15/08/2025
Rais wa Zanzibar Dr. Hussein Ali Mwinyi Awataka Viongozi wa Dini na Waumini Kuiombea Nchi Amani Haswa Kipindi Hiki Kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Ameyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa swala ya ijumaa Ampapo Rais. Hussein Ali Mwinyi Alijumuika na waumini wa dini ya Kiislamu katika Sala ya Ijumaa pamoja na Dua Maalumu ya kuwaombea Viongozi Wakuu wa Nchi, iliyofanyika katika Msikiti wa Shaafi, Mbuyu Mnene, Mkoa wa Mjini Magharibi leo tarehe 15 Agosti 2025.
Katika salamu alizotoa baada ya swala na dua hiyo, amewasihi wanasiasa kutumia majukwaa ya kisiasa kutangaza sera za vyama vyao kwa wananchi badala ya kueneza siasa za chuki.
Ni vema wanasiasa kuhubiri amani na kueleza namna watakavyowatumikia wananchi baada ya kupata ridhaa ya kuwaongoza, badala ya kutangaza siasa za chuki, matusi na mifarakano ndani ya jamii.
Aidha, nimewasisitiza viongozi wa dini na waumini kuiombea nchi amani, hasa katika kipindi hiki ambacho kimebakia miezi michache kabla ya Uchaguzi Mkuu.