Habari za UN

UNKiswahili (Habari za UN), ni ukurasa rasmi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, inayolenga kukuletea habari kuhusu kazi za Umoja wa Mataifa na mashirika yake kote duniani. Tunakuletea habari kutoka makao makuu mjini New York, Marekani, halikadhalika kutoka mashinani kupitia waandishi wetu wa habari walioko katika baadhi ya nchi wanachama, pamoja na washirika wetu, ikiwemo radio na blogu.

06/25/2019
Tunayojifunza UN, tunayapeleka Tanzania yanatekelezwa-Mbunge

Mbunge kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi Riziki Lulida anaeleza wanavyonufaika baada ya kuhudhuria mikutano ya Umoja wa Mataifa. Ni kandoni mwa mkutano wa 12 wa nchi wanachama wa mkataba wa haki za watu wenye ulemavu, CRPD, uliofanyika mapema mwezi huu wa Juni, 2019 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani.

Viana mpo? Hapa ni nchini Guinea-Bissau vijana wakivua samaki kutoka kwenye vizimba vya samaki vinavyoelea. Katika kila ...
06/24/2019

Viana mpo?

Hapa ni nchini Guinea-Bissau vijana wakivua samaki kutoka kwenye vizimba vya samaki vinavyoelea. Katika kila mzunguko wa uvuaji wa kizimba kimoja, vijana wanavua takribani samaki 90,000 sawa na tani 22.5 na kwa mwaka ni tani 45 za samaki.

Shirika la chakula na kilimo duniani, @FAO limewasaidia kupata stadi za uvuvi huu endelevu.

PICHAL ©FAO/Mamadou Sene

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema huu ni wakati wa mabadiliko , na kizazi chacke kimeanza kuelewa...
06/23/2019

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema huu ni wakati wa mabadiliko , na kizazi chacke kimeanza kuelewa kwamba vijana wanaweza na wanapaswa kushika usukani .
Guterres ameyasema hayo Jumapili mjini Lisbon Ureno katika hotuba yake ya kufunga mkutano wa kimataifa wa mawaziri wa vijana wa mwaka 2019 mkutano ambao ni jukwaa la Lisbon+21. Katika jukwaa hilo la siku mbili amesisitiza kuwa “huu ni wakati wa mabadiliko ya jinsi gani Umoja wa Mataifa unashughulikia masuala ya vijana lakini pia umuhimu wao na mchango wao katika kusongesha mbele ajenda ya maendeleo SDGs

Ili kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, #SDGs, serikali na asasi za kiraia duniani kote zinahimizwa kuzijumuhisha...
06/21/2019

Ili kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, #SDGs, serikali na asasi za kiraia duniani kote zinahimizwa kuzijumuhisha na pia kuzishirikisha jamii za watu wa asili katika mikakati ya kitaifa na kimataifa ya ajenda hiyo ya #2030

Pichani ni mwanamke kutoka jamii ya #Ndebelee akiwa katika soko la #Kwadlaulate Afrika kusini mnamo tarehe 01/01/1985

06/21/2019
Machafuko yalazimisha watoto 600,000 kukosa elimu Cameroon:

Zaidi ya asilimia 80 ya shule zimefungwa katika majimbo ya Kaskazini Magharibi na Kusini magharibi mwa #Cameroon kufuatia machafuko yanayoendelea na kulazimisha zaidi ya watoto 600,000 kukosa fursa ya elimu, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto #UNICEF.

06/21/2019
Sehemu ya 7 filamu ya lazarus

Katika sehemu hii ya saba, mapambano ya #lazarus na wengine ya kupigania haki za watu wenye #ualbino yamewakilishwa katika #Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Côte d'Ivoire (MINUCI) ulianzishwa baada ya kupitishwa kwa azimio 1479 tarehe 13,M...
06/20/2019

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Côte d'Ivoire (MINUCI) ulianzishwa baada ya kupitishwa kwa azimio 1479 tarehe 13,Mei mwaka 2003 na Baraza la Usalama kuwezesha utekelezaji wa Mkataba wa Linas-Marcoussis kati ya pande kinzani katika mgogoro nchini humo.
Baraza la usalama liliidhinisha uanzishwaji wa ujumbe huo mdogo kusaidia na kusimamia masuala ya kisiasa, kisheria, usalama wa raia wakati wa uchaguzi.
Pichani ni wakimbizi nchini Cote D'ivore katika kambi ya Guiglo wakisubiri mgao wa chakula tarehe 03 Septemba 2003

06/20/2019
Sehemu ya 6 film ya Lazarus

Baada ya #Lazarus mwanamuziki mweye #ualbino katika Sehemu ya 5 kuelezea kilichomsukukuma kufanya muziki.
katika Sehemu hii ya 6 #Lazarus amefanikiwa kwa mara ya kwanza kuzungumza na #IKPONWOSA- ERO ambaye ni mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu ualbino.
Je nini kilichojiri katika mazungumzo hao? endelea kutazama.

#Wanajeshi wafurushwa katika moja ya shule ambako walikuwa wamepiga kambi nchini #Sudan kusini baada ya mamlaja kuika...
06/19/2019

#Wanajeshi wafurushwa katika moja ya shule ambako walikuwa wamepiga kambi nchini #Sudan kusini baada ya mamlaja kuikabidhi shule kwa #wizara ya #elimu kwajili shughuli za wanafunzi. #MINUSCA
Picha ya maktaba ya #UN.

06/19/2019
Filamu ya Lazarus sehemu ya 5

#Filamu kuhusu maisha ya #Lazarus, mwanamuziki wa #Malawi mwenye #ualbino inazidi kupamba moto na kusisimua wengi.
Kuanzia sehemu ya kwanza tumeshuhudia maisha na changamoto zake, kiasi kwamba kuna wakati alinusurika kuuzwa kwa wauaji.
Katika sehemu hii ya 5, #Lazarus anaeleza kilichomsukuma kwenye #muziki, lakini kwa mara ya kwanza unapata nafasi ya kumsikiliza mke wake. Endelea…

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS na wadau wake wanalenga kuyaondoa majeshi na wapiganaji wa nchi h...
06/18/2019

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS na wadau wake wanalenga kuyaondoa majeshi na wapiganaji wa nchi hiyo kutoka katika maeneo ya raia ili kuweka mazingira mazuri kwa wananchi wanaorejea katika maeneo yao huko Upper Nile.

#Pichayasiku inamwonesha askari akihamisha 'virago' vyake kutoka katika shule ambayo askari walipageuza kuwa makazi yao.

Picha: UNMISS / Isaac Billy

06/18/2019
Filamu ya Lazarus sehemu ya 4

Huu ni mwendelezo wa filamu ya #Lazarus, mwanamuziki mwenye ualbino kutoka #Malawi.
Baada ya kuponea kusafirishwa Tanzania na watu wenye nia mbaya katika sehemu ya 3, #Lazarus katika sehemu ya 4 amefanikiwa kumpata mfadhili ambaye ni muaandaji wa #muziki kutoka #Ulaya ambaye amejitolea kurekodi ya nyimbo zake.

Uliruka kamba? Unakumbuka hata nyimbo ambazo ulipenda zaidi kuimba ukiruka kamba? Hili ni zoezi tosha lakini sasa ni nad...
06/17/2019

Uliruka kamba? Unakumbuka hata nyimbo ambazo ulipenda zaidi kuimba ukiruka kamba? Hili ni zoezi tosha lakini sasa ni nadra kuona watoto wakicheza mchezo huu!

Hapa ni Haiti watoto wakiruka kamba kwenye mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince.

PICHA: UN /Logan Abassi

06/17/2019
Watu wenye ulemavu wakumbukwe katika suala la utalii-Mbunge Tanzania

Mkutano wa 12 wa nchi wanachama wa mkataba wa haki za watu wenye #ulemavu, #CRPD, ukiingia wiki yake ya pili hii leo katika Makao Makuu ya #UmojawaMataifa mjini #NewYork, #Marekani, wadau wanaendelea kujadili mikakati mbalimbali ya kuhakikisha ahadi ya kutomwacha yeyote nyuma inatekelezwa kama anavyosimulia #UN #TANZANIA

06/15/2019
Filamu ya Lazarus sehemu ya 3

Huu ni mwendelezo wa filamu ya Lazarus, mwanamuziki mwenye ualbino kutoka Malawi. Baada ya kumpata meneja na muziki wake kuanza kujulikana katika sehemu ya pili, sasa sehemu ya tatu utapata kusikililiza kisa kilichomkuta Lazarus wakati watu wasiojulikana walijaribu kumsafirisha kwenda
Tanzania kwa nia ya kumuua na kuuza viungo vyake.
Endelea kuuatilia kwa undani zaidi.#Lazarus #Malawi #Ualbino

Wakimbizi washinda mbio za nyika au maratoni ya kilomita 10 huko Geneva Uswisi, kwa kushika nafasi ya kwanza, pili, n...
06/14/2019

Wakimbizi washinda mbio za nyika au maratoni ya kilomita 10 huko Geneva Uswisi, kwa kushika nafasi ya kwanza, pili, nne na tano .
Domnic Lokinyomo Lobalu ambaye ni mshindi wa kwanza amesema kuwa ushindi huo umewapa matumaini ya kushiri mashindano ya Olimpiki huko Tokyo 2020 ya mwaka ujao wakati timu ya wakimbizi itakaposhindana.
Picha kwa hisani ya UNHCR/Bernard Rono

06/14/2019
Filamu ya Lazarus sehemu ya pili

Katika sehemu ya kwanza ya filamu hii ilionyesha simulizi kuhusu maisha ya Lazarus, ambaye ni mwanamuziki mwenye ualbino nchini Malawi.
Na Katika Sehemu ya pili hii Lazarus amefanikiwa kumpata meneja ambaye atamsaidia kumtangaza na pia kuufanya muziki wake uwafikie wengi. Je nini kilichotekea alipoalikwa kuimba kwenye tamasha lake kubwa la kwanza?
Fuatilia kwa undani zaidi.#Lazarus #Malawi #Ualbino

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio kulikubali taifa la kenya kuwa mwanachama wa kudumu wa Umoja w...
06/13/2019

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio kulikubali taifa la kenya kuwa mwanachama wa kudumu wa Umoja wa Mataifa.mnamo tarehe 16 desemba 1963.

Siku hiyo ya kiistoria ilifanya Kenya kuwa mwanachama rasmi wa 113 wa Umoja wa Mataifa .

Pichani kusho ni Balozi Adlai Stevenson, mwakilishi wa kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani wa Kenya hayati Oginga Odinga, baba mzazi wa Raila Odinga .

Picha kwa hisani ya maktaba ya Umoja wa Mataifa.

06/13/2019
Filamu imenitoa hofu, sasa watu wengi wanafahamu shida zetu- Lazarus

Leo ni siku ya kimataifa ya uelimishaji kuhusu ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi ikibeba kauli mbiu "Bado tunasimama imara" ikihimiza jamii kuwajumuisha watu wenye ulemavu wa ngozi na kuwalinda kwani wana haki na wanamchango. Miongoni mwa watu hao ni Lazarus Chigwandali, mlemavu wa ngozi kutoka Malawi ambaye sasa anatumia kipaji chake cha ameomba kuwepo kwa mfuko wa kujengea uwezo watu wenye ulemavu wa ngozi barani Afrika ili waweze kushiriki kwenye shughuli za kiuchumi na hatimaye kujiongezea kipato na kujikwamua kimaisha. #ALBINO #ULEMAVUWANGOZI #HAKIZABINADAMU

06/13/2019
Filamu ya Lazarus sehemu ya kwanza

Filamu hii ni maisha ya Lazarus Chigwandali , mlemavu wa ngozi mkazi wa Lilongwe, nchini Malawi ambaye mara kadhaa amenusurika kuuawa na watu wanaoamini ushirikina wa viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi.
Lazarus anatumia gitaa lake kuburudisha watu na kubadili mtazamo wa jamii kuhusu watu wenye ulemavu wa ngozi.
Hii ni sehemu ya kwanza ya filamu inayohusu maisha yake. Kaa tayari mwendelezo wa filamu kesho. #Lazarus #Ulemavuwangozi #Malawi

Elimu haina ukomo, hata kama hukupata fursa ya kusoma bado unanafasi ya kujiendeleza ilimradi una uzima.Pichani ni wanaw...
06/12/2019

Elimu haina ukomo, hata kama hukupata fursa ya kusoma bado unanafasi ya kujiendeleza ilimradi una uzima.

Pichani ni wanawake wanaosomeshwa kupitia programu ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini #Mali #MUNISMA iliyoanzishwa kuwakwamua wanawake katika mji wa #Gao kuendeleza elimu,
Picha kwa Hisani ya UN Photo/Harandane Dicko

06/12/2019
Ulemavu sio sababu ya kubweteka na kutofanya vizuri maishani

Ummy Nderiananga, mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu nchini Tanzania SHIVYAWATA, katika mahojinano na Idhaa ya Umoja wa Mataifa New York ametoa wito kwa jamii, serikali na mashirika kuwajuimisha watu wenye ulemavu katika maendeleo endelevu. #SHIVYAWATA #Tanzania #UmmyNderiananga

06/12/2019
Ulemavu si kulemaa. Nirishiriki mafunzo ya jeshi-Ummy Nderiananga

Mkutano wa 12 wa nchi wanachama wa mkataba wa watu wenye ulemavu, CRPD umeng'oa nanga leo Juni 11, 2019 kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Ummy Nderiananga ambaye ni Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu nchini Tanzania SHIVYAWATA anaeleza changamoto alizopitia lakini bila kukata tamaa.

Wakati mkutano wa kimataifa wa watu wenye ulemavu ukiendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Mare...
06/11/2019

Wakati mkutano wa kimataifa wa watu wenye ulemavu ukiendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani, Katibu Mkuu Antonio Guterres ametoa wito wa kutomuacha mtu nyuma kwa kuwajumuisha kikamilifu watu wenye ulemavu katika maendeleo endelevu.

Pichani ni mashindano ya mbio ya watu wenye ulemavu jijini Monrovia, nchini Liberia
Picha kwa hisani ya UN

06/11/2019
Tunataka dijitali iwe na manufaa na si kuleta matatizo-Nanjira

Nanjira Sambuli mjumbe wa jopo la Umoja wa Mataifa la kuhakikisha hakuna anayesalia nyumba katika zama za kidijitali hasa kwa nia ya kusongesha mbele ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu au SDGs pia ni meneja wa masuala ya será katika mfuko wa kimataifa, world wide web Foundation akizungumza na Flora Nducha kandoni mwa mkutano wa jopo hilo la ngazi ya juu baada ya kuwasilisha ripoti yao kwenye Baraza Kuu, anaeleza kazi ya jopo na pia faida ya dijitali katika kusongesha maendeleo.

Zaidi ya walinda amani 70 katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan UNMISS hujitolea kila jumamosi kuwatembelea wat...
06/10/2019

Zaidi ya walinda amani 70 katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan UNMISS hujitolea kila jumamosi kuwatembelea watoto yatima katika vituo mbalimbali katika mji wa Juba.
Baadhi ya kazi ambazo wanazifanya katika vituo hivyo ni pamoja na usafi,kuandaa chakula kwa ajili ya watoto na pia kucheza nao.
Pichani ni mfano wa mlinda amani akimpa mtoto juisi.
Picha kwa hisani ya UNMISS

Wasio nacho wafungua milango kwa wakimbizi huku wenye nacho "wakihofia" ni aibu- JolieWakati idadi ya wakimbizi na waham...
06/09/2019

Wasio nacho wafungua milango kwa wakimbizi huku wenye nacho "wakihofia" ni aibu- Jolie

Wakati idadi ya wakimbizi na wahamiaji kutoka Venezuela imefikia milioni 4, mjumbe maalum wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Angeline Jolie amesema kinachohijika hivi sasa ni utu na ubinadamu kuliko wakati wowote kwa watu ambao wana hofu ya kuwajibika kuonyesha uongozi katika kusaidia wakimbizi.

Bi. Jolie amesema hayo baada ya kutembelea Colombia na kushuhudia wimbi la wakimbizi wa Colombia wanaorejea nchini humo kutoka Venezuela sambamba na raia wa Venezuela wanaosaka hifadhi nchini humo kutokana na sababu za kiuchumi, kijamii na kisiasa nchini mwao.

Kupitia taarifa iliyotolewa na UNHCR huko Geneva, Uswisi, mjumbe huyo maalum amesema “ni jambo la kipekee kuona Colombia, ambayo yenyewe inakabiliwa na changamoto nyingi, imeonesha utu kwa kusaidia wavenezuela wanaokimbia kwao. Napenda kutambua ujasiri wao, uthabiti na mnepo wa wananchi wa Colombia.”

06/08/2019
Teknolojia ni muhimu katika uhifadhi wa kumbukumbu za kitamaduni

Carson Kibet kijana kutoka jamii wa watu wa asili Endorois nchini kenya katika mahojiano na Grace Kaneiya wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anaeleza umuhimu wa uhifadhi wa kumbukumbu ya jamii yake kwa kutumia teknolojia ya kisasa. #Endorois #CarsonKiburo #Kenya #GlobalIndigenousYouthCaucus

Hata mbuyu ulianza kama mchicha! Mashindano ya kombe la dunia la soka kwa wanawake yakiwa yameanza leo huko Ufaransa, t...
06/07/2019

Hata mbuyu ulianza kama mchicha!

Mashindano ya kombe la dunia la soka kwa wanawake yakiwa yameanza leo huko Ufaransa, tunakupeleka Mutwanga,jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kuangazia mechi hii iliyochezwa kati ya walinda amani kutoka Nepal na timu ya wanawake kutoka Mutwanga.

PICHA:MONUSCO Michael Ali.

06/07/2019
kukwamua vijana lazima taasisi, mashirika na serikali wafanye kazi pamoja

Katika mahojiano na Grace Kaneiya ya Idhaa ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Walter Mong'are ambaye ni Naibu Mkurugenzi wa masuala ya vijana Ofisi ya nchini kenya ameeleza nini kifanyike ili vijana wanufaike katika ajenda ya maendeleo andelevu ya mwaka 2030. #SDG #WalterMongareSr #kenyaPresidency

#PichayaSikuKazi na dawa! Unasemaje? Kutoka maktaba yetu tunakurejesha mwaka 2004. Pichani ni walinda amani kutoka Seneg...
06/06/2019

#PichayaSiku

Kazi na dawa! Unasemaje? Kutoka maktaba yetu tunakurejesha mwaka 2004.

Pichani ni walinda amani kutoka Senegal wakiwa nchini Cote d'Ivoir wakti baraza la usalama lilimamua kuanzisha operesheni za ulinzi wa amani kwa kipindi cha miezi 12 kuanzia Aprili 4, 2004. Hap ni katika kambi ambayo bado ukarabati wake unaendelea eneo la San Pedro.

Picha UN Photo/Eskinder Debebe 05/08/2004

06/06/2019
Kuna maambuziki zaidi ya milioni 1 ya magonjwa ya zinaa kila siku :WHO

Kiwango cha kimataifa cha maambukizi ya magonjwa ya zinaa (STI) kinapaswa kuwa kengele ya kuziamsha serikali , wameonya leo wataalam wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya afya wakibainisha takwimu zinazoonyesha kwamba mtu mmoja kati ya 25 leo ana moja ya maradhi ya zinaa yanayotibika ambayo hutokea katika kiwango cha maambukizi zaidi ya milioni moja kwa siku.#STI #STD #VVU #Magonjwayazinaa

Address

405 East 42nd Street
New York, NY
10017

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Habari za UN posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Habari za UN:

Videos

Nearby media companies


Other Media/News Companies in New York

Show All