Locha Media

Locha Media Ukurasa Rasmi wa Locha Media | Follow
(1)

Shirikisho la Soka la Uholanzi (KNVB) limeripotiwa kuanza mazungumzo na kocha raia wa Hispania, Roberto Martínez, kuhusu...
08/12/2026

Shirikisho la Soka la Uholanzi (KNVB) limeripotiwa kuanza mazungumzo na kocha raia wa Hispania, Roberto Martínez, kuhusu uwezekano wa kumteua kuwa kocha mpya wa timu ya taifa.

Kwa mujibu wa De Telegraaf, Martínez amekuwa mmoja wa majina mapya yaliyoibuka katika mchakato wa kutafuta mrithi wa Ronald Koeman, aliyeondoka kwenye nafasi hiyo baada ya Uholanzi kutolewa katika hatua ya 32 bora ya Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Morocco kwa mikwaju ya penalti.

Ripoti zinaeleza kuwa Nigel de Jong, ambaye ni mkurugenzi wa soka wa KNVB, amefanya mazungumzo na Martínez kuhusu uwezekano wa kocha huyo kurejea kwenye kazi ya ukocha wa timu ya taifa.

Martínez mwenye umri wa miaka 53 amewahi kuiongoza Ubelgiji na Ureno, hivyo ana uzoefu mkubwa wa kusimamia timu za taifa katika mashindano makubwa ya kimataifa.

Sponsored by

Kwa mujibu wa Reuters, tukio moja lilitokea katika Ghuba ya Oman, huku shambulio jingine likiripotiwa katika eneo la Bab...
08/12/2026

Kwa mujibu wa Reuters, tukio moja lilitokea katika Ghuba ya Oman, huku shambulio jingine likiripotiwa katika eneo la Bab el-Mandeb, lango la kuingia Bahari ya Shamu. Maeneo hayo ni muhimu kwa usafirishaji wa mafuta na bidhaa duniani.

Katika tukio la Bab el-Mandeb, shambulio linalodaiwa kufanywa na Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran dhidi ya meli ya mizigo Tihamah liliua wafanyakazi wanne wa meli pamoja na waokoaji wawili wa Yemen, huku wengine wakijeruhiwa. Wahouthi wamedai kuwa meli hiyo ilikuwa imebeba vifaa vya kijeshi vya Saudi Arabia.

Wakati huo huo, jeshi la Marekani liliripoti hatua dhidi ya meli ya mizigo yenye bendera ya Panama katika Ghuba ya Oman, likisema meli hiyo ilikiuka zuio la majini la Marekani dhidi ya bandari za Iran.

Iran nayo imesisitiza kuwa Mlango wa Hormuz hautafunguliwa kikamilifu hadi Marekani itimize masharti yake, yanayohusisha masuala ya vikwazo, mali zilizogandishwa na kusitishwa kwa hatua za kijeshi dhidi yake.

Hali hiyo imeongeza hofu kuhusu usalama wa usafirishaji wa mafuta duniani. Reuters imeripoti kuwa idadi ya meli zinazopita katika Mlango wa Hormuz imepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na mvutano huo.

Licha ya Rais wa Marekani Donald Trump kutoa kauli mbalimbali kuhusu uwezekano wa kufikiwa kwa makubaliano, hadi sasa hakuna makubaliano ya mwisho yaliyofikiwa, huku mashambulizi mapya yakifanya matarajio ya kumalizika kwa vita kuwa magumu zaidi.

Sponsored by

08/12/2026

Mashabiki wamebaki wakishangaa baada ya Daliwonga kuonekana akiwa na mwili wenye misuli zaidi kwenye show yake ya hivi karibuni.

Inaonekana gym imeanza kulipa

Sponsored by

08/12/2026

Wapenzi wawili kutoka Uingereza Em na Sam wamewasili jijini Nairobi baada ya kukamilisha safari ya kipekee ya barabarani yenye urefu wa takribani kilomita 23,000 kutoka London nchini Uingereza hadi Kenya.

Safari hiyo, waliyoifanya chini ya jina “The Adventure Way,” imechukua jumla ya siku 222, huku wawili hao wakipitia nchi mbalimbali za Ulaya kabla ya kuendelea na safari yao kupitia mataifa kadhaa barani Afrika.

Katika safari yao Em na Sam walikabiliana na mazingira na maeneo mbalimbali yenye changamoto wakivuka baadhi ya maeneo magumu ya Afrika huku wakisafiri kwa njia ya barabara kuelekea Afrika Mashariki.

Wawili hao walitumia Toyota Land Cruiser katika safari hiyo, wakitegemea uimara wa gari hilo katika kuvuka umbali mrefu na maeneo ya mbali ambayo mara nyingi yalikuwa na changamoto za usafiri.

Sponsored by

08/12/2026

video inayowaonyesha wakiwa juu ya magodoro ndani ya Ziwa Tanganyika, wakieleza hali yao baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama.

Kwa mujibu wa taarifa zinazosambaa, watu hao walinusurika baada ya kutumia magodoro k**a njia ya kujihifadhi juu ya maji, huku wakielea kwa takribani siku nne katika eneo la mwambao wa Tanzania.

Sponsored by

Mabingwa wa UEFA Champions League Paris Saint-Germain (PSG) wanakutana na mabingwa wa UEFA Europa League, Aston Villa, k...
08/12/2026

Mabingwa wa UEFA Champions League Paris Saint-Germain (PSG) wanakutana na mabingwa wa UEFA Europa League, Aston Villa, katika mchezo wa UEFA Super Cup leo, Jumatano, Agosti 12, 2026, kwenye Stadion Salzburg nchini Austria.

PSG wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa mabingwa watetezi wa UEFA Super Cup baada ya kulitwaa taji hilo mwaka 2025. Kikosi cha Luis Enrique kinalenga kuongeza taji lingine la Ulaya katika kipindi ambacho klabu hiyo imeendelea kujijengea historia katika soka la bara hilo.

Sponsored by

Kocha wa Manchester City Enzo Maresca, ameripotiwa kumtaja kiungo wa Chelsea, Enzo Fernández k**a moja ya chaguo lake ku...
08/12/2026

Kocha wa Manchester City Enzo Maresca, ameripotiwa kumtaja kiungo wa Chelsea, Enzo Fernández k**a moja ya chaguo lake kuu katika mpango wa kuimarisha safu ya kiungo ya timu hiyo.

Hatua hiyo inakuja wakati Manchester City ikijiandaa kwa mabadiliko katika eneo la kiungo, huku kukiwa na taarifa kwamba Rodri yuko kwenye mazungumzo ya juu kuhusu uwezekano wa kuhamia Barcelona.

Hata hivyo dili la kumsajili Fernández halitarajiwi kuwa rahisi. Chelsea imeweka bei ya Euro milioni 120 kwa kiungo huyo wa Argentina.

Chelsea pia iko tayari kumhifadhi Fernández iwapo Manchester City haitafikia dau linalokidhi thamani waliyoweka.

Sponsored by

08/12/2026

Ahmed Ally anakwambia kuwa Fei toto akitua ndani yako ili nipate klabu ya Simba basi tamasha la Simba Day litarudiwa ili amtambulishe upya.

Sponsored by

08/12/2026

Msichana aliyekuwa sehemu ya kipindi cha 20v1 cha Drake amegusa hisia za wengi baada ya kumueleza mama yake kuhusu zawadi aliyopata kutoka kwa msanii huyo.

Wakati wa kipindi hicho cha kuchagua wachumba, msichana huyo alishinda na Drake akamwambia angeweza kuomba chochote k**a zawadi yake.

Badala ya kuomba kitu kwa ajili yake mwenyewe, msichana huyo alimfikiria kwanza mama yake na dada zake, akizingatia mambo ambayo mama yake amefanya kwa ajili yao.

Hatimaye alimuomba Drake amsaidie kumnunulia mama yake nyumba.

Sponsored by

08/12/2026

Mwanamke mmoja ameripotiwa kuhama kutoka jimbo moja kwenda jingine baada ya kudai kuwa alikuwa akifuatiliwa mara kwa mara na mwanaume.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyosambaa mtandaoni mwanamke huyo aliamua kuhamia jimbo jingine akiamini kuwa hatua hiyo ingemsaidia kupata usalama na kuanza maisha mapya.

Hata hivyo inadaiwa kuwa baada ya kuhamia eneo hilo jipya, mwanaume huyo alifanikiwa kumpata tena na kuonekana katika mlango wa nyumba yake.

Sponsored by

Address

Houston Tx
Houston Tx, TX

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Locha Media posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share