Adventist Review Swahili

  • Home
  • Adventist Review Swahili

Adventist Review Swahili Karibu kwenye ukurasa wa Facebook wa Gazeti la Adventist Review Kiswahili. Note the Sign-up button at the top right of this page.

This Page is your connection to the Kiswahili Edition of the Adventist World Magazine. The magazine is delivered digitally for mobile devices on a WhatsApp Channel, free to subscribers in East and Central Africa, and around the world. The Kiswahili Adventist World Magazine contains translations of the English articles, plus up to 25% original Kiswahili material. Other devotional material is also a

vailable on the WhatsApp Channel, such as the Grace Notes by Bill Knott, Editor in Chief of the Adventist Review Ministries. This material is also easy to share with others, via WhatsApp. Here you will find posts highlighting the latest articles in the magazine. Inbox us if you have any question, or let us know which articles you have enjoyed. We’d love to hear from our subscribers/readers. Don’t forget to “like” this page

Agosti 2025Utangulizi unazungumzia wazo hatari la kumtegemea mchungaji mmoja kufanya kila kitu. Kanisa halipaswi kusubir...
01/08/2025

Agosti 2025
Utangulizi unazungumzia wazo hatari la kumtegemea mchungaji mmoja kufanya kila kitu. Kanisa halipaswi kusubiri mtu mmoja kutekeleza kile ambacho Mungu amekiagiza kifanywe na mwili wote wa waumini kwa pamoja.

Kuhusu kurudi kwa Kristo mara ya pili, mada hii imeelezewa katika makala za “Roho ya Unabii” pamoja na makala kuu ya “Ufufuo wa Kiroho”.

Makala ya “Sauti Yenye Uhakika” inaeleza kwamba tunapaswa kupiga tarumbeta ya onyo kuwa Yesu anakuja upesi, lakini tarumbeta hiyo lazima iwe na sauti iliyo wazi na yenye maana! Sauti ya tumaini na maandalizi – si ya hofu na uzushi.

Tunazungumzia pia umuhimu wa kutoisahau huduma ya kuwakaribisha wageni katika makala ya “Ukarimu wa Nyakati za Mwisho” (Eschatological Hospitality).

Bofya hapa kusoma toleo la Agosti 2025
https://send-it.me/go/ARAgosti2025

Fikia maktaba ya kidijitali yenye majarida yote ya Adventist Review kwa kubofya kiungo kilicho hapa chini.
https://bit.ly/ARSwahiliLibrary

Makala Maalum: Kurudi kwenye Kiini cha Utume Wetu Kuanzisha kwa makusudiNa Boyan Levteroy Boyan Levteroy anatukumbusha k...
20/06/2025

Makala Maalum: Kurudi kwenye Kiini cha Utume Wetu

Kuanzisha kwa makusudi
Na Boyan Levteroy

Boyan Levteroy anatukumbusha kuwa vuguvugu la awali la Waadventista halikuhusu tu kukuza makanisa mahalia. Lilikuwa ni vuguvugu la kufanya wanafunzi na kuanzisha makanisa. Wanafunzi wapya walitumwa k**a wainjilisti kwa jamii mpya, miji, nchi, na hata mabara. Leo hii makanisa mengi ambayo yanaangazia maslahi yao binafsi yamedumaa au yanadorora, ilihali yale ambayo yamechukua kuanzisha makanisa k**a mkakati wao wa kuwafikia wengine yanakua na kongezeka. Makala hii maalum inahimiza kurudi kwenye kiini cha utume wetu na kuanzisha kwa kusudi.

Bofya hapa ili kuisoma makala hiyo.
https://send-it.me/go/AWJuni2025?page=16

Mtazamo wa Kiulimwengu: Mwito Mkuu Sasa ndio wakatiNa Ted N.C. Wilson Ted Wilson anaandika kuhusu jinsi sasa ndio wakati...
13/06/2025

Mtazamo wa Kiulimwengu: Mwito Mkuu

Sasa ndio wakati
Na Ted N.C. Wilson

Ted Wilson anaandika kuhusu jinsi sasa ndio wakati wa mwito mkuu wa kumwabudu Mungu k**a Muumba wetu. Uhusikaji wa Washiriki Wote Ulimwenguni (TMI) ni kuhusu kila mtu, kila mahali, kushiriki ujumbe wetu tuliopewa na Mungu kwa ulimwengu. Umeitwa, umechaguliwa na Mungu Mwenyewe, kuwafikia wengine kwa ajili Yake.

Bonyeza hapa ili kuisoma makala hiyo
https://send-it.me/go/AWJuni2025?page=13

Fokasi: Kuuelewa Ujumbe wa Malaika Watatu Injili na ujumbe wa onyoNa Thomas R. Shepherd Makala hii inaangazia ujumbe wa ...
06/06/2025

Fokasi: Kuuelewa Ujumbe wa Malaika Watatu

Injili na ujumbe wa onyo
Na Thomas R. Shepherd

Makala hii inaangazia ujumbe wa malaika wa onyo la wokovu na kuangamizwa. Tunaitwa ili kurudi kwa Mungu au tuangamie milele, kwa sababu ibada ya uongo itaangamiza maisha yako. Mungu anatutaka tuliskie onyo hili na kuokolewa.

Bofya hapa ili kusoma makala hiyo
https://send-it.me/go/AWJuni2025?page=11

Toleo hili linaangazia “Kuuelewa ujumbe wa Malaika Watatu” na linaeleza kuwa tunapaswa kutii ujumbe wa onyo ili tuweze k...
30/05/2025

Toleo hili linaangazia “Kuuelewa ujumbe wa Malaika Watatu” na linaeleza kuwa tunapaswa kutii ujumbe wa onyo ili tuweze kuokolewa. Makala maalum “Kurudi kwenye Kiini cha Utume Wetu”, inatuhimiza kurudi kwenye kiini cha utume wetu na kuanzisha makanisa tukiwa na kusudi.

Kwenye makala “Kifungoni, Ng’ambo ya kifungo”, Vicki Funk anaelezea mpango wa Mungu usiotarajiwa wa kumtumia katika huduma za magereza.

Kisa chetu cha Afya na Uzima kinaelezea ni kwa nini mazoezi ya kila mara ni muhimu kwa afya ya kimwili na kiakili, na “Uaminifu Unalipa” kinaelezea kisa cha keshia mwaminifu aliyerudisha senti 45 ambazo zililipishwa zaidi na matokeo yake yalikuwa chanya.

Bofya hapa ili kusoma Toleo la Juni 2025 la hivi karibuni
https://send-it.me/go/AWJuni2025

Ifikie maktaba ya mtandaoni ambapo magazeti yote ya AW yanahifadhiwa kwa kubofya kiungo kilicho hapo chini.
https://bit.ly/AWSwahiliMagazineLibrary

Kutazama Nyuma: “Ujasiri wa Kusonga Mbele” Unaoungwa Mkono na Waumini Kisa cha Redio ya Waadventista Ulimwenguni Na Alle...
23/05/2025

Kutazama Nyuma: “Ujasiri wa Kusonga Mbele” Unaoungwa Mkono na Waumini

Kisa cha Redio ya Waadventista Ulimwenguni
Na Allen Steele Pamoja na watumishi wa AWR

Makala hii inaelezea jinsi Redio ya Waadventista Ulimwenguni ilianza na kuchukua hatua ya “Ujasiri wa Kusonga Mbele” ili kupanua huduma na eneo inapofika redio kwa kutafuta uungwaji mkono wa washiriki wa kanisa. Waliungwa mkono na waumini.

Bofya hapa ili kusoma makala hiyo
https://send-it.me/go/AWMei2025?page=14

Makala Maalum: Kutupwa Chini Lakini Kutoangamizwa Mungu ni mkuu zaidi ya kizuizi chochote ambacho tunaweza kukutana nach...
16/05/2025

Makala Maalum: Kutupwa Chini Lakini Kutoangamizwa

Mungu ni mkuu zaidi ya kizuizi chochote ambacho tunaweza kukutana nacho
Na Alicia Marie Harding

Alicia, mmishonari anayehudumu katika Taasisi ya Riverside Farm huko Zambia Pamoja na mumewe Craig, na wanao wanne, anaelezea vizuizi ambavyo timu za uinjilisti na matibabu za Riverside zilipitia wakati wa programu yao kubwa ya kuifikia jamii. Alijua jinsi ambavyo Mungu alijua kile kilichokuwa mbele yao, na maombezi yalikuwa yanaendelea kwa ajili yao hata kabla wajue ni kwa nini. Makala hii inaonyesha jinsi mungu ni mkuu kuliko changamoto yoyote tunayoweza kukabiliana nayo.

Bofya hapa ili kuisoma makala hiyo
https://send-it.me/go/AWMei2025?page=12

Fokasi: Kanisa Linaposononesha Kwa nini ninasalia katika kanisa la Mungu Na Nicole ParkerNicole Parker ni mpinga dhuluma...
09/05/2025

Fokasi: Kanisa Linaposononesha

Kwa nini ninasalia katika kanisa la Mungu
Na Nicole Parker

Nicole Parker ni mpinga dhuluma na ni mke wa mchungaji. Ameshuhudia Wakristo wengi wakikataa dini yenye utaratibu, au hata kupoteza imani kabisa, asili ya uchaguzi wa wengi ikiwa ni kuendewa kinyume na kuumizwa na kanisa. Katika makala “Kanisa Linaposononesha”, anapeana sababu kadhaa kwa nini Yesu anatutaka kusalia katika kanisa Lake, hata inapokuwa vigumu.

Bofya hapa ili kusoma makala hiyo
https://send-it.me/go/AWMei2025?page=11

Mei 2025 Toleo hili linaangazia “Kanisa Linaposononesha” na sababu zinazomfanya Yesu kututaka tusalie kwenye kanisa Lake...
02/05/2025

Mei 2025

Toleo hili linaangazia “Kanisa Linaposononesha” na sababu zinazomfanya Yesu kututaka tusalie kwenye kanisa Lake, hata inapokuwa vigumu.

Tunaangazia “Kusudi la Mungu kwa Kanisa Lake,” na Ted Wilson anazungumzia “mwaliko” anaotupa Mungu na jinsi tunavyopaswa kuwa “Tayari kwa Dhifa ya Harusi” ili “Kristo anapotupatia vazi Lake la haki, vazi zuri . . . tunatakiwa tu kulikubali na kulivaa.”

"Tukio la hadubini” linaonyesha wakati mwafaka wa Bwana kwa ajili ya kliniki ya Cochabamba, na katika kisa chetu cha Afya na Uzima, tunachunguza ikiwa kweli vikoleza sukari visivyo vya asili ni mbadala wenye afya.

Bofya hapa ili kusoma Toleo la Mei 2025
https://send-it.me/go/AWMei2025

Pata maktaba ya mtandaoni ambapo majarida yote yanahifadhiwa kwenye kiungo kilicho hapo chini.
https://bit.ly/AWSwahiliMagazineLibrary

Imani Inayokua: RebaMaombi na wema barabarani Na Cathlynn Doré LawMakala yetu ya Imani Inayokua inasimulia kisa cha “bib...
25/04/2025

Imani Inayokua: Reba

Maombi na wema barabarani
Na Cathlynn Doré Law

Makala yetu ya Imani Inayokua inasimulia kisa cha “bibi”, ambaye, kwenye ziara zake za kila siku, alikutana na kuingiliana na Reba, mbwa ambaye mbweko wake ulikuwa mbaya zaidi kuliko kung’ata kwake. Kisa maalum kinachofunua nguvu ya imani na uwezo wa Mungu wa kuponya.

Bonyeza hapa ili kuisoma makala hiyo
https://send-it.me/go/AWAprili2025?page=21

Mtazamo wa Kiulimwengu: Mwaliko Mzuri ZaidiKuitikia witoNa Ted N C WilsonTed Wilson anajadili “mwaliko” tuliopewa na Mun...
17/04/2025

Mtazamo wa Kiulimwengu: Mwaliko Mzuri Zaidi

Kuitikia wito
Na Ted N C Wilson

Ted Wilson anajadili “mwaliko” tuliopewa na Mungu kwa kunukuu baadhi ya mialiko maarufu ya Biblia - “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha” (Mt. 11:28). Anaendelea kuelezea kuwa mialiko hiyo kwa kweli ni miwili, na kwamba “Mungu ameweka baraka nyingi kwa ajili ya wale wanaoalika wenzao kujifunza Kwake.” Makala hii pia inataja njia nzuri zaidi ambazo Mungu amewasaidia watu wanapokuwa katika mchakato wa kuwaalika wengine.

Bonyeza hapa ili kusoma makala hiyo
https://send-it.me/go/AWAprili2025?page=13

Address

MD

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Adventist Review Swahili posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Adventist Review Swahili:

Shortcuts

  • Address
  • Telephone
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share