
14/07/2025
Mwenyekiti na Mwanzilishi wa , Bi Asma Ali Hassan Mwinyi (), amekabidhi sanda kwa ajili ya maiti wasio na ndugu katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupitia Taasisi ya JAI – taasisi inayohudumia na kuzika maiti zisizo na ndugu au waliotelekezwa.
Kupitia mchango huu, AMF inaendeleza dhamira yake ya kuhudumia watu wote – hata wale waliotangulia mbele ya haki pasipo kuwa na wa kuwazika. Bi Asma ametoa wito kwa Watanzania wote kuchangia kwa uwezo wao, kwani kumstiri mwenzako ni ibada yenye thawabu kubwa.