27/08/2024
MUNGU USIKUBALI PART THREE
Mungu usikubali jasho langu kupotelea hewani maana unaibariki kazi ya mikono yangu.
Mungu usikubali nikose pesa za kulipa kodi,caro ya shule na mahitaji yangu ya kila siku.
Mungu usikubali ndoa yangu ikavunjika kwa fedheha na aibu tena maana nishailipia gharama.
Mungu usikubali mawazo maovu yakatawala moyo wangu na akili zangu.
Mungu usikubali nzige waharibu mazao yangu.
Mungu usikubali dhoruba inibebe na mawimbi yake.
Mungu usikubali laana zisizo na sababu kufuata maisha yangu.
Mungu usikubali ibada yangu kwako ikawa kelele mbele zako bali niwie Radhi mwanao.
Mungu usikubali marafiki wanafiki wakapata nafasi katika maisha yangu.
Mungu usikubali mihuri isiyofaa kupigwa katika kurasa za maisha yangu.
Mungu usikubali maombi yangu ya siri yakapotelea hewani bali unijibu kwa wakati unaofaa.