Michuzi TV

Michuzi TV Karibu Michuzi Blog a.k.a Globu ya Jamii the most read Swahili blog on Earth

http://issamichuzi.blo

When I started this blog at Finlandia Hall in Helsinki, Finland, on Septermber 28, 2005, my aim was to bridge the news and information gap for the benefit of Tanzanians in the Diaspora. Since I was the first Tanzanian blogger operating from Tanzania ( http://issamichuzi.blogspot.com/2005_09_01_archive.html) about 4 years elapsed before others started blogging. Therefore I boast of millions of fait

hful old and new followers who have made Michuzi the most read Swahili blog on earth. Moreso its the top most blog with authoritative and authentic content.

 Klabu ya Yanga imempongeza mchezaji wake (Kolipika Msheri) kwa kufunga ndoa Leo huko Kigamboni jijini Dar es salaam 👇👇👇...
25/02/2025



Klabu ya Yanga imempongeza mchezaji wake (Kolipika Msheri) kwa kufunga ndoa Leo huko Kigamboni jijini Dar es salaam 👇👇👇


——
Hongera sana Golilkipa wetu kwa Kufunga Ndoa siku ya leo, Tunakutakia kila la Heri🤩🤩.

 NAIBU Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Tanzania Bara (UVCCM), M***a Mwakitinya amesema ushindi kwa...
25/02/2025



NAIBU Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Tanzania Bara (UVCCM), M***a Mwakitinya amesema ushindi kwa Chama cha Mapinduzi sio ombi bali ni lazima kutokana na kazi kubwa zilizofanyika chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambazo zinauzika kwa wananchi.

Amesema kuwa lengo la Chama hicho kuendelea kushika dola sio kwenda kucheza rede bali ni kuendelea kutatua shida na changamoto za wananchi.

Mjumbe huyo wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (Nec) alitoa kauli hiyo jana wakati wa uzinduzi wa kambi ya Vijana wa ccm mkoa wa Kilimanjaro wapatao zaidi ya 700 inayofanyika wilayani Hai.

Alisema kuwa, hakuna Chama cha siasa kinachoweza kutatua matatizo ya Wananchi katika Taifa hili zaidi ya Chama cha Mapinduzi na kuwataka wananchi kutodanganyika na watu wenye nia hovu na Taifa.

"Vijana mnapaswa kutambua kuwa CCM sio Chama ambacho kinatafuta dola ili kwenda kucheza rede bali ni kuendelea kutatua matatizo ya wananchi na ndio maana mmeshuhudia fedha nyingi zimetolewa na serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo" Alisema Mwakitinya.

Aliwataka Vijana kusimamia maadili na kuchunga njia zao k**a vijana wa CCM ili kuendelea kuwavutia vijana walio nje ya Chama kujiunga na Chama hicho.

Alisema kuwa, CCM kinamisingi ya Umoja na mshik**ano na kuwataka kutokuruhusu kutengana kwani itaruhusu kuingiliwa na maadui na kuruhusu Chama kushindwa katika chaguzi mbalimbali.

Akitoa taarifa ya kambi hiyo, Katibu wa UVCCM mkoa Kilimanjaro, Ahmady Kibamba alisema kuwa, vijana wameamua kujinoa, kujiivisha na kujiimarisha ili kuweza kuhakikisha CCM inapata ushindi wa kishindo katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan leo Februari 25, 2025 ameweka jiwe la msingi la ujenzi ...
25/02/2025



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan leo Februari 25, 2025 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji wa miji 28 utaohudumia miji ya Handeni,Korogwe, Muheza na Pangani.

Aidha mheshimiwa Rais amesema “Wizara ya Maji mmetoka kuwa Wizara ya Lawama na kuwa Wizara ya Mfano, nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya”

Mwaka 2021 tulikuwa tunasukumana sana, lakini tangu mwaka 2022 Sekta ya Maji mmekuwa mnafanya vizuri. Kazi yangu ni kutafuta fedha, nyie kazi yenu uteklezaji Nawapongeza watumishi wote wa Sekta ya Maji, endeleeni kuchapa kazi. amesema Rais Samia.

Amesema amefanya kazi kubwa ya kutafuta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi na amekuwa akitiwa moto na wizara kutokana na usimamizi mzuri ambao umewezesha mafanikio makubwa katika usimamizi na utekelezaji wa miradi.

Awali akizungumza mbele ya Rais, Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso (Mb) amesema Wizara ya Maji imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na ushirikiano wanaoupata kutoka kwa Rais Samia. Amesema miradi mingi ya maji imeweza kutekelezwa kwa wakati kutokana na utayari wa Rais Samia kuruhusu fedha ya utekelezaji wa miradi hiyo

Rais samia yuko katika ziara ya kikazi mkoani Tanga.

 Akizungumza  wakati akiiwakilisha Nchi ya Tanzania katika Kikao cha 58 Cha Haki za Binadamu kinachofanyika Geneva Nchin...
25/02/2025



Akizungumza  wakati akiiwakilisha Nchi ya Tanzania katika Kikao cha 58 Cha Haki za Binadamu kinachofanyika Geneva Nchini Uswisi Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Dr. Damas Ndumbaro (Mb) amesema kuwa,   Nchi ya Tanzania imeendelea kuweka kipaumbele katika uendelezaji na ulinzi wa Haki za Binadamu katika utekelezaji wa shughuli za Serikali.

Waziri Ndumbaro amesema  kupitia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,1977 na Katiba ya Zanzibar, 1984, Tanzania  imeendelea kusimamia Utu wa Kibinadamu kwa mujibu wa  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 na Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu na inaendana na mkakati uliopitishwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan ambao umejikita katika 4Rs kuwa ni Maridhiano, Uthabiti,Mageuzi na Kujenga upya.

Akiwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa Haki za Binadamu katika Hifadhi ya Ngorongoro, Waziri Ndumbaro amesema kuwa Serika ya Tanzania imeendelea kuweka uwiano sawa wa  Haki za Binadamu na Maisha kwa kuzingatia uhifadhi.

Waziri Ndumbaro amefafanua kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kusimami Haki za Binadamu Ngorongoro alikutana na Viongozi wa Vijiji na Kimila na kusikiliza kero zao na kuanzisha Tumbe mbili za Ushauri, kushauri masuala ya Ardhi na kushauri kuhusu Mpango unaoendelea wa kuwahamisha wakazi wa Ngorongoro kwenda Msomera.

Aidha, Waziri Ndumbaro ameongezea lengo la jitihada hizo ni kuhakikisha zoezi la hiari linafanya kazi kwa urahisi na kwamba kero za Wananchi zinashughulikiwa

Maeneo mengine ya usimamizi wa Haki za Binadamu yaliyowasilishwa katika Mkutano huo ni pamoja na kufanya Uchaguzi Huru na Haki kila baada ya miaka mitano,Uhuru wa Vyombo vya Habari na kujieleza,kulinda Haki za makundi hatarishi ukiwemo ustawi wa Watu Wenye Ualbino na Usaidizi kwa Watu wenye Ulemavu.

 KATIBU Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo amewataka watumishi wa Tume kufanya kazi kwa kujituma na we...
25/02/2025



KATIBU Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo amewataka watumishi wa Tume kufanya kazi kwa kujituma na weledi hasa kwenye usimamizi wa shughuli za uchimbaji, uchenjuaji na biashara ya madini ili Sekta ya Madini iendelee kuwa na mchango mkubwa kwenye Pato la Taifa.

Mhandisi Lwamo ametoa rai hiyo mapema leo Februari 25,2025 jijini Dodoma akifungua mafunzo ya matumizi ya mashine maalum za kupima madini ya metali kwa njia ya Mionzi /X-RAY kwa watalam wa Tume ya Madini wakiwemo Wahandisi Migodi, Wahasibu, Watakwimu, Maafisa Utawala na Wataalam wa Maabara ‘Lab Technologist.

Amesema kuwa, tangu kuanzishwa kwa Tume ya Madini rekodi ya makusanyo ya maduhuli ya Serikali imeendelea kukua hali iliyopelekea wadau wengi wa madini na wananchi kwa ujumla kuwa na taswira chanya ya Tume.

“Mwaka wa fedha uliopita 2023/2024 tulimaliza kwa kukusanya Shilingi Bilioni 753, mwaka huu tunatakiwa kukusanya Shilingi Trilioni Moja, sote tunapaswa kuwa na weledi ili tuweze kufikia lengo, hatuwezi kufika bila uadilifu, kujituma na kutunza vitendea kazi,”amesema Mhandisi Lwamo.

Katika hatua nyingine, Mhandisi Lwamo amesema kuwa Serikali kupitia Tume ya Madini itaendelea kuboresha mazingira ya utendaji kazi kwa Ofisi za Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa, Masoko ya Madini, Vituo vya Ununuzi wa Madini na Maabara ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa vitendea kazi vya kutosha na kutatua changamoto zinazowakabili wachimbaji wa madini nchini.

Awali akizungumza, Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini, Venance Kasiki amesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha watumishi wanajengewa uwezo wa matumizi sahihi ya mashine za kupima madini ya metali ambazo kwa kiasi kikubwa zimesaidia sana kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali.

 Marais wa zamani wa Kenya na Nigeria, pamoja na Waziri Mkuu wa zamani wa Ethiopia wameteuliwa na Jumuiya ya Afrika Mash...
25/02/2025



Marais wa zamani wa Kenya na Nigeria, pamoja na Waziri Mkuu wa zamani wa Ethiopia wameteuliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Mataifa ya Kusini mwa Afrika (SADC), kuongoza mchakato wa amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Kupitia taarifa iliyotolewa na Rais wa Kenya William Ruto ambaye pia ni Mwenyekiti wa EAC alisema walifikia uamuzi wa pamoja kwamba Uhuru Kenyatta wa Kenya, Olusegun Obasanjo wa Nigeria na Hailemariam Desalegn wa Ethiopia wataongoza mikakati ya EAC na SADC ya kupata amani Mashariki mwa Congo.

Makubaliano ya uteuzi huo yalifanyika katika Mkutano wa Pamoja wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa EAC na SADC uliofanyika Dar es Salaam tarehe 8 Februari 2025, ukiongozwa na Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe na Rais Ruto wa Kenya, kujadili hali ya usalama nchini DRC.

Haya yanajiri baada ya Rais wa Angola João Lourenço kutangazwa kuwa majukumu aliyonayo yatamzuia kuendelea kuwa mpatanishi wa mzozo wa DRC unaoendelea.

Kikundi Kazi cha EAC kilifanya majadiliano kuhusu hali ya usalama, na kutoa mapendekezo muhimu, ikiwa ni pamoja na kusitisha mapigano mara moja na kutoa msaada wa kibinadamu.

M23 na wahusika wote wanahimizwa kusitisha mapigano na kutii mapatano ya amani yaliyotangazwa.

Serikali ya DRC na waasi wa M23 wamelaumiana kwa kukiuka makubaliano ya Luanda, ambayo yaliwania kurejesha amani Congo na badala yake migogoro imeshuhudiwa kwa zaidi ya miaka 30.

 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda amesema ujio wa Watafiti wa Mimea Vamizi kutoka nchini Cuba waliokuja nchini watasai...
25/02/2025



Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda amesema ujio wa Watafiti wa Mimea Vamizi kutoka nchini Cuba waliokuja nchini watasaidia katika kukabili Mimea Vamizi katika Hifadhi ya Taifa Saanane pamoja na Ziwa Viktoria ambayo yamekuwa changamoto katika Shughuli za usafirishaji, Uvuvi na Utalii.

RC Mtanda amebainisha hayo mara baada ya kuipokea timu ya Watafiti wa Mimea vamizi kutoka Jamhuri ya Cuba walioungana na Wataalamu wa Ikolojia kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii ambao wametembelea mwambao wa Ziwa Viktoria eneo la Kigongo Busisi pamoja na Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saa Nane ambapo amesema ujio wa wao utaleta suluhu ya tatizo la Magugu ya maji katika Ziwa hilo kubwa na katika Hifadhi hiyo ya kipekee Duniania.

"Tumefurahi kupata huu ugeni wa Watafiti wa Mimea Vamizi kutoka Cuba, ambao wameandaliwa kuja na Wizara ya Mambo ya Nje kupitia Balozi wetu wa Tanzania Mhe. Balozi. Humphrey Polepole na Wizara ya Maliasili na Utalii kwani wamekuja wakati muafaka kwakuwa hivi karibuni kuna gugu vamizi linazaa mara kwa mara na kwa muda mfupi ziwa limekuwa linafunikwa kwahiyo huathiri miundombinu ya usafirishaji na samaki wa Vizimba"- Alieleza Mkuu wa Mkoa Mtanda

Aidha ameeleza kuwa Magugu vamizi yanaweza kuleta athari kwa wafugaji wa Samaki kwa njia ya vizimba hivyo serikali imeleta wataalamu hao katika muda muafaka.

“Sasa hivi Ziwa Viktoria tunafuga samaki kwa vizimba na kuna vizimba takribani 1047, kwahiyo endapo gugu vamizi litaendelea kusambaa katika maeneo mengine litaleta athari kiuchumi, kwa vijana wafugaji ndio maana tunaishukuru serikali kwa kuwaleta Wataalamu haraka kabla hawajaathirika”-aliongeza Mhe. Mtanda.

Afisa Mistu Mkuu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mwenyekiti ziara ya timu ya watafiti mimea vamizi kutoka Jamhuri ya Cuba na Tanzania Bw. Emmanuel Msofe amasema sekta mbalimbali zimeathiriwa na Mimea Vamizi hususani katika maeneo yaliyohifadhiwa kisheria hivyo ziara ya Watafiti hao inatarajiwa kuleta neema katika Mkoa wa Mwanza na Tanzania kwa ujumla.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Jumanne, Februari 25, 2025, anaendele...
25/02/2025



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Jumanne, Februari 25, 2025, anaendelea na ziara yake mkoani Tanga, ambapo atatembelea miradi muhimu ya maendeleo kwa wananchi wa mkoa huo ikiwemo na kuiwekea mawe ya msingi na kuizindua kwa ile ambayo ujenzi wake umekamilika.

Katika ratiba ya leo, Rais Samia atazindua Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Tanga na kuzungumza na wananchi wa Wilaya ya Kilindi.

Aidha, atafungua jengo jipya la Halmashauri ya Mji wa Handeni na kusalimiana na wakazi wa eneo hilo.

Pia, ataweka jiwe la msingi kwa Mradi wa Maji wa Miji 28, unaolenga kuboresha huduma za maji safi kwa wakazi wa miji mbalimbali nchini.

Ziara ya Rais Samia imekuwa na mafanikio makubwa, ambapo jana Februari 24, 2025 alitembelea wilaya za Korogwe na Lushoto, akizindua miradi na kuzungumza na wananchi.

 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Deus  Sangu ameonesha kuumizwa na mwitikio mdogo wa elimu...
25/02/2025



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Deus Sangu ameonesha kuumizwa na mwitikio mdogo wa elimu Mkoani Rukwa huku akiwaonya wazazi wenye tabia ya kuwaelekeza watoto wao kujikosesha au kuchora picha katika mitihani yao kwa lengo la kujihusisha na shughuli za kilimo na ufugaji.

Sangu ambaye pia ni Mbunge wa Kwela ametoa kauli hiyo wakati alipotembelea na kuzungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Miangalua iliyopo katika wilaya ya Sumbawanga, Mkoani Rukwa.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya uwekezaji mkubwa wa miundombinu ya elimu huku akitaja ujenzi Shule za Sekondari kila Kata pamoja na Shule ya Wasichana ya Rukwa, lengo ni kuhakikisha hakuna mtoto anayeachwa nyuma.

Hata hivyo, Sangu amesema kutokana na msukumo mdogo kutoka kwa wazazi, watoto walio wengi wamekuwa wakiishia darasa la saba na wale wanaoendelea na Sekondari wamekuwa hawafanyi vizuri kwenye mitihani yao ya mwisho.

Kufuatia hali hiyo, Sangu amesema Mkoa huo umekuwa kinara kwa idadi kubwa ya watoto wa k**e kukatishwa masomo kutokana na kupata mimba, utapiamlo pamoja na tabia ya utapeli.

Amesisitiza kuwa elimu ndio injini ya maendeleo ya familia yoyote na kutoa angalizo kwa wazazi kuwa yoyote anayecheza na elimu ya mtoto wake atabaki kuwa nyuma huku fursa za kiuchumi za Mkoa huo zikiendelea kuporwa na wananchi wa Mikoa mingine.

" Mkoa wa Rukwa umejaaliwa rasilimali za kila aina ikiwemo madini pamoja kuwa ya pili kwa kuzalisha chakula lakini hali zetu ni duni kutokana na kukosekana kwa elimu" amesisitiza Mhe.Sangu

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Miangalua, Didas Kayanda amesema jamii yoyote iliyostarabika ni lazima ikumbatie elimu, hivyo amewataka waumini hao kuwa mstari wa mbele kuwahimiza watoto wao juu ya umuhimu wa elimu.

 Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa ameongoza waombolezaji kwenye kisomo cha Alhaj Omary Mchengerwa, baba mzazi wa Waziri w...
25/02/2025



Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa ameongoza waombolezaji kwenye kisomo cha Alhaj Omary Mchengerwa, baba mzazi wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa aliyefariki dunia alfajiri ya Jumatatu, Februari 24 katika mji wa Madina nchini Saudi Arabia baada ya kumaliza Ibada ya Umrah kwa siku 10 Makkah na Madina.

Hafla hii imefanyika nyumbani kwa Mhe Mchengerwa Masaki jijini Dar es salaam jana, ikifuatiwa na kisomo kingine nyumbani kwa marehemu Yombo. Dua ingine inafanyika Rufiji, nyumbani kwa ukoo wa Mchengerwa.

 Mahak**a ya Uganda imepuuzilia mbali ombi la kutaka kuachiliwa kwa mpinzani wa Uganda, Dkt. Kizza Besigye, na mwenzake,...
24/02/2025



Mahak**a ya Uganda imepuuzilia mbali ombi la kutaka kuachiliwa kwa mpinzani wa Uganda, Dkt. Kizza Besigye, na mwenzake, Hajji Obeid Lutale, ikisema kuwa ombi hilo limepitwa na wakati na hivyo halina mashiko.

Uamuzi huo ulitolewa Jumatatu na jaji ambaye alisema kuwa kuzuiliwa kwao bila kufuata sheria hakutajwi, kwani wawili hao walifikishwa mbele ya mahak**a ya kiraia wiki iliyopita, kusomewa mashtaka yao rasmi, na kufungwa katika gereza la jiji kuu la Kampala.

Uamuzi huu unafuatia uamuzi wa mwezi jana wa Mahak**a ya Kuu ya Uganda, ambao ulizuia jopo la kijeshi kusikiliza kesi za kiraia.

Hata hivyo, mawakili wa Besigye walikata rufaa kwa ombi la kuachiliwa huru, wakishinikiza serikali kumuachilia mteja wao pamoja na mshukiwa mwenza.

Wakati huohuo, wabunge wa chama tawala cha National Resistance Movement (NRM) walipitisha pendekezo la kulenga kubadili sheria ili mahak**a ya kijeshi iwe na uwezo wa kusikiliza kesi za raia wanaoshukiwa na hatia ya kumiliki silaha.

Haya yanajiri baada ya wanaharakati wa haki za binadamu kutoka Uganda na Kenya kuandamana leo kutaka serikali ya Uganda imuachilie huru Dkt. Kizza Besigye, ambaye hali yake ya kiafya inaripotiwa kuwa si nzuri.

 Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme nchini (ETDCO) imebuka mshindi kat...
24/02/2025



Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme nchini (ETDCO) imebuka mshindi katika kipengele cha Mkandarasi Bora wa Ujenzi wa Miundombinu ya Umeme, katika Tuzo za Zanzibar International Construction Awards (ZICA) zilizofanyika Zanzibar.

Akizungumza wakati akikabidhi Tuzo kwa Washindi, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohamed, amesema kuwa sekta ya ujenzi ni msingi mkuu wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, huku akiwataka washiriki wote kutumia tuzo hizo k**a chachu ya kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kufikia viwango vinavyohitajika na kuleta tija kwa Taifa.

Kaimu Meneja Mkuu wa ETDCO CPA. Sadock Mugendi, ameishukuru ZICA
kwa kutambua mchango wao katika sekta ya ujenzi wa miundombinu ya umeme nchini, na kuahidi kuendelea kutoa huduma zenye viwango ili kukuza uchumi wa nchi.

"ETDCO tumejipanga kuhakiksha tunaboresha matumizi ya teknolojia kwa kununua mashine za kisasa pamoja na kuwajengea uwezo wataalamu ili kufikia viwango vinavyohitajika kimataifa" amesema CPA. Mugendi

CPA. Mugendi ameeleza kuwa ETDCO ni kampuni iliyopewa jukumu la kutekeleza miradi ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya umeme kupitia wadau mbalimbali ikiwemo TANESCO, REA pamoja na makampuni binafsi.

Katika Tuzo za ZICA kilikuwa na washiriki 150 na ETDCO miongoni mwa washindi 30 waliotunukiwa tuzo hizo kutokana na ufanisi wa kazi pamoja na juhudi katika kuhakikisha miundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme inakuwa bora na salama ili watanzania waweze kupata umeme wa uhakika wakati wote na kupelekea kuchochea maendeleo ya uchumi kwa wananchi.

Address


Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00

Telephone

+255713422313

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Michuzi TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Michuzi TV:

Shortcuts

  • Address
  • Telephone
  • Opening Hours
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share