
15/06/2023
RAIS DK.MWINYI KUMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA UZINDUZI WA MASHINDANO YA DUNIA YA OLIMPIKI MAALUMU
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dk.Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuondoka Zanzibar tarehe 15 Juni 2023 kuelekea Ujerumani kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi wa Mashindano ya Dunia ya Olimpiki Maalumu (Special Olympics World Games) ambayo maelfu ya wanamichezo wenye mahitaji maalumu kushindana katika michezo mbalimbali, mashindano hayo yanatarajiwa kuanza tarehe :17 hadi 25 Juni 2023.