aligawa kwa wananchi wa Mnekezi, vifaa 50 vya Umeme Tayari (UMETA) bure, mbali na vile 250 ambavyo kila mkandarasi wa miradi ya umeme vijijini hutakiwa kugawa katika eneo lake.

PICHANI: Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (katikati-mwenye kipaza sauti), akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mnekezi, wilayani Chato, Mkoa wa Geita, kabla ya kuwasha rasmi umeme kijijini hapo, Desemba 3, 2019. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Charles Kabeho.

NI LIONEL MESSI TENA:MUARGENTINA Lionel Messi amefanikiwa kunyakuwa tuzo ya Ballon d’Or 2019.Tuzo hiyo imetolewa usiku w...
03/12/2019

NI LIONEL MESSI TENA:
MUARGENTINA Lionel Messi amefanikiwa kunyakuwa tuzo ya Ballon d’Or 2019.

Tuzo hiyo imetolewa usiku wa kuamkia Desemba 3, 2019 nchini Ufaransa katika jiji la Paris baada ya kuwashinda beki wa Liverpool Van Dijk aliyeshika nafasi ya pili huku nafasi ya tatu ikishikwa na Christiano Ronaldo wa Juventus.

Messi anayechezea FC Barcelon, hiyo inakuwa ni tuzo yake ya sita ya Ballon d’Or akimzidi mpinzani wake wa muda wote Cristiano Ronaldo aliyetwaa tuzo hiyo mara tano.

Wengine waliofanikiwa kushinda tuzo katika usiku wa Ballon d’Or 2019 ni beki wa Juventus Matthijs De Light tuzo ya mchezaji bora kijana (Kopa Trophy) kwa kuwashinda Jadon na Joao.

Golikipa wa Liverpool Alisson Becker akiwa ndio mshindi wa tuzo ya kipa bora wa mwaka na Megan Rapinoe wa timu ya taifa ya wanawake ndio akashinda tuzo ya mchezaji bora wa k**e (Ballon d’Or)

29/11/2019

Msimamo wa ACT Wazalendo kuhusu vifurushi vipya vya Bima ya Afya nchini vinavyotolewa kupitia NHIF

YUROPA LIGI:MAN UNITED, ARSENAL HOIUSIKU wa kuamkia Novemba 29,2019 zimechezwa mechi 12 za UEFA Yuropa ligi, huku Man Un...
29/11/2019

YUROPA LIGI:MAN UNITED, ARSENAL HOI
USIKU wa kuamkia Novemba 29,2019 zimechezwa mechi 12 za UEFA Yuropa ligi, huku Man United na Arsenal za Uingereza zikifungwa.

Hata hivyo pamoja na kichapo , Man United imefuzu kendelea na hatua inayofuata huku Arsenal ikisumbilia mechi zinazofuata

Arsenal ilikuwa nyumbani katika uwanja wake wa Emirates kuikaribisha Frankfurt ya Ujerumani wakati Man United ilikuwa ugenini kuikabili Astana ya Kazakhstan.

Arsenal akiwa nyumbani alipokea kipigo cha magoli 2-1, magoli yakifungwa na Kamada dakika ya 55 na 64 huku goli la kufuta machozi la Arsenal lilifungwa na Pierre Aubameyang dakika ya 45.

Pia Man United walipoteza kwa kufungwa 2-1 magoli ya Astana yakifungwa na Shomko dakika ya 55 na Benard akijifunga dakika ya 62, Jesse Lingard ndio alifunga goli la mapema kwa Man United dakika ya 10.

Huo ndio unakuwa mchezo wa kwanza kwa Astana kupata ushindi katika mashindano hayo kwani ilikuwa imepoteza michezo yote minne ya mwanzo.

Matokeo kamili haya hapa:

28/11/2019

HUYU KUKU BHANA!!!

UEFA LIGI:MAN CITY, JUVE, SPURS, MADRID, PSG ZAFUZURAUNDI ya tano ya michuano ya UEFA Championi Ligi hatua ya makundi us...
27/11/2019

UEFA LIGI:MAN CITY, JUVE, SPURS, MADRID, PSG ZAFUZU
RAUNDI ya tano ya michuano ya UEFA Championi Ligi hatua ya makundi usiku wa kuamkia Novemba 27, 2019 imeendelea tena kwa michezo kadhaa kuchezwa huku timu nne zikifanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo

Tottenham Hotspurs chini ya Jose Mourihno inafuzu kwa kujihakikishia kumaliza nafasi ya pili nyuma ya FC Bayern Munich anayeongoza Kundi kwa point, 15.

Hapo jana usiku Spurs ya Mourinho ilifanya maajabu baada ya kusawazisha na kutoka kufungwa goli 2-0 na kupata ushindi wa 4-2 dhidi ya Olympiacos.

Real Madrid na PSG nazo zimefunzu baada ya kutoka sare ya 2-2 , Real Madrid wakiwa nafasi ya pili kwa point 8 huku PSG akiongoza kwa point 13.

Ushindi wa 1-0 wa Juventus dhidi ya Atletico Madrid unaipeleka Juventus hatua inayofuata na licha ya Atletico kuwa nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 7 atalazimika kusubiri hadi mchezo wake wa mwisho ili kujua hatma yake kwani FC Bayer Leverkusen aliyepo nafasi ya 3 ana pointi 6 hivyo bado ana nafasi nae.

Sare ya 1-1 nyumbani inamvusha Man City dhidi ya Shakhtar na Shakhtar kubaki na sintofahamu kwa kutakiwa kusubiri hadi mchezo wa mwisho ndio wajue hatma yao

Address


Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Azania Post posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Azania Post:

Shortcuts

  • Address
  • Telephone
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share