13/10/2025                                                                            
                                    
                                                                            
                                            JE? WASICHANA WA TANZANIA WANAPATA NAFASI YA KUONYESHA UONGOZI NA KULETA MABADILIKO KATIKA JAMII ZAO ?
Na Ezra Meshack
Katika wiki ya maadhimisho ya Mtoto wa k**e Duniani yaliyoanzishwa rasmi mwaka 2011 kwa lengo la kubaini changamoto zinazowakabili watoto wa k**e na kuwanyima fursa mbali mbali za muhimu katika maisha yao ambazo hufanyika kila mwaka tarehe 11 Octoba kumekuwa na mambo ya kujadili ikiwa ni pamoja na swali liloulizwa hapo juu
Akitoa majibu ya swali hilo Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Uvinza Bi Sharifa Masudi amesema jibu la hilo ni NDIYO tena ndiyo yenye ukubwa na uhakika zaidi kwa kutoa mfano kadhaa ya watoto wa k**e (wanawake) waliofanya, wanaofanya na wanaoendelea kufanya vizuri majukumu yao k**a viongozi, watumishi wa umma, wakuu wa taasisi na wengineo kwa kuonyesha mchango wao na mabadiliko waliyoleta kwa Jamii
"Tunae Rais wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan, tunae Dr. Amna Henga Mkurugenzi mtendaji wa LHRC anayepambania haki za wanawake na binadamu kwa ujumla, tunae Mwenyekiti wa Chupukizi wa CCM Taifa CDE Qayllah Bilal, tunae Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mh. Dinah Madhamani, Maafisa Maendeleo, Usitawi, Biashara, waandishi wa habari na kada zingine zote wote kwa pamoja wanaofanya kazi nzuri sana yenye mchango mkubwa na mabadiliko kwa Jamii" Sharifa
Lakini pia, amewasihi wazazi na walezi kuhakikisha wanawalinda watoto wa k**e dhidi ya ukatili wa aina zote bila  kuwasahau watoto wa kiume ambao nao pia wamekuwa wakikumbwa na ukatili k**a vile kulawitiwa na kupigwa kupita kiasi yote haya kwa pamoja yataifanya nchi yetu kuwa na watu bora, familia bora, watumishi bora na iongozi bora.
Kwa upande wake Mchungaji Eliud Rafael Mpinda wa Dayosisi ya Tanganyika Magharibi (D.W.T) Kanisa Anglikana Tanzania Parishi ya Uvinza amesema "watoto wa k**e ni tunu kubwa katika jamii na wanapaswa kupewa kupaumbele k**a ilivyo kwa watoto wa kiume"
Amesema, katika shughuli za kidini watoto wa k**e wanafanya vizuri na kwa uaminifu mkubwa katika nafasi mbali mbali ikiwemo kumwimbia Mungu (kwaya), kuhubiri injiri, uongozi wa makundi, Elimu na kadharika, huku akiwataka watoto wa k**e kuendelea kujitunza