Kite TV kenya

  • Home
  • Kite TV kenya

Kite TV kenya Swahili news channel

 : Rais William Ruto amemteua Erastus Edung’ Ethekon kuwa mwenyekiti mpya wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), baa...
08/05/2025

:
Rais William Ruto amemteua Erastus Edung’ Ethekon kuwa mwenyekiti mpya wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), baada ya mchakato wa usaili uliofanywa na jopo maalum lililoongozwa na Nelson Makanda kati ya Machi 24 hadi 26, 2025.

Ethekon ameteuliwa kutokana na tajriba yake ya kisheria na maono ya kuimarisha uadilifu wa uchaguzi. Uteuzi wake na Makamshina wengine sita sasa unasubiri kuidhinishwa na Bunge la Kitaifa. Kabla YA kuchukua Usukani Rashmi.

www.kitetvkenya.com

 :Kadinali Robert Prevost ametangazwa kuwa Papa mpya.Robert Kardinali Prevost anatokea Chicago nchini Marekani, na hadi ...
08/05/2025

:
Kadinali Robert Prevost ametangazwa kuwa Papa mpya.

Robert Kardinali Prevost anatokea Chicago nchini Marekani, na hadi kuchaguliwa kwake alikuwa akihudumu k**a mkuu wa Dicastery wa kanisa kwa Maaskofu.

Prevost ametumia muda wake mwingi akitumikia nchini Peru, na ana uraia wa Marekani na Peru.

Robert Kardinali Prevost ana umri wa miaka 69. Kwa Sasa atahudumu k**a Papa Wa awamu ya 267.

www.kitetvkenya.com

 : Waumini wa kanisa Katoliki duniani kwa sasa wanaendelea kusherehekea na kuimba nyimbo za shangwe huko Vatican  ya mos...
08/05/2025

: Waumini wa kanisa Katoliki duniani kwa sasa wanaendelea kusherehekea na kuimba nyimbo za shangwe huko Vatican ya moshi mweupe kuonekana ishara ya kupatikana kwa Papa mpya.


www.kitetvkenya.com

AFRIKA KUSINI: Serikali ya Afrika Kusini imefuta pendekezo la kuongeza  ushuru wa thamani (VAT) kwa asilimia 0.5. Pendek...
24/04/2025

AFRIKA KUSINI: Serikali ya Afrika Kusini imefuta pendekezo la kuongeza ushuru wa thamani (VAT) kwa asilimia 0.5.

Pendekezo hilo lilipingwa vikali na chama cha Democratic Alliance (DA), ambacho kilifikisha suala hilo mahak**ani. Vyama vingine vya upinzani pia vilipinga ongezeko hilo.

Uamuzi wa kufuta nyongeza hiyo umetangazwa na Wizara ya Fedha Wa nchi hio Enock Godongwana.

Kulingana na Waziri Wa fedha, amesema kuwa uamuzi huo umetokana na mashauriano na vyama vya kisiasa pamoja na bunge, lakini ikaonya kuwa utaathiri pakubwa mapato ya serikali.

www.kitetvkenya.com

TANZANIA: Tanzania imepiga marufuku bidhaa zote za kilimo kutoka Afrika Kusini na Malawi, kufuatia maamuzi ya awali ya n...
24/04/2025

TANZANIA: Tanzania imepiga marufuku bidhaa zote za kilimo kutoka Afrika Kusini na Malawi, kufuatia maamuzi ya awali ya nchi hizo mbili wa kupiga marufuku uingizaji wa mazao ya Tanzania.

Waziri wa Kilimo wa Tanzania, Hussein Bashe ametangaza hatua hii licha ya kuendelea kwa mazungumzo ya kidiplomasia.

Tanzania imechukua hatua hii ya kulipiza kisasi, baada ya Malawi, kuzuia uingizwaji wa bidhaa kutoka Tanzania k**a unga, mchele, tangawizi na mahindi, huku Afrika Kusini nayo ikizuiwa uingizaji wa ndizi kutoka Tanzania.

www.kitetvkenya.com

 :kampeni za uchaguzi utakaofanyika kesho Jumapili nchini Ujerumani zinatamatika leo .Muungano wa upinzani wa vyama ndug...
22/02/2025

:

kampeni za uchaguzi utakaofanyika kesho Jumapili nchini Ujerumani zinatamatika leo .Muungano wa upinzani wa vyama ndugu vya CDU/CSU unafanya mkutano wao wa mwisho mchana huu mjini Munich.

Kansela Angela Merkel ,na mpinzani wake ,Peer Steinbrück , wamekuwa wakizunguka nchi nzima ya Ujerumani katika juhudu za kutafta kura . Huku wahamiaji wakitarajiwa kupiga Kura Yao ya kwanza hapo kesho.

www.kitetvkenya.com

 Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya waziri wa serikali ya Rwanda, James Kabarebe kutokana na kuunga mkono kundi la waa...
21/02/2025


Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya waziri wa serikali ya Rwanda, James Kabarebe kutokana na kuunga mkono kundi la waasi la M23 linalopigana mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Aidha imemuwekea vikwazo Lawrence Kanyuka Kingston, mwanachama wa M23 na kambi nyingine inayojulikana k**a Muungano wa Mto Congo, pamoja na kampuni zake mbili.

www.kitetvkenya.com

 :Marekani imewasafirisha wahamiaji 177 kutoka kwenye kituo chake cha kijeshi cha Guantanamo, Cuba, na kuwapeleka nyumba...
21/02/2025

:
Marekani imewasafirisha wahamiaji 177 kutoka kwenye kituo chake cha kijeshi cha Guantanamo, Cuba, na kuwapeleka nyumbani kwao nchini Venezuela hapo jana ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya ushirikiano kati ya serikali hizo mbili ambazo zimekuwa na mivutano kwa muda mrefu.

www.kitetvkenya.com

DRC:Serikali ya Kenya kupitia kwa Waziri wake wa Mambo ya Nje,  Musalia Mudavadi imewataka raia wake kuondoka nchini DRC...
21/02/2025

DRC:
Serikali ya Kenya kupitia kwa Waziri wake wa Mambo ya Nje, Musalia Mudavadi imewataka raia wake kuondoka nchini DRC kutokana na kuongezeka kwa ghasia kati ya vikosi vya usalama na waasi wa M23.

Waziri Mudavadi, ameonyesha wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya usalama na kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano mara moja k**a ilivyokubaliwa katika mkutano wa pamoja wa viongozi wa kanda uliofanyika Dar es Salaam, Tanzania, kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)

www.kitetvkenya.com

SUDAN:Serikali ya kijeshi nchini Sudan, hapo jana imemuita nyumbani balozi wake nchini Kenya, kupinga kile imesema Nairo...
21/02/2025

SUDAN:
Serikali ya kijeshi nchini Sudan, hapo jana imemuita nyumbani balozi wake nchini Kenya, kupinga kile imesema Nairobi kuruhusu wapiganaji wa RSF na washirika wao kufanya mikutano ya kuunda serikali mbadala.

Sudan ilimshtumu Rais wa Kenya William Ruto kwa kuchukua msimamo wa kufedhehesha kwa kukubali na kuhimiza njama inayokiuka mamlaka ya Sudan.

www.kitetvkenya.com

 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) nchini Kenya , Wafula Chebukati, ameaga dunia.Amekuwa ak...
21/02/2025


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) nchini Kenya , Wafula Chebukati, ameaga dunia.

Amekuwa akipatiwa matibabu kwa muda kwa ugonjwa ambao bado haujawekwa wazi, tangu baada ya uchaguzi mkuu wa 2022.

www.kitetvkenya.com

 :Marekani imetetea matamshi yaliyotolewa na rais DonaldTrump kuhusu êneo la Gaza, Waziri wake wa mambo ya nje akisema m...
06/02/2025

:
Marekani imetetea matamshi yaliyotolewa na rais DonaldTrump kuhusu êneo la Gaza, Waziri wake wa mambo ya nje akisema mpango wa kuwahamisha wapalestina kutoka Gaza utakuwa ni wa muda.

Utetezi wa Marekani umekuja saa chache baada ya nchi za kiarabu na washirika wa Marekani, akiwemo katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, AntonioGuterres, wakikosoa mpango huu waliosema ni wakibaguzi.

www.kitetvkenya.com

Address


Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kite TV kenya posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Kite TV kenya:

  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share