Tifu Tv Zanzibar

Tifu Tv Zanzibar ASILI KWANZA

Mkutano huo, umeongozwa na kinara wa mageuzi ya taasisi za Umoja wa Afrika ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. D...
25/10/2025

Mkutano huo, umeongozwa na kinara wa mageuzi ya taasisi za Umoja wa Afrika ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Ruto na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali na wawakilishi wa kisekta wa Umoja wa Afrika.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa T...
25/10/2025

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Kamati Maalum ya Uangalizi ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) kuhusu Mageuzi ya Taasisi za Umoja wa Afrika, uliyofanyika kwa njia ya mtandao akiwa Jijini Dodoma.

CP ZANZIBAR AWAKAKIKISHIA USALAMA SIKU YA UCHAGUZI MKUUJeshi la Polisi limewataka wananchi kutokuwa na khofu ya ulinzi n...
25/10/2025

CP ZANZIBAR AWAKAKIKISHIA USALAMA SIKU YA UCHAGUZI MKUU
Jeshi la Polisi limewataka wananchi kutokuwa na khofu ya ulinzi na usalama wao siku ya uchaguzi Oktoba 29, 2025 na limewasihi wakapige kura na limewahakikishia kuwa hakutakuwa na changamoto za kiusalama.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Kamishna wa Polisi Zanzibar CP KOMBO KHAMIS KOMBO leo Oktoba 24, 2025 Makao Makuu ya Polisi Kamisheni ya Zanzibar amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vikosi vyengine vya ulinzi na usalama limejipanga na limeweka mikakati ya kuimarisha ulinzi wakati na baada ya uchaguzi.
INSERT CP KOMBO KHAMIS KOMBO KAMISHNA WA POLISI ZANZIBAR ………………………………………
Amesisitiza Jeshi la Polisi litawachukulia hatua kwa mujibu wa sheria na halitakubali, halitamvumilia mtu au kikundi kitakachojaribu kuchochea ghasia, Kuhamasisha maandamano haramu au Kuwashawishi wananchi kuvunja sheria.
INSERT CP KOMBO KHAMIS KOMBO KAMISHNA WA POLISI ZANZIBAR ………………………………………

SACP SENGA AKIMKABIDHI FUNGUO ZA GARI HIZO SSP KADOGOSA  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi Mwandamizi ...
24/10/2025

SACP SENGA AKIMKABIDHI FUNGUO ZA GARI HIZO SSP KADOGOSA Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga, amekabidhi magari mawili mapya aina ya Robur Armored TLC300 kwa Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoa wa Songwe kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camillus Wambura.

Makabidhianao hayo yamefanyika Oktoba 23, 2025, katika ofisi ya Kamanda Mkoa wa Songwe iliyopo Vwawa Wilaya ya Mbozi Mkoani humo na mara baada ya kukabidhi magari hayo, SACP Senga alitoa shukrani za dhati kwa IGP Camillus Wambura na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuimarisha uwezo wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kupitia upatikanaji wa vitendea kazi vya kisasa, huku akisema kuwa magari hayo yataongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku hususan katika kudhibiti ghasia, kulinda raia na mali zao, pamoja na kuimarisha amani na utulivu Mkoani humo.

Makamu Mwenyekiti  wa CCM (Bara) Ndg. Stephen Wasira  akizungumza na viongozi wa CCM wilayani Bariadi Mkoa wa Simiyu, Le...
18/10/2025

Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Stephen Wasira akizungumza na viongozi wa CCM wilayani Bariadi Mkoa wa Simiyu, Leo Oktoba 18 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameshiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi...
17/10/2025

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameshiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ Troika Summit) kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, uliofanyika kwa njia ya mtandao akiwa Babati mkoani Manyara.

Mkutano huo umeongozwa na Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Malawi Mhe. Prof. Arthur Peter Mutharika.

Mkutano huo umejadili hali ya kisiasa na usalama katika Jamhuri ya Madagascar kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika hivi karibuni.

Pia umeweka dhamira ya kuunga mkono juhudi za kurejesha hali ya amani na utulivu Jamhuri ya Madagascar na kutoa wito kwa wananchi wa Madagascar kuhakikisha njia ya mazungumzo inatumika katika kukabiliana na hali iliyopo hivi sasa na kuachana na vurugu, uporaji na uharibifu wa mali.

Mkutano huo, umeiagiza Sekretarieti ya SADC kuhakikisha inashirikisha wadau muhimu k**a vile Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Kamisheni ya Nchi za Bahari ya Hindi ili kuwa na uratibu wa pamoja katika kutafuta suluhu ya mgogoro nchini Madagascar.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
16 Oktoba 2025
Babati – Manyara.

MAKAMU WA RAIS AWASILI KENYA KUMWAKILISHA RAIS MAZISHI YA KITAIFA YA RAILA ODINGA (PRESS/ PICHA CAPTION - MAKAMU WA RAIS...
17/10/2025

MAKAMU WA RAIS AWASILI KENYA KUMWAKILISHA RAIS MAZISHI YA KITAIFA YA RAILA ODINGA (PRESS/ PICHA CAPTION - MAKAMU WA RAIS AWASILI KENYA KUMWAKILISHA RAIS MAZISHI YA KITAIFA YA RAILA ODINGA)

Vijana mbalimbali wa halaiki wakifanya maonesho mbalimbali wakati wa hafla ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, K...
14/10/2025

Vijana mbalimbali wa halaiki wakifanya maonesho mbalimbali wakati wa hafla ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, Kumbukizi ya Baba wa Taifa hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere pamoja na Wiki ya Vijana Kitaifa kwa Mwaka 2025 zilizofanyika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya leo tarehe 14 Oktoba 2025.

DK.MWINYI AKUTANA NA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM TZ BARAMakamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi, ambaye pi...
30/09/2025

DK.MWINYI AKUTANA NA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM TZ BARA

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi, ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara, Ndugu Stephen Masato Wasira aliyefika Ikulu Zanzibar , leo tarehe 30 Septemba 2025.

MAKAMU WA RAIS KUSHIRIKI MKUTANO WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA - MAREKANI
20/09/2025

MAKAMU WA RAIS KUSHIRIKI MKUTANO WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA - MAREKANI

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, akimuombea kura Mgombea wa Ubunge jimbo la...
16/09/2025

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, akimuombea kura Mgombea wa Ubunge jimbo la Njombe Ndg. Deo Mwanyika katika Mkutano wa Ndani uliofanyika wilayani humo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi Jamii Wilaya ya Mbozi Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Deborah Mhekwa, aliwataka wananch...
15/09/2025

Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi Jamii Wilaya ya Mbozi Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Deborah Mhekwa, aliwataka wananchi hao kuongeza juhudi za kukomesha mimba za utotoni, kwa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi, huku akiwasisitiza kuwa mimba za utotoni hukatisha ndoto za watoto wa k**e na kuongeza utegemezi katika jamii, hivyo aliwataka wazazi, walezi na jamii nzima kushirikiana katika malezi bora ili watoto wa k**e waweze kutimiza ndoto zao za baadae.

Ikumbukwe kuwa fainali ya Mavuno Cup ndani ya Kata ya Hasamba imeendelea kuonyesha wazi kuwa michezo ni zaidi ya burudani, pia ni jukwaa la kukuza uelewa wa haki za binadamu, ustawi wa jamii, na ujenzi wa taifa lenye amani na mshik**ano.

Address

VIKOKOTONI
Zanzibar

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tifu Tv Zanzibar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Tifu Tv Zanzibar:

Share