TAMU FM

TAMU FM Tamu FM – Vipindi vya kujenga jamii, vijana & amani. Matangazo na ushirikiano: +255 690 000 128 | www.tamufm.com | [email protected]

05/09/2026

Taarifa inayosambazwa mitandaoni ikidai kuwa Mbunge wa Baraza la Wawakilishi na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu, Simai Mohammed Said, amesema kuwa "Tumsadie Rais Samia apate tena Urais 2030" si ya kweli. Hakuna ushahidi wowote unaothibitisha kuwa amewahi kutoa kauli hiyo.

02/09/2026

Dkt Samia awatolea 'uvivu' Wakuu wa Mikoa kukithiri uchafu

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amewataka wakuu wa mikoa wote nchini kusimamia usafi wa mazingira katika maeneo yao, akieleza kwa sasa baadhi ya maeneo hali si nzuri.

Kwa mujibu wa Samia, kitendo cha kuwapa madiwani zabuni za usafi ndio kinachosababisha uchafu, kwa sababu hawana uwezo wa kusimamia suala hilo, hivyo halmashauri zinapaswa kubadilika na kuwapa wakandarasi wenye uwezo.

Dkt Samia ameeleza hayo Jumatano Septemba 2,2026 wakati wa akiwaapisha wakuu wa mikoa na katibu tawala aliowateua hivi karibuni. Uapisho huo umefanyika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Kusini Unguja.

“Kuna watu wanaweza, wanaomba lakini mnawanyima.Mnawapa madiwani ili mkae nao vizuri, hawa uwezo, miji michafu, imeenea uchafu kila pembe aibu, hatuwezi kuendelea hivyo, nendeni mkasimie usafi, asiyeweza aondolewe,” amesema.

Katika uapisho huo, Rais Samia aliutaja Mkoa wa Dar es Salaam (uso wa Tanzania) akisema hajaridhika na suala la usafi, hasa katika mitaa yake, akiahidi kukaa nao kikao na watendaji wao mkoa huo.

“Lazima tuimarishe usafi wa nchi yetu, tuondoe uchafu. Tunapovutia watalii, mtalii hana kikomo, anapenya penya, kuna wengine wataka kuona tu Dar es Salaam ipoje,” amesema Dkt Samia.

02/09/2026

Dkt Samia awapa 'somo' wakuu wa mikoa

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amesema kupata uzoefu na kuondoa dhana ya watendaji kujenga ‘falme’ katika maeneo wanayohudumu ni miongoni mwa sababu zilizomfanya kufanya mabadiliko na kuwahamisha baadhi ya wakuu wa mikoa.

Dkt Samia ameeleza hayo Jumatano Septemba 2,2026 wakati wa akiwaapisha wakuu wa mikoa na katibu tawala aliowateua hivi karibuni. Uapisho huo umefanyika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Kusini Unguja.

“Moja ni kupata uzoefu kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine. La pili, kutotengeneza ufalme pale ulipo, kwamba ndio kwangu na himaya ulizozijenga ndio za kwako. Hapana, wewe ni mtumishi wa umma, unaweza kutumika popote pale,” ameeleza.

Rais Samia amekumbusha kuwa katika mkutano wake wa mwisho na wakuu wa mikoa aliwaambia kuwa yeye anawachukulia k**a jeshi lake, hivyo hatarajii kuona jeshi hilo likichafuka.

“Huko mliko nimekuwa nikipata taarifa hizi, zile; huyu ana hivi, huyu ana lile. Sasa kuwabadilisha ni kuwaondosha katika matatizo yale ambayo nayapokea. Sasa k**a ulikuwa unajijua una tabia mbaya au yoyote, nenda kajirekebishe, tumikia wananchi k**a inavyotakiwa,” amesema Dkt Samia.

02/09/2026

Dkt Samia awataka wakuu wa mikoa wakawe watumishi

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amewaambia wateuliwe wapya wa ukuu wa mkoa na katibu tawala kwamba hawajapeleka maeneo hayo, kuwa wafalme bali kuwa watumishi wa wananchi.

Dkt Samia ameeleza hayo Jumatano Septemba 2,2026 wakati wa akiwaapisha wakuu wa mikoa na katibu tawala aliowateua hivi karibuni. Uapisho huo umefanyika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Kusini Unguja.

Amefafanua kuwa kwa mujibu wa Katiba, Rais amekasimu madaraka yake katika eneo lililokatwa la mkoa na kukabidiwa wakuu wa mikoa.

“Wewe jichukulie k**a rais wa eneo hilo, mkoa hauna fedha ni lako, umekumbwa na mazingira baada ya mvua kunyesha ni lako, kwa Rais ni msaada tu,” amesema na kuongeza kuwa;

“Unabeba dhamana ya mkoa, na unasema huu mkoa na watu wake ndio Taifa langu, hatuwapeleki pale mkale raha,” amesema Rais Dkt Samia.

30/08/2026

RAIS DKT. MWINYI AWASILI SERBIA KUMWAKILISHA RAIS SAMIA KATIKA MKUTANO WA KUMBUKUMBU YA MIAKA 65 YA NAM

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewasili leo, tarehe 30 Agosti 2026, jijini Belgrade, Jamhuri ya Serbia, kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano Maalum wa Ngazi ya Juu wa Kumbukumbu ya Miaka 65 tangu kufanyika kwa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi wa Harakati za Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM).

Rais Dkt. Mwinyi amewasili akiwa ameambatana na ujumbe wake, akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nikola Tesla, Rais Dkt. Mwinyi amepokelewa na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Uchumi wa Jamhuri ya Serbia, Mhe. Adrijana Mesarović, pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Italia ambaye pia anaiwakilisha Tanzania katika Jamhuri ya Serbia, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk.

29/08/2026

RAIS DKT. MWINYI KUMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA KATIKA KUMBUKUMBU YA MIAKA 65 YA MKUTANO WA KWANZA WA NAM

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, anatarajiwa kuelekea Jamhuri ya Serbia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano Maalum wa Ngazi ya Juu wa Kumbukizi ya Miaka 65 tangu kufanyika kwa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM), jijini Belgrade.

Rais Dkt. Mwinyi, akiambatana na ujumbe wake, atashiriki maadhimisho hayo yatakayofanyika tarehe 31 Agosti hadi 01 Septemba 2026 katika Kasri la Serbia, jijini Belgrade, nchini Serbia.

Rais Dkt. Mwinyi anatarajiwa kuondoka Zanzibar tarehe 29 Agosti 2026 na kurejea tarehe 02 Septemba 2026, mara baada ya kukamilisha ziara hiyo.

29/08/2026
29/08/2026

Ndejembi ukakue akili, usiharibikiwe -Rais Samia

Rais Samia Suluhu Hassan, amemtaka Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi kuhakikisha anatumia wadhifa aliopewa kukua kiakili badala ya kuharibikiwa.

Mkuu huyo wa nchi, ameyasema hayo leo, Agosti 29, 2026 wakati wa hotuba yake baada ya uapisho wa Ndejembi uliofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Amerejea kauli ya Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, aliyewahi kuwasihi vijana wasiwe k**a samaki kwa kadiri anavyokua na akili inaharibika.

Rais Samia, amesema pamoja na kumpa majukumu makubwa, anaamini atayamudu.

29/08/2026

Rasmi Ndejembi aapishwa kuwa Makamu wa Rais

Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi, ameapishwa kushika wadhifa huo rasmi, siku tatu baada ya jina lake kupendekezwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Jina la Ndejembi, lilipendelezwa Agosti 26, 2026 na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Dk Emmanuel Nchimbi, aliyejiuzulu na baadaye kufukuzwa uanachama wa CCM.

Jana, Agosti 28, 2026 jina la Ndejembi lilipelekwa bungeni na kuthibitishwa kwa kura za ndio 329 sawa na asilimia 100 ya wabunge waliokuwepo bungeni.

Ndejembi, ameapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, George Masaju leo, Agosti 29, 2026 Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, tukio lililoshuhudiwa na Rais Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wa Serikali.

28/08/2026

Bunge lamthibitisha Ndejembi kwa asilimia 100, aahidi utii kwa Rais Samia

Bunge la Tanzania limemthibitisha Deogratius Ndejembi, kuwa Makamu wa Rais mteule kwa asilimia 100, akisema dhamana aliyopewa haitapimwa kwa ujana wake, bali utii kwa Rais Samia Suluhu Hassan na uadilifu kwa Watanzania.

Ndejembi, amethibitishwa na Bunge, kwa kupigiwa kura za ndiyo na wabunge wote 324 waliokuwepo bungeni, sawa na asilimia 100. Hakukuwa na kura ya hapana wala iliyoharibika.

Akizungumza baada ya kuthibitishwa bungeni jijini Dodoma leo, Agosti 28, 2026 Ndejembi, amesema ukubwa wa dhamana hiyo hautapimwa kwa ujana wake, bali kwa utii kwa Rais, uadilifu kwa Watanzania, kazi yoyote atakayotumwa kuitekeleza na mkuu wa nchi.

Ameeleza anakwenda kuwa Makamu wa Rais sio wa Wana CCM pekee, bali vyama vyote na Watanzania kwa ujumla k**a ilivyo kwa Rais wa nchi.

“Nitajitahidi kwa unyeyekevu mkubwa sana, kumsaidia Rais kuwa kiungo kwa Watanzania wote. K**a vile mapenzi yake yatakavyotaka kwa sababu nafanya kazi chini ya Rais Samia Suluhu Hassan,” amesema Ndejembi.

Address

Zanzibar
Zanzibar City
71800

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TAMU FM posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category