23/12/2025
Kupenda ni nini?
Ni nini maana halisi ya kupenda, ama upendo wa kweli ukoje?
Mapenzi ni neno linalojaribiwa kupewa tafsiri na watu wengi, ni hisia inayoaminika kupitiwa na watu wengi, ni hisia inayoshindwa kukwepeka japo mara nyingi huishia kuwaumiza watu.
Ni kwanini watu huumia katika mapenzi? Ni kwasababu watu wengi hawajui maana halisi ya mapenzi, Kupenda ni nini?
Leo tuzungumzie kuhusu hili, tuitafute maana halisi ya kupenda ni ipi.
Kijana na msichana wamekutana, kijana akavutiwa na mwonekano wa msichana kisha akaamini kuwa eti ndio anampenda.
Kiuhalisia kijana alivutiwa na msichana na kuona kuwa atakidhi mahitaji yake ya kimwili,kijana hakufikiria lolote la yeye kuwa na faida kwa msichana yule, isipokuwa amefikiria ni kwa kiwango gani msichana atamtimizia matamanio yake ya starehe zake za kimwili na msichana ni hivyo hivyo, japo mara nyingi wenyewe huvutiwa zaidi na wanaume watakaokidhi mahitaji yao ya kimaisha, apate kodi ya nyumba, apate kuvaa na kupendeza, atumie simu nzuri na gari zuri.
Kila mmoja hufikiri juu ya vile atakavyo faidi kihisia na mahitaji yake ya kimwili, kila mmoja hufikiri atakavyopata faida za kiuchumi. Hiyo ndio maana na vigezo walivyojiwekea binadamu siku hizi wanapochagua mpenzi wa kuwa nae.
SWALI: Je kwa kufanya hivyo tuko sawa au la? Yaani kumpenda mtu sababu tu anakutimizia matamanio na mahitaji yako.
Katika ukurasa wa Urban Dictionary msichana mmoja aliandika:-
"Upendo wa kweli haukutii upofu, ukimpenda mtu bado utaona kasoro zake lakini bado utamuona ni mzuri mbele yako. Utaona k**a uso wa unaempenda umejaa chunusi, utaona vile ambavyo unaempenda ni mfupi, utaona wengi ambao kwa hakika wamemzidi uzuri yule unayempenda , lakini bado utachagua kuendelea kumpenda yule uliye mchagua pamoja na kasoro zake na huo ndio upendo wa kweli".
Hapa tunapata somo la kujifunza, kwamba:-
Mapenzi sio kuvutiwa na mtu kwa tamaa za kimwili tu au mvuto wa maumbile, labda kifua kikubwa alichonacho au hipsi zilizishiba nyama. Mapenzi ya kweli yanavuka matamanio ya kimwili.
Nitakwambia mambo kadhaa yatakayo kufanya uelewe zaidi upendo wa kweli ni upi, una nguvu kiasi gani na haya maumivu mnayoyapitia siku hizi siri yake ikoje.
1. Ni ngumu mno kuupata upendo wa kweli, ni rahisi sana kwa penzi kuvunjika, kuliko kuanzisha penzi jipya. Yaani kwa sekunde moja tu ghafla amekuteleza, ameondoka na sio wako tena. Hivyo k**a kwa namna yeyote utapata mtu anayekupenda na ukadhani alichonacho ni upendo wa kweli, usiache upite.
2. Binadamu wanapokutana huwa inachukua dakika 4 tu nafsi zao kuchagua kupendana au la. Ukiona mtu ni mwaka wa nane sasa anakusumbua, anakuzungusha, hakupi jibu, pole... achana nae, acha kujiumiza huyo hakupendi.
3. Tafiti zinaonesha, katika mapenzi mkichaguana watu mnaofanana sana kwa tabia na vitu mnavyopenda na mnavyovichukia, basi hiyo nayo ni sababu moja wapo itakayo wafanya penzi lenu livunjike mapema.
Ni vyema wapenzi wakiwa wanaendana kwenye baadhi ya vitu ila mfanano ukiwa mkubwa basi maisha yenu yataboa mambo yatakuwa yanatabirika sana na kutakuwa hakuna suprize zinazochochea mapenzi yenu.
4. Na kwa watu wengi walio kwenye mahusiano tatizo lingine kubwa zaidi linalovunja maelewano, heshina na kupendana ni "Mawasiliano mabovu". Hii ndio sababu kubwa zaidi ya kuvunjika kwa mahusiano duniani kote.
Michepuko hupendwa zaidi sababu wana lugha za kupembeleza kuliko lugha za wapenzi wenu, wake au waume zenu. Maneno yako makali humfanya mpenzi wako akatafute kwingine kwa kubembelezwa.
Nimekwambia mambo ambayo yamekujenga na kukupa mtazamo mpya wa upendo yaani mapenzi, namaliza kwa kusema kuwa mapenzi ni kujitoa kwa dhati kwa yule unaempenda bila kutarajia chochote kutoka kwake.
Siri ya upendo wa kweli ipo kwenye kutoa na sio kupokea.
Maoni yako ni yapi juu ya posti hii?
Share kwa watu ambao unapenda waisome hii.
Follow kwa posti nyingi k**a hizi.