19/12/2025
Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda imefanya ziara maalum ya kukagua Miradi ya Maendeleo ya Viwanda katika eneo tengefu la Uwekezaji wa Viwanda liliopo Dunga Zuze, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusuni Unguja kwa lengo la kuona hatua iliyofikiwa kwa Miradi hiyo.
Aidha ziara iliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Habiba Hassan Omar ambae aliambatana na Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Viwanda, Dkt. Abdulla R. Abdulla, Katibu Tawala Wilaya ya Kati,Ndugu Hamza Ibrahim Mahmoud, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kati (OCD), Joram. N. Samson, Afisa wa Idara ya Uhamiaji, na Maafisa kutoka Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda.
Viongozi hao kwa pamoja walitembelea ujenzi wa kiwanda cha nguo (Mama Afrika Textile Company Lilited), kiwanda cha Dawa (Africa Bio Chem Co. Ltd na Kiwanda cha kusarifu chuma, mbao na Aluminiam (Arenist Group (Z) Company Lilited) na kuona hatua iliyofikiwa ya ujenzi huo wa Viwanda.
Ziara hiyo imefanyika leo tarehe 18/12/2025 ikiwa ni hatua ya maandalizi ya uwekaji wa jiwe la msingi kwa Miradi ya Wizara kufuatia maandalizi ya Sherehe za miaka 62 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
Idara ya Habari Maelezo Zanzibar
Ikulu habari Zanzibar
Wizara ya Viwanda na Biashara
MKOA WA Kusini Unguja
Zanzibar Fair Competition Commission
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania