08/08/2023
MATUMIZI YA MMEA WA MZIWAZIWA
Mmea huu huitwa mziwaziwa kwa sababu hutoa utomvu mweupe unaofanana na maziwa ukiukata shina au jani lake. Leo ninakuletea matumizi muhimu kabisa ya mmea huu k**a ifuatavyo:
1.KUTIBU MACHO
Ukiwa na matatizo ya macho k**a vile kuuma, kuwasha, kuvimba, kuwa mekundu kupita kiasi au kutoa matongotongo kata vishina kazaa vya mmea huu na kisha dondoshea utomvu huo ktk macho hadi utakapoona tatizo hilo limekoma.
2.KUTIBU VIDONDA VYA TUMBO
Ng'oa huo mmea pamoja na mizizi yake uoshe vizuri, kisha upondeponde baada ya hapo weka kwenye maji na uchemshe mpaka ibadilike rangi iwe k**a chai kisha, iache ipoe na utakunywa kikombe kimoja asubuhi,mchana na jioni kwa siku 7 tu
Hakikisha kila siku unatengeneze dawa mpya sio kurudia majani yale yale
3.KUTIBU U.T.I NA FANGASI
Uchemshe na kunywa k**a ilivoelezwa kipengele No.2
4.KUJIFUNGUA KWA WAJAWAZITO
Hapa anaetakiwa kutumia mmea huu ni mama mjamzito ambae siku zake za matazamio ZIMEPITA, yaani kwa yule ambae mimba yake imepitiliza miezi 9 bila kujifungua. Jinsi ya kutumia rejea kipengele No.2 hapo juu
ANGALIZO: Kwa mama mwenye ujauzito wa chini ya mie 9 haruhusiwi kutumia mmea huu.
5.KUTIBU UGUMBA
Kwa wanawake ambao hawashiki ujauzito watumie mmea huu husaidia kupevusha mayai ya k**e na kuleta ute zile siku za kupevuka kwa yai, kwa wale wasiopata ute.Jinsi ya kutumia rejea kipengele No.2 hapo juu
6.KUONGEZA MAZIWA KWA MAMA ANAENYONYESHA.
Kwa wamama wanaojifungua na ikatokea maziwa hayatoki au yanatoka kidogo sana basi watumie mmea huu huongeza uzalishaji maziwa kwa kasi.
Jinsi ya kutumia rejea kipengele No.2 hapo juu