12/25/2025
Askofu wa Kanisa la Uamsho la Moravian Tanzania, Emmaus Mwamakula, amesema kuwa kumsh*taki Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima, kwa Papa ni sawa na kuwash*taki Maaskofu Katoliki wote wa Tanzania.
Askofu Mwamakula ametoa kauli hiyo katika mahojiano maalumu na Jambo TV jijini Dar es Salaam, akisisitiza kuwa Padri Kitima anatekeleza majukumu yake k**a Katibu Mkuu aliyeteuliwa na Baraza la Maaskofu, hivyo maoni na kauli zake ni kwa niaba ya TEC nzima.
Ameeleza kuwa wito wa baadhi ya watu wanaodai Papa achunguze utendaji wa Padri Kitima kimsingi ni sawa na kumtaka Papa aunde k**ati ya kuwachunguza Maaskofu wote wa TEC, wakiwemo Kardinali Polycarp Pengo, Kardinali Protase Rugambwa na viongozi wengine wa Kanisa Katoliki nchini.
Kwa mujibu wa Askofu Mwamakula, hoja hiyo inaonyesha kutoielewa vizuri mfumo wa uongozi wa Kanisa Katoliki, ambapo Katibu Mkuu hafanyi kazi binafsi bali chini ya maamuzi na mwelekeo wa Baraza la Maaskofu.