
04/29/2025
Papa Francis, kiongozi wa kanisa katoliki duniani na ambaye aliaminika kuwa Papa mwanabadiliko toka Agentina, amezikwa Jumamosi, Aprili 25, 2025 katika kanisa kuu la Mt Maria Major.
Papa Francis ambaye alilitikisa kanisa Katoliki na hasa waumini wanaoshikilia misimamo mikali ya kiimani kwa kuwasikiliza watu wa jinsia moja ndani ya kanisa na kusimamia haki za wahamihaji, alifariki dunia Jumatatu ya Pasaka (Aprili 21, 2025) akiwa na miaka 88.
Mazishi yake yalitanguliwa na maombolezo ya laki kadhaa za waumini ambao walikusanyika Vatikan kuomboleza kifo cha kiongozi huyu aliyependwa na wengi duniani kwa msimamo dhidi ya vita, ubepari, mabadiliko ya tabia nchi na hata kazi zake za kupinga umaskini.
Papa Francis, kiongozi wa kanisa katoliki duniani na ambaye aliaminika kuwa Papa mwanabadiliko toka Agentina, amezikwa Jumamosi, Aprili 25, 2025 katika kanis...