Swahili Times

  • Home
  • Swahili Times

Swahili Times Habari bila mipaka, saa 24.
(448)

15/08/2025

  Ijumaa Agosti 15, 2025
15/08/2025



Ijumaa Agosti 15, 2025

14/08/2025

Mgombea Urais wa Tanzania kupitia chama cha Alliance For Democratic Change (ADC), Wilson Mulumbe amesema akishinda Urais wa Tanzania atahakikisha kila mzazi aliyetelekezwa anapewa mafao la kulea hadi mtoto atakapotimiza umri wa miaka 18.

AD: Mixx by Yas imezindua rasmi kampeni ya Kila Hatua Mixx yenye lengo la kuchochea ujumuishwaji wa kifedha kwa Watanzan...
14/08/2025

AD: Mixx by Yas imezindua rasmi kampeni ya Kila Hatua Mixx yenye lengo la kuchochea ujumuishwaji wa kifedha kwa Watanzania wote pamoja na kuongeza upatikanaji wa huduma za mikopo, akiba, bima, na uwekezaji hususan kwa vijana na wanawake.

Kampeni hiyo imezinduliwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx by Yas, Bi. Angelica Pesha pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Yas, Bw. Pierre Canton Bacara, katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Katika hotuba yake, Bi. Pesha amesema Mixx by Yas imewawezesha wateja zaidi ya milioni 20 kufanya miamala ya zaidi ya TZS trilioni 6 kila mwezi, kutoa ajira zisizo za moja kwa moja kwa mawakala 200,000 nchi nzima, na kusaidia wafanyabiashara zaidi ya 500,000 kupokea malipo ya bidhaa na huduma za kidigitali.

  FT: Morocco 3-1 Zambia
14/08/2025



FT: Morocco 3-1 Zambia

Klabu ya Yanga imesema mchango wa TZS milioni 100 kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) ulitolewa na taasisi ya GSM chini ya mdh...
14/08/2025

Klabu ya Yanga imesema mchango wa TZS milioni 100 kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) ulitolewa na taasisi ya GSM chini ya mdhamini na mfadhili wa klabu, Ghalib Mohamed, na siyo kupitia pesa za wanachama au kutoka kwenye mfuko wa klabu.

Aidha, uongozi wa Yanga umewaomba radhi wanachama, mashabiki na wapenzi wa mpira wa miguu kwa usumbufu wowote uliojitokeza kupitia sintofahamu hiyo.

Rais Samia Suluhu Hassan ameielekeza Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na vyombo vya Usalama kupeleka misaada ya haraka na kuo...
14/08/2025

Rais Samia Suluhu Hassan ameielekeza Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na vyombo vya Usalama kupeleka misaada ya haraka na kuongeza jitihada za uokoaji kufuatia maafa yaliyotokea katika mgodi wa Nyandolwa, Kata ya Mwenge Wilaya ya Shinyanga Vijijini.

Ajali hiyo imetokea Agosti 11, 2025 baada ya ardhi kutitia wakati wafanyakazi na mafundi wakifanya ukarabati wa mashimo matatu katika eneo hilo ambapo takriban watu 25 walifunikwa ardhini huku wanne kati yao wakiokolewa.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mohamed Mhita, shimo la kwanza lilikuwa na mafundi 11, la pili lilikuwa na mafundi 8, na shimo la tatu lilikuwa na mafundi 6 ambao wanne kati ya mafundi 6 waliweza kuokolewa na mmoja kufariki baadaye.

Rais Samia Suluhu Hassan akipewa Tuzo ya Heshima ya Uanachama wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani na Makamu wa Rais ...
14/08/2025

Rais Samia Suluhu Hassan akipewa Tuzo ya Heshima ya Uanachama wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani na Makamu wa Rais wa CISM Kanda ya Afrika, Meja Jenerali Maikano Abdullahi kutoka Nigeria, kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.

"Mimi nimehamia hiki chama cha ACT-WAZALENDO kwa dhati, na kwa watu niliowakuta tutalisaidia taifa, na sitegemei kuhama ...
14/08/2025

"Mimi nimehamia hiki chama cha ACT-WAZALENDO kwa dhati, na kwa watu niliowakuta tutalisaidia taifa, na sitegemei kuhama leo wala kesho." - Mgombea Urais wa Tanzania, Luhaga Mpina akizungumza na vyombo vya Habari

14/08/2025

Mgombea wa Urais kupitia ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina amesema alianza maandalizi ya kuondoka Chama cha Mapinduzi (CCM) muda mrefu baada ya kuona hakuna maelewano.

"Uzoefu [wa kiuongozi] unanipa uwezo wa kumudu majukumu yote ambayo ninayaomba, hata hii nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Mu...
14/08/2025

"Uzoefu [wa kiuongozi] unanipa uwezo wa kumudu majukumu yote ambayo ninayaomba, hata hii nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naimudu na kupitiliza." - Mgombea Urais kupitia ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina akizungumza na vyombo vya habari

Address


Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Swahili Times posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Swahili Times:

Shortcuts

  • Address
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share