Vibration tv

Vibration tv VIBRATIONS TV
BURUDANI MASIKIO PAKO

KWA NINI BRAZIL HUANZA HOTUBA KATIKA MKUTANO MKUU WA UMOJA WA MATAIFA?NEW YORK, Marekani.Kila mwaka Viongozi wa dunia wa...
09/24/2026

KWA NINI BRAZIL HUANZA HOTUBA KATIKA MKUTANO MKUU WA UMOJA WA MATAIFA?

NEW YORK, Marekani.

Kila mwaka Viongozi wa dunia wanapokusanyika katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN General Assembly) Jijini New York, kuna utaratibu wa kidiplomasia unaojirudia: Brazil huwa nchi ya kwanza kuzungumza katika mjadala mkuu, ikifuatiwa na Marekani, ambayo ni mwenyeji wa Umoja wa Mataifa.

Umoja wa Mataifa unasema nafasi hiyo ya Brazil si haki maalum iliyoandikwa katika sheria au kanuni za shirika hilo, bali ni heshima ya kidiplomasia iliyojengwa na utamaduni wa muda mrefu. Tangu kikao cha 10 cha Mkutano Mkuu mwaka 1955, Brazil imekuwa ikifungua rasmi mjadala mkuu, kabla ya Marekani kupewa nafasi ya pili k**a nchi mwenyeji.

Mizizi ya utamaduni huo inarudi katika miaka ya mwanzo ya Umoja wa Mataifa, ambapo Mwanadiplomasia wa Brazil Oswaldo Ar**ha alikuwa na nafasi muhimu katika shughuli za shirika hilo. Ar**ha aliongoza kikao maalumu cha kwanza cha Mkutano Mkuu mwaka 1947 na baadaye akachaguliwa kuwa Rais wa kikao cha pili cha Mkutano Mkuu mwaka huo huo.

Kwa mujibu wa maelezo ya Umoja wa Mataifa, heshima ya Brazil kuanza mjadala mkuu ilijengwa kutokana na nafasi yake katika miaka ya mwanzo ya shirika hilo na baadaye kuwa utaratibu wa kidiplomasia. Umoja wa Mataifa unasisitiza kwamba utaratibu huo haujawekwa kuwa sheria ya lazima, bali ni desturi iliyodumu kwa miongo kadhaa.

Taarifa ya Folha de S.Paulo pia inaeleza kuwa utamaduni huo umehusishwa na kipindi cha mwanzo cha Umoja wa Mataifa, wakati Brazil ilijitokeza kuchukua nafasi ya kuanzisha mjadala. Tangu mwaka 1955, mpangilio huo umekuwa ukifuata mfumo wa Brazil kwanza na Marekani baada yake, ingawa kumekuwa na tofauti chache katika historia. Mwaka 1983 na 1984, kwa mfano, Marekani ilizungumza kabla ya Brazil.

Baada ya hotuba za Brazil na Marekani, mpangilio wa Viongozi wengine huamuliwa kwa kuzingatia mambo mbalimbali ya kiitifaki na kiutendaji, ikiwemo ngazi ya mwakilishi anayehutubia, uwiano wa kijiografia na utaratibu wa kujiandikisha katika orodha ya wazungumzaji.

Nafasi ya kwanza imekuwa pia na umuhimu wa kidiplomasia kwa Brazil kwa sababu inaiwezesha nchi hiyo kutoa ujumbe wake kwa Viongozi wa dunia, wanadiplomasia na vyombo vya habari kabla ya hotuba nyingi za Viongozi wengine kuanza. Kwa miaka mbalimbali, Brazil imekuwa ikitumia jukwaa hilo kueleza misimamo yake kuhusu ushirikiano wa kimataifa, maendeleo, njaa, mabadiliko ya tabianchi, amani na mageuzi ya mfumo wa kimataifa.

Katika Mkutano Mkuu wa 81 wa Umoja wa Mataifa mwaka 2026, utamaduni huo uliendelea ambapo Rais Luiz Inácio Lula da Silva wa Brazil alifungua mjadala mkuu tarehe 22 Septemba, kabla ya hotuba ya Rais wa Marekani Donald Trump.

Hata hivyo, kuwa nchi ya kwanza kuzungumza hakumpei Brazil mamlaka ya ziada ndani ya Umoja wa Mataifa, wala haki maalum katika upigaji kura. Ni nafasi ya kiitifaki na kidiplomasia iliyogeuka kuwa moja ya mila zinazotambulika zaidi katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Toa maoni yako

TRUMP AISHAMBULIA UN NA CPI, ATAKA NCHI WANACHAMA KUJIONDOA MARA MOJA.NEW YORK, Marekani.Rais wa Marekani, Donald Trump,...
09/24/2026

TRUMP AISHAMBULIA UN NA CPI, ATAKA NCHI WANACHAMA KUJIONDOA MARA MOJA.

NEW YORK, Marekani.

Rais wa Marekani, Donald Trump, ameshambulia vikali Umoja wa Mataifa (UN) na Mahak**a ya Kimataifa ya Uhalifu (CPI), akisisitiza umuhimu wa mamlaka ya kitaifa na kupinga kile alichokiita kuongezeka kwa nguvu za taasisi za kimataifa.

Trump alitoa kauli hizo Jumanne, Septemba 22, 2026, wakati akihutubia Mjadala Mkuu wa Kikao cha 81 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Mjini New York.

Katika hotuba hiyo, Trump aliikosoa vikali CPI, akisema Marekani haitakubali wanajeshi wake au Raia wake kuchunguzwa au kufikishwa katika mahak**a hiyo, ambayo aliieleza kuwa haina mamlaka juu ya Marekani.

Akiitaka nchi wanachama wa CPI kujiondoa katika taasisi hiyo, Trump alisema: “Marekani pia inapinga kabisa taasisi isiyodhibitiwa inayojulikana k**a Mahak**a ya Kimataifa ya Uhalifu. Hatutawahi kuruhusu wanajeshi wa Marekani au mtu mwingine yeyote kuchunguzwa au kufikishwa katika kesi za maonyesho na mahak**a inayopinga Marekani ambayo haina mamlaka juu yetu. Ni kundi la watu waovu. Ninaziomba nchi zote ambazo ni wanachama wa CPI kujiondoa rasmi katika taasisi hii potovu mara moja.”

Kauli hiyo inakuja wakati utawala wa Trump ukiendelea kuchukua msimamo mkali dhidi ya CPI. Human Rights Watch imesema Marekani imekuwa ikiendesha kampeni ya kuidhoofisha mahak**a hiyo, huku ikitaja pia vikwazo vilivyowekwa dhidi ya baadhi ya maafisa na majaji wa CPI.

Trump pia aliikosoa Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa pamoja na UNESCO, akidai kuwa taasisi hizo zinaingilia masuala ambayo, kwa mtazamo wake, yanapaswa kuamuliwa na mataifa yenyewe.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Trump alihusisha mjadala wa uhamiaji na suala la mamlaka ya kitaifa, akisema:

“Hakuna haki ya binadamu ya uhamiaji haramu, lakini kuna haki ya kubaki taifa lenye mamlaka kamili, na tunataka kubaki taifa lenye mamlaka kamili, na ninyi pia mnapaswa kufanya hivyo.”

Trump pia alisema hakuna “serikali ya dunia”, akisisitiza kwamba Marekani haitakubali mipango ya kimataifa ambayo, kwa mtazamo wake, inalenga kuhamisha mamlaka kutoka kwa mataifa kwenda kwenye taasisi za kimataifa. Ikulu ya Marekani imeeleza hotuba hiyo k**a msisitizo wa sera ya “kurejesha” mamlaka ya Marekani na kulinda uhuru wake wa kitaifa.

Toa maoni yako

PEZESHKIAN AONYESHA PICHA ZA WATOTO WALIOUAWA MINAB MBELE YA UN; ASEMA “ISRAEL INAUWA, IRAN INAWEKEWA VIKWAZO”.Rais wa I...
09/24/2026

PEZESHKIAN AONYESHA PICHA ZA WATOTO WALIOUAWA MINAB MBELE YA UN; ASEMA “ISRAEL INAUWA, IRAN INAWEKEWA VIKWAZO”.

Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, ameitumia hotuba yake katika Mkutano Mkuu wa 81 wa Umoja wa Mataifa (UN) Mjini New York, Marekani kuonyesha picha za watoto waliouawa katika shambulio la anga dhidi ya Shule ya Msingi ya Shajareh Tayyebeh Mjini Minab, Iran, pamoja na picha za Ali Khamenei, Kiongozi Mkuu wa zamani wa Iran aliyeuawa katika mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

Pezeshkian, akizungumza Jumatano, Septemba 23, 2026, alikosoa kile alichokiita viwango viwili katika namna Jumuiya ya kimataifa inavyoshughulikia Iran na Israel, huku akikanusha madai ya Marekani kwamba Iran ni mfadhili mkuu wa ugaidi.

“Tumekuwa wahanga wa ugaidi.” Pezeshkian alisema, akijibu kauli za Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu Iran. Aliongeza: “Tumekuwa tukijilinda tu. Sisi si magaidi.”

Rais huyo pia alizungumzia shambulio la Minab, ambalo kwa mujibu wa uchunguzi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kutafuta ukweli, kuna “sababu za msingi za kuamini” kuwa Marekani ilihusika katika shambulio hilo na kwamba tukio hilo linaweza kuwa uhalifu wa kivita. Ripoti hiyo ilisema shambulio hilo liliua zaidi ya Raia 150, wakiwemo zaidi ya watoto 120.

Ripoti zinaeleza kuwa shambulio hilo la Februari 28 liliua angalau watu 168, wengi wao wakiwa watoto, huku mamlaka za Iran zikisema wanafunzi 120 na wafanyakazi 26 wa shule waliuawa. AP pia imebaini ushahidi kwamba angalau kombora moja la Marekani liliipiga shule hiyo, ingawa serikali ya Marekani haijatoa hadharani matokeo ya uchunguzi wake wa kijeshi kuhusu tukio hilo.

Akisisitiza hoja yake kuhusu kile anachokiona k**a kutotumika kwa viwango sawa katika siasa za kimataifa, Pezeshkian alisema: “Silaha za nyuklia ziko Israel, lakini wakaguzi wako Iran. Israel inaua, lakini Iran inawekewa vikwazo.”

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Pezeshkian alisema Marekani na Israel ziliishambulia Iran kwa kutumia silaha za kisasa, huku Iran ikijibu kwa kile alichokiita kujilinda. Alisema: “Marekani na Israel walitushambulia kwa silaha za kisasa, nasi tulijilinda kwa nguvu.”

Pezeshkian pia alieleza kuwa mashambulizi hayo yaliwalenga Raia, wakiwemo watoto, na akataja vifo vya watu katika Minab na maeneo mengine ya Iran.

Pezeshkian pia aliendelea kukosoa vikwazo dhidi ya Iran, akisema vinaathiri Raia wa kawaida, wakiwemo Wagonjwa, maskini na watu walio katika mazingira magumu.

“Israel inaua. Sisi tunawekewa vikwazo. Tunaadhibiwa. Hiki ni kiwango cha aina mbili.” alisema, akitaka kuwe na viwango vinavyofanana kwa nchi zote.

Akizungumzia Palestina, Rais huyo wa Iran alisema hali ya Palestina imeendelea kuwa jeraha kwa dhamiri ya Jumuiya ya kimataifa, akisisitiza kwamba amani ya kudumu katika Asia Magharibi haiwezi kupatikana bila haki kwa Palestina.

Hotuba ya Pezeshkian imekuja siku moja baada ya Trump kuhutubia Mkutano Mkuu wa UN na kutoa onyo kali dhidi ya Iran, huku akisema Marekani inaweza “kuangamiza” Iran iwapo makubaliano ya amani hayatapatikana.

Kwa upande mwingine, uchunguzi wa Umoja wa Mataifa kuhusu mashambulizi ya Marekani nchini Iran pia umetaja madai ya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na serikali ya Iran, ikiwemo mauaji, mateso na uk**ataji holela katika kukabiliana na maandamano ya ndani. Marekani imekataa matokeo ya ripoti hiyo na kuikosoa baraza la UN lililohusika na uchunguzi.

Toa maoni yako

M23 YAKUMBWA NA MGOGORO WA NDANI KUHUSU UONGOZI WA KIJESHI.Mvutano wa ndani umeibuka katika uongozi wa kisiasa na kijesh...
09/24/2026

M23 YAKUMBWA NA MGOGORO WA NDANI KUHUSU UONGOZI WA KIJESHI.

Mvutano wa ndani umeibuka katika uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Muungano wa Waasi wa AFC-M23, unaoendesha shughuli za kijeshi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), huku jaribio la kuhoji mamlaka ya k**anda wake wa kijeshi, Jenerali Sultani Makenga, likiripotiwa kuzuiwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na Africa Intelligence tarehe 23 Septemba 2026, kumekuwa na mgawanyiko ndani ya uongozi wa AFC-M23, ambapo mpango wa kubadilisha mfumo wa uongozi na kupunguza au kuondoa mamlaka ya Makenga ulidaiwa kuandaliwa na baadhi ya Viongozi wa kundi hilo.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa mpango huo ulihusisha kuandaliwa kwa muundo mpya wa uongozi, ikiwa ni pamoja na mgawanyo mpya wa nafasi za kiutawala katika maeneo yanayodhibitiwa na AFC-M23.

Miongoni mwa majina yaliyotajwa katika mpango huo ni Théo Binamungu, ambaye alitarajiwa kupewa nafasi ya uongozi katika Mkoa wa Nord-Kivu, huku Jean-Marie Runiga akitajwa katika mpango wa kupewa nafasi ya kuongoza Sud-Kivu. Taarifa nyingine za ndani ya DRC pia zimeripoti kuwa Binamungu alik**atwa mwishoni mwa Agosti huko Goma na baadaye kuhamishiwa katika Gereza la Munzenze.

Kwa mujibu wa ripoti hizo, mvutano huo unaonekana kuhusisha tofauti kati ya mrengo wa kijeshi unaohusishwa na Makenga na sehemu ya uongozi wa kisiasa wa AFC.

Africa Intelligence imeripoti kwamba mpango huo uliokuwa ukilenga mamlaka ya Makenga uligunduliwa na kuzuiwa, hali inayodhihirisha uwepo wa tofauti za ndani katika kile kinachoitwa uongozi wa kisiasa na kijeshi wa AFC-M23.

Hata hivyo, baadhi ya maelezo kuhusu watu waliokuwa wakipendekezwa kushika nafasi mbalimbali yametolewa na vyanzo vya habari vya ndani na hayajathibitishwa kwa upande huru. Africa Intelligence yenyewe inathibitisha kuwepo kwa taarifa kuhusu jaribio la kuhoji mamlaka ya Makenga, lakini maelezo yote ya muundo uliopendekezwa wa uongozi hayajaweza kuthibitishwa kwa vyanzo huru.

Mpaka sasa, uongozi wa AFC-M23 haujatoa taarifa rasmi ya hadharani inayothibitisha au kukanusha madai hayo.

Taarifa hizi zinaibuka wakati M23 ikiendelea kuwa mhusika mkuu katika mzozo wa mashariki mwa DRC, huku muundo wa uongozi wa kisiasa na kijeshi wa AFC-M23 ukiendelea kufuatiliwa na Umoja wa Mataifa na vyombo vya habari vya kimataifa.

Toa maoni yako

LISSU AANZA MAWASILISHO YA MWISHO, ASEMA ADHABU YA KIFO HAIWEZI KUTUMIKA KWA MAKOSA YA KISIASA.Dar es Salaam, Tanzania.M...
09/24/2026

LISSU AANZA MAWASILISHO YA MWISHO, ASEMA ADHABU YA KIFO HAIWEZI KUTUMIKA KWA MAKOSA YA KISIASA.

Dar es Salaam, Tanzania.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ameanza kuwasilisha hoja zake za mwisho katika kesi ya uhaini inayomkabili mbele ya Mahak**a Kuu ya Tanzania, akisisitiza kuwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania na ushahidi uliowasilishwa Mahak**ani, hawezi kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa kile alichokitaja kuwa makosa yanayotokana na shughuli za kisiasa.

Lissu ameyasema hayo Jumatano, Septemba 23, 2026, wakati akianza Final Submissions mbele ya Jopo la Majaji watatu linaloongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, akisaidiwa na Majaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde.

Katika mawasilisho yake, Lissu amesema kesi hiyo ina umuhimu mpana kisheria kwa sababu uamuzi wa mahak**a unaweza kuweka msingi wa kisheria utakaotumika katika kesi zijazo.

Kwa mujibu wa habari hiyo, Lissu ameliambia Jopo hilo kuwa Majaji hawataamua tu hatma yake binafsi, bali wanaweza kuweka mfano wa kisheria utakaofuatwa na mahak**a kwa miaka mingi ijayo. Ameomba uamuzi utolewe kwa ujasiri, bila upendeleo na kwa kuzingatia viapo vyao vya kimahak**a.

Lissu pia amesisitiza kuwa hakuwahi kuficha wala kukana kutoa kauli zinazohusishwa na mashtaka dhidi yake, lakini anapingana na tafsiri kwamba kauli hizo zinatimiza kosa la uhaini chini ya sheria za Tanzania.

Katika maelezo yaliyoripotiwa kutoka mahak**ani, Lissu amesema: “Sijawahi kuficha wala kukana maneno ninayodaiwa kusema. Mkiangalia ukurasa wa 97 wa rekodi ya Mahak**a ya Kabidhi Kisutu tarehe 18 Agosti 2025, niliiambia Mahak**a Kabidhi maneno yafuatayo: ‘Ni kweli nilitamka maneno hayo katika mkutano wa wazi, suala ni k**a maneno hayo yanafanya kosa linalodaiwa kuwa ni uhaini.’”

Akiendelea kueleza msimamo wake, Lissu amesema suala kuu si k**a alitamka maneno hayo au la, bali k**a maneno hayo yanaweza kisheria kuunda kosa la uhaini.

Lissu anakabiliwa na shtaka linalohusiana na madai kwamba Aprili 3, 2025, alitenda kwa nia ya kulazimisha Serikali kwa kuwahamasisha wananchi kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2025 kupitia kauli na machapisho mtandaoni. Lissu anakiri kutoa baadhi ya kauli zinazohusishwa na kesi hiyo, lakini anapinga kwamba kauli hizo zilikuwa kosa la jinai.

Katika hatua ya awali ya kesi, upande wa mashtaka uliwasilisha mashahidi 17, huku upande wa utetezi ukiwasilisha mashahidi watano, akiwemo Lissu mwenyewe. Utetezi ulifungwa Septemba 18, 2026 baada ya Afisa waandamizi wa usalama waliokuwa wamependekezwa kuwa mashahidi wa utetezi kutotoa ushahidi.

Kesi hiyo inasikilizwa chini ya Kifungu cha 39(2)(d) cha Penal Code, kinachohusu kitendo cha kutishia Serikali. Imeelezwa kuwa Lissu amebainisha tofauti kati ya shtaka lake na kesi mbili zilizowahi kufunguliwa Tanzania chini ya Kifungu cha 39, ambazo zilihusisha madai ya kujaribu kuipindua Serikali au kumuua Rais.

Katika sehemu nyingine ya mawasilisho yake, Lissu amesema: “Wanaosema nifungwe, waambieni katika historia hakuna shujaa yeyote anayeitwa shujaa ambaye hajaonja kifungo au mambo tunayopitia. Hilo sio taji la miba ni taji la dhahabu. Ni taji ambalo limetengwa kwa ajili ya watu wa maana.”

Kauli hiyo aliitoa leo hii Septemba 23, 2026 wakati akiendelea na mawasilisho yake ya mwisho.

Aidha, Lissu amewaomba Majaji kutoa uamuzi bila upendeleo na kwa ujasiri. Kesi hiyo imeendelea kuvuta uangalizi wa kimataifa kutokana na uwezekano wa adhabu ya kifo endapo atapatikana na hatia.

Imeripotiwa kuwa mawasilisho ya mwisho yameanza baada ya kukamilika kwa ushahidi wa pande zote, huku upande wa mashtaka ukisisitiza kuwa ushahidi uliowasilishwa unakidhi kiwango kinachohitajika kisheria, wakati utetezi ukipinga uhalali wa hoja hiyo.

Mawasilisho ya mwisho yanaendelea, na kwa taarifa iliyotolewa kuhusu mwenendo wa shauri hilo, Lissu ameendelea na hoja zake katika hatua hii ya mwisho ya kesi kabla ya Mahak**a kuanza hatua ya kuzingatia hoja za pande zote na baadaye kutoa uamuzi kwa mujibu wa sheria.

Kesho tena Septemba 24, wasilisho la mwisho la Lissu litaendelea.

Toa maoni yako

MWENDESHA BAISKELI MIGUEL MASAÏSAÏ AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI CONGO-BRAZZAVILLEMwendesha Baiskeli kutoka Jamhuri ya Kide...
09/21/2026

MWENDESHA BAISKELI MIGUEL MASAÏSAÏ AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI CONGO-BRAZZAVILLE

Mwendesha Baiskeli kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Miguel Masaïsaï, amefariki dunia Ijumaa, Septemba 18, 2026, baada ya kupata ajali ya barabarani katika eneo la Ouesso, kaskazini mwa Jamhuri ya Congo (Congo-Brazzaville), karibu na mpaka wa Cameroon.

Taarifa kuhusu kifo chake imethibitishwa na vyanzo rasmi vya Serikali ya DRC, huku ikielezwa kuwa Masaïsaï alipoteza maisha wakati akiendelea na safari yake ya Baiskeli barani Afrika.

Masaïsaï alikuwa akitekeleza mradi wake uliouita “Pedals for Peace”, safari ya takribani kilomita 14,000 kutoka Mjini Goma, mashariki mwa DRC, hadi Mjini Rabat nchini Morocco, akilenga kutumia mchezo wa Baiskeli kueneza ujumbe wa amani na umoja barani Afrika.

Alianza safari hiyo Mei 1, 2026, na baada ya kuvuka DRC kutoka mashariki hadi magharibi, aliwasili Kinshasa Agosti 5 baada ya kutumia siku 67 barabarani na kusafiri zaidi ya kilomita 6,500.

Baadaye, Septemba 6, aliondoka Kinshasa kuelekea Congo-Brazzaville. Alipitia Brazzaville, Gamboma na Oyo, ambapo Septemba 14 alikamilisha hatua yake ya 71 baada ya kusafiri kilomita 98 kutoka Gamboma hadi Oyo.

Mpango wake ulikuwa kuendelea kutoka kaskazini mwa Congo-Brazzaville kwenda Cameroon na baadaye kuelekea Morocco, lakini safari hiyo ilikatishwa na ajali iliyotokea karibu na Ouesso.

Masaïsaï pia alikuwa tayari amefanya safari nyingine kubwa mwaka 2025, alipounganisha Goma na Cape Town nchini Afrika Kusini kwa Baiskeli, akipitia Rwanda, Tanzania, Zambia, Botswana na Namibia.

Kifo chake kimeacha safari ya Pedals for Peace ikiwa haijafikia mwisho wake wa Rabat, huku mradi huo ukiwa umeunganisha michezo na ujumbe wa amani aliokusudia kuufikisha kwa jamii mbalimbali alizokutana nazo katika safari yake.

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa hadi sasa, maelezo kamili kuhusu mazingira ya ajali hiyo bado hayajawekwa wazi na mamlaka za eneo hilo. Iliripotiwa awali kwamba taarifa za kifo chake zilikuwa zikisubiri uthibitisho rasmi, kabla ya vyanzo vya DRC kuthibitisha tukio hilo.

"Tangu tumeanza kushirikiana na Urusi ,tumekuwa na maendeleo makubwa tofauti na awali, kwetu sisi Urusi ni rafiki wa kwe...
09/21/2026

"Tangu tumeanza kushirikiana na Urusi ,tumekuwa na maendeleo makubwa tofauti na awali, kwetu sisi Urusi ni rafiki wa kweli, hawana tamaa, kwa sababu biashara baina yetu inazingitia faida kubwa kwa Burkina Faso hasa katika sekta za madini na wananchi wetu wanaliona hilo, kwa sababu maendeleo hayajifichi"

- Ibrahim Traore, Rais wa Burkina Faso.

Toa maoni yako

IRAN YASEMA HORMUZ ITABAKIWA FUNGA HADI TRUMP NA NETANYAHU WAONDOLEWE MADARAKANI.Mshauri wa kisiasa wa Kiongozi Mkuu wa ...
09/21/2026

IRAN YASEMA HORMUZ ITABAKIWA FUNGA HADI TRUMP NA NETANYAHU WAONDOLEWE MADARAKANI.

Mshauri wa kisiasa wa Kiongozi Mkuu wa Iran, Mojtaba Khamenei, Mohammad Baqer Zolqadr, amesema Iran haitafungua tena Mlango wa Hormuz hadi Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu waondolewe madarakani.

Zolqadr ametoa kauli hiyo wakati mvutano kati ya Iran, Marekani na Israel ukiendelea, huku Mlango wa Hormuz ukiwa kitovu cha mzozo kutokana na umuhimu wake katika usafirishaji wa nishati duniani. Imeripotiwa kuwa Iran, kwa uhalisia, imeufunga njia hiyo tangu kuanza kwa vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Serikali ya Iran (IRNA), Zolqadr amesema: “Wapiganaji wetu hawatafungua Mlango wa Hormuz hadi watakapomshusha kutoka kwenye kiti cha madaraka Trump huyo Mhalifu na Netanyahu huyo mwenye kiu ya damu.”

Kauli hiyo inaongeza uzito wa msimamo wa Tehran kuhusu mustakabali wa njia hiyo muhimu ya majini, ambayo hupitisha sehemu kubwa ya biashara ya mafuta na gesi duniani.

Wakati huo huo, juhudi za kidiplomasia za kutafuta njia ya kumaliza vita zinaendelea. Rais Trump amesema Marekani inaweza kuwa inakaribia mwisho wa vita hivyo na amedai kuwa amezungumza moja kwa moja na upande wa Iran, ingawa Tehran haijathibitisha kuwa mazungumzo ya moja kwa moja yameanza tena.

Mzozo kuhusu Mlango wa Hormuz umeendelea kuwa moja ya masuala makuu yanayozuia kurejea kwa utulivu katika eneo la Mashariki ya Kati, huku mataifa mbalimbali yakihofia athari zake kwa usafirishaji wa mafuta, biashara ya kimataifa na bei za nishati.

Toa maoni yako

MAREKANI KURUHUSU WAJUMBE WA IRAN KUHUDHURIA MKUTANO MKUU WA UN NEW YORK.Marekani imesema itaruhusu ujumbe wa Iran, ukiw...
09/21/2026

MAREKANI KURUHUSU WAJUMBE WA IRAN KUHUDHURIA MKUTANO MKUU WA UN NEW YORK.

Marekani imesema itaruhusu ujumbe wa Iran, ukiwemo ujumbe wa ngazi ya juu unaoongozwa na Rais wa Iran, kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Mjini New York wiki ijayo, licha ya vita kati ya Marekani na Iran kuingia katika mwezi wake wa saba.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani amesema uamuzi huo umetokana na wajibu wa Marekani k**a nchi mwenyeji wa Umoja wa Mataifa.

“Kwa kuzingatia wajibu wetu k**a nchi mwenyeji, ujumbe mkuu wa utawala wa Iran utaweza kuhudhuria Wiki ya Ngazi za Juu ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa,” Msemaji huyo alisema.

Chanzo kinachofahamu suala hilo kimethibitisha kuwa ruhusa hiyo itamhusisha pia Rais wa Iran.

Mkutano huo wa kila mwaka unatarajiwa kuwakutanisha Viongozi na Wawakilishi wa nchi mbalimbali duniani Mjini New York, huku mzozo wa kijeshi kati ya Washington na Tehran ukiwa miongoni mwa masuala yanayoweza kutawala mijadala ya kimataifa.

Toa maoni yako

Saudi Arabia yakabiliwa na uhaba wa makombora ya ulinzi, yaomba msaada wa dharura kutoka kwa washirika.Saudi Arabia imea...
09/19/2026

Saudi Arabia yakabiliwa na uhaba wa makombora ya ulinzi, yaomba msaada wa dharura kutoka kwa washirika.

Saudi Arabia imeanza kutafuta msaada wa kijeshi kutoka kwa mataifa washirika baada ya akiba yake ya makombora ya kuzuia mashambulizi ya anga (interceptors) kupungua, huku mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani kutoka kwa Wahouthi nchini Yemen yakiendelea kuongezeka.

Kwa mujibu wa ripoti ya AP, Riyadh imewaomba Ufaransa, Uingereza, Pakistan na Misri kusaidia kwa kupeleka mifumo ya ulinzi wa anga katika eneo hilo ili kukabiliana na mashambulizi kutoka kwa Wahouthi na makundi mengine yanayoungwa mkono na Iran.

Hatua hiyo inakuja wakati Saudi Arabia ikikabiliwa na shinikizo kubwa la kulinda vituo vyake vya kijeshi, miundombinu muhimu ya serikali pamoja na miundombinu ya mafuta dhidi ya mashambulizi ya anga.

AP imeripoti kuwa ombi la Riyadh limechochewa pia na hali ya Marekani, ambayo ni mshirika mkuu wa Saudi Arabia na muuzaji wake mkubwa wa silaha, ambapo akiba ya makombora ya kuzuia mashambulizi nayo imepungua baada ya miezi kadhaa ya vita na Iran.

Hata hivyo, hadi sasa hakuna kati ya mataifa hayo manne iliyotangaza hadharani kwamba imekubali kupeleka msaada wa kijeshi nchini Saudi Arabia. Msemaji wa Waziri Mkuu wa Uingereza amethibitisha kuwepo kwa ushirikiano wa karibu wa kiulinzi kati ya London na Riyadh, lakini hakusema iwapo Uingereza imepokea ombi rasmi la msaada wa kijeshi.

Ripoti ya Reuters pia inaonyesha kuwa Washington imekuwa ikisita kutoa uingiliaji wa moja kwa moja wa kijeshi, huku ikitoa zaidi msaada wa kijasusi. Hali hiyo imeifanya Riyadh kutafuta washirika wengine huku mashambulizi ya Wahouthi yakiongezeka.

Mzozo huo umeongeza wasiwasi kuhusu usalama wa miundombinu ya mafuta ya Saudi Arabia na usafirishaji katika Bahari ya Shamu (Red Sea), wakati Wahouthi wakiendelea kuongeza mashambulizi katika eneo hilo. Reuters imeripoti pia kuwa Wahouthi wamepata mafanikio ya kijeshi katika maeneo muhimu karibu na Mlango wa Bab el-Mandeb, njia muhimu ya kimataifa ya usafirishaji wa mafuta na bidhaa.

Wakati huo huo, juhudi za kidiplomasia zinaendelea. AP imesema Oman na Misri zinaongoza juhudi za kupunguza mvutano nchini Yemen, huku Saudi Arabia ikijaribu kuzuia mzozo huo usipanuke zaidi na kuhatarisha usalama wa nishati na biashara katika eneo la Mashariki ya Kati.

Saudi Arabia sasa inakabiliwa na changamoto mbili kwa wakati mmoja, kuongezeka kwa mashambulizi ya Wahouthi na kupungua kwa akiba ya makombora ya kuzuia mashambulizi ya anga wakati mshirika wake mkuu, Marekani, pia akabiliwa na upungufu wa silaha hizo.

Toa maoni yako

Address

411 Sheppard Court
Bowling Green, KY
42101

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Vibration tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Vibration tv:

Shortcuts

Share