25/06/2025
🌐 JavaScript – Lugha ya Wavuti Unayopaswa Kuelewa!
Je, umewahi kubonyeza button kwenye website na ukashangaa jinsi kila kitu kinavyotokea kwa haraka? Popups, animations, forms zinazojijaza, hata apps unazotumia kwenye simu – yote hayo yanawezekana kwa sababu ya JavaScript.
Katika video hii ya pili ya mfululizo wa lugha za programu kwa Kiswahili, utajifunza:
✅ JavaScript ni nini?
✅ Inafanya kazi gani kwenye wavuti?
✅ Inatumika wapi (frontend & backend)?
✅ Nani anapaswa kujifunza lugha hii?
✅ Na kwa nini wewe unapaswa kuanza kuijifunza leo?
💡 JavaScript ni lugha ya lazima kwa yeyote anayependa kutengeneza websites, apps, au hata kucheza na data. Imeajiri mamilioni ya developers duniani, na bado mahitaji yanaongezeka kila siku.
👨💻 Iwe wewe ni mwanafunzi, mpenda teknolojia, au mtu unayetaka kubadili kazi yako – hii ni video sahihi kwako.